MSHTAKI NA MASHTAKA


Na Mchungaji Bryson Lema, Ufufu na uzima Morogoro.

Utangulizi:Katika Kitabu  cha Ayubu 31:35imeandikwa ...[Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu);  Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu! ]…. Unapoyaangalia maisha yako ya kila siku, ikiwemo  ndoa yako,  afya yako, biashara zako n.k. unaweza kukosa majibu, lakini maswali kuhusu kinachotokea yapo pale pale. Ayubu pamoja na kuwa mkamilifu mbele za Bwana,  lakini hata hivyo alijikuta akipata taabu, misiba na mateso mbalimbali bila kujua aliyemshataki ni  nani na mashtaka yake ni yapi.
Bila kuwepo kwa mshataki huwezi kupelekwa mahakama yoyote ile, au  kwa balozi wa nyumba kumi mtaani mwako. Katika Biblia,  shetani anaitwa ni mshataki. Mfano: UFUNUO 12:10…[Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.]…. Unapaswa kufahamu kuwa wewe kama masihi wa Bwana unaye mshtaki, naye ni shetani. Kesi yoyote ile huanzishwa na mshtaki. Kinachofuata ni taratibu za kuwa na polisi na wapelelezi wakiaangalia mashtaka uliyotuhumiwa nayo.
Kwa haraka waweza kuona kuwa mfumo wa serikali za dunia hii umeundwa kwa mpango wa kishetani. Unapoona mshtaki, ujue katika ulimwengu  wa roho yapo mashtaka, mahakimu, mapolisi na mfumo wote wa kimashtaka.  Endapo utashatakiwa huko kwenye Mahakama za kishetani unakuwa umebadilishwa jina na kuitwa ‘mtuhumiwa’. Vita huibuka kwa sababu katika mahakama za kishetani, wanakuwepo walinzi wanaopewa kazi ya kukulinda ili usiweze kusonga mbele. Pengine mshtaki wako anachukizwa tu  na maombi yako hapo mtaani mwako na ambayo yanaharibu kazi zao za giza. Kwa hiyo mwisho wa siku, mashetani yanakuwekea ulinzi usipandishwe cheo au usifanikiwe n.k.  kumbuka yote haya siyo  kwa sababu Bwana hapendi ufanyiwe hivyo bali ni kwa sababu ya uwepo kwa mahakama za kishetani zenye kuwaweka watu magerezani kwao.
Mashetani  yana aina mbali  mbali za vifungo. Wengine hufungwa ili wasipate kazi, na kama hujaifuatilia ile mahakama ya kishetani  yenye kukuhukumu usipate kazi basi hutaweza kufurukuta kamwe. Vifungo vingine ni kwenye ndoa au biashara n.k.

Vifungo vyote hivi huanzia katika ulimwengu  wa roho. Kwani  maandiko matakatifu yanasemaje? Baadhi ya mifano ya Kibiblia ni hii ifuatayo: 

1.      Kumbuka Mungu alimwambia Yeremia “Kabla hujakaa tumboni mwa mama yako nalikujua”. Je, kabla Yeremia hajaingia tumboni alikuwa wapi? Alikuwa katika ulimwegnu wa roho.

2.      Utawaona wale mamajusi wa mashariki, waliokuja Jerusalemu kuifuatilia nyota ya Yesu Kristo alipokuwa amezaliwa. Je, safari ya hawa mamajusi ilikuwa ya siku moja? La hasha. Kumbuka kuwa enzi hizo hazikuwepo ndege za kasi ili  kusafirisha watu kwa haraka namna ile. Maana yake ni kuwa, nyota ya Yesu ilishaonekana pengine miaka mitatu kabla ya Mariamu kuwa mjamzito.  Hii inadhihirisha kuwa hata mafanikio  yako katika ulimwengu wa roho yameshaonekana, na ndiyo maana mashtaka  hupelekwa kwa mashetani ili kukuzuia.

3.      Kumbuka pia kuwa kabla ya Musa kuzaliwa hali ilikuwa shwari. Lakini kipindi kile cha kukaribia kuzaliwa kwa Musa, ndipo Farao na Wamisri walianza harakati za kutaka kuwazuia Israeli wasiondoke wala kuwa na mkombozi wa kuwavusha kwenda kwenye nchi yao ya ahadi.
Inapokaribia wakati wakuondoka hapo ulipo kwenda asehamu iubngunbe vita  huchachamaa, na washtaki hukaa kila  upande ili kukuzuia. Hii ni  kwa sababu katika mahakama za kishetani hiyo hujulikana mapema tu. Kumbuka kuwa kila jambo na wakati wake. Mungu ameuweka wakati wako wa kuinuliwa. Wakati huu ukeshasogea, mashtaka na vita huongezeka.

