MJUE KWA UNDANI NABII TB JOSHUA.

Nabii TB Joshua.
Kutoka kwenye Moja ya account za mitandao ya kijamii zinazoendeshwa na huduma ya T.B Joshua zimewekwa Picha zinazomuonesha nabii Temitope Balogun Joshua au maarufu kama T.B. Joshua ambaye alizaliwa June 12, 1963 nchini Nigeria na amekua kiongozi wa kanisa kubwa nchini Nigeria lijulikanalo kama The Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) ambapo kanisa hilo pia linaendesha kituo cha televisheni chan Emmannuel TV.
Mtumishi huyu wa MUNGU amehusika katika miujiza mingi na maelfu ya watu wamefunguliwa na kupokea uponyaji kutokana na huduma ya Nabii TB Joshua.
Moja ya Shule alikosomea TB Joshua.
  Nabii T.B Joshua ametokea kujitwalia umaarufu sana katika nchi nyingi za Afrika na barani Ulaya na Asia kwa kutabiri mambo mbalimbali ambayo baadae yalikua yakitokea kweli na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vikubwa na vinavyoheshimika Duniani. 
Nyumbani kwako Tb Joshua, mahali alipozaliwa na kukulia.
Nabii T.B.Joshua amewahi kutunukiwa Nishani kama Officer of the Order of the Federal Republic (OFR) kutoka kwa serikali ya Nigeria mwaka 2008 na pia aliwahi kuchaguliwa kua mtu wa Karne toka kabila la Yoruba nchini Nigeria ambapo alipewa wadhifa huo toka taasisi ijulikanayo kama Pan-Yoruba media outlet Irohin-Odua
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 25
Nabii T.B. Joshua pia amewahi kutambulika kama moja ya watu 50 toka Afrika wenye nguvu ya Ushawishi kwa jamii wadhifa aliopewa na taasis ya Pan-African magazines na pia kumtaja kama moja ya watu maarufu sana Duniani
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 20
Amejulikana sana duniani kupitia mitandao ya kijamiii ambapo T.B. Joshua anatajwa kua na mashabiki wapatao Milion 1,na laki 5 kupitia akaunt ya Facebook na mamia ya video zake zilizopo kwenye mtandao wa Youtube  baadhi ziliwahi kuleta utata sana duniani kutokana na utata wa mambo aliyowahi kutabiri na hatimaye kusababisha mamilion ya watu duniani kuzitafuta hizo video ili wazitazame kwenye mtandao.
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 17
Jarida maarufu la FORBES mwaka 2011 lilimtaja nabii T.B. Joshua kua anashikilia nafasi ya tatu katika wachungaji matajiri zaidi nchini Nigeria akiwa na utajiri unakadiriwa kufikia Dola za kimarekani Milion 10 mpaka 15 (US$ 10-15 million )
Moja ya mikutano ya injili ya TB Joshua huko Mexico
endelea kutembelea blog hii mara kwa mara kazi yangu ni kuhakikisha unahabarika na kupata taarifa mbalimbali kadri zinaponifikia

Comments