DANIELI 6:4-5…[Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake. 5 Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake.]….Washtaki wa duniani nao hukaa ili kutafuta makosa. Nguvu ya mshtaki iko kwenye mashtaka. Inabidi ujue  kuwa pale msalabani ulipata msamaha wa dhambi zako na hati zote za mashtaka zilifutwa.
Vipoaina mbili za vifungo.kifungo  cha ndani na kifungo cha nje. Kifungo cha ndani shetani  hukaa ndani ya mtu. Huyu  akiombewa mapepo ndani mwake hutoka.  Kifungo cha nje ndicho kigumu sana kwa sababu shetani hakai ndani ya mtu, ila huweka vizuizi mahali. Mathalani, mtu wa aina hii hata akiombewa halipuki  mapepo kwa sababu mapepo hayapo ndani mwake. Badala yake, mapepo ya kumlinda yapo nje ya mwili wake  ili kuzuia  na kusimamia aina hii ya kifungo alichowekewa mtu huyu. Mathalani,  mtu amehukumiwa katika mahakama za kishetani ili apate ajali na miguu yake ikatwe, na hivyo mtu wa aina hii apatapo ajali miguu yake itakatwa kwa sababu ya hukumu iliyoamuriwa.
Leo ni siku ya kumfuatia mshatka na mashtaka yake. Kila adui aliyensihtaki, leo nakupiga wewe na washtaki wako wote. Lazima ieleweke kuwa wewe una mamlka kuliko yeye. Sisi tunaye mwakili ambaye ni Yesu Kristo aliyetupa uwezo waw kuangusha kila kazi ya kishetani. Imeandikwa “wewe ni rungu la Bwana na silaha za Bwana za vita”.  Adui zangu  mnaponiwangia nyakati za usiku na kupita angani, tutakutana huko huko,ila tofauit yangu na ninyi ni kuwa  kwenu muda huo huo kama mwali wa moto, kwa kuwa imeandikwa  Bwana huwafanya watumishi wake kuwa miale ya moto”. Leo siji kwenu kama mwanakondoo tena, bali ninakuja kwenu kama mwali wa moto. Ule ukristo wa kupigwa shavu la kulia na kugeuza uso ili upigwe shavu lingine ulishapitwa na wakati kwa sababu kizazi hiki kimezidi uovu kupitiliza.  Leo nitakupiga wewe mchawi na mkoba wako wa uchawi. Nitaidondosha minyororo mliyonifunga kwa miali yangu ya moto. Mlikuja kwangu na mikuki na silaha zenu lakini mimi nakuja kwenwana wa Majeshi.
Wengi wa watu hawjui manuizo. Kwa kawaida manuizo si shetani  bali ni nguvu ya kishetani. Mfano, shetani anaweza kuweka hali fulani ya kishetani na ambayo huwa  katika kifungo ili kwamba mtu awe na maisha wanayotaka wao. Kama uonavyo wafungwa magerzani, pia wapo wakristo waendao makanisani lakini ni wafungwa na wapo magerezani bila wao kujua. Wakienda makanisani huridhika waambiwapo, “Nendeni kwa amani” na kumbe warudipo majumbani mwao,  bado maisha yao, ndoa zao, na kila wakifanyacho vimewekewa kuta ambazo haziwaruhusu kupita. Lazima uffahamu kuwa,  tatizo ulilo nala ni gereza la kishetani. Wallinzi wa kusimamia haya mashtaka hukuzuia pande zote ili mtu  wa aina hii asiweze kupenya. Leo hii tunaye Yesu Krsito na malaika wa vita ili kufuatilia kila aina za kuta na vizuizi vilivyowekwa na mashetni,na ni lazima nipite kwa Jina la Yesu.
Mashtaka ya kishetani huongeza kwa sababu yamenuiziwa nguvu  za kishetani. Pengine mashtaka yako yansema ‘Hakikisha haolewi’, ‘Hakikisha ndoa yake haina amani’  ‘Hakikisha watoto wake hawasomi’  ‘Hakikisha hafanikiwi kwenye biashara yake’ n.k. Wasimamizi wa mashtaka hukaa mkao wa kuhakikisha kuwa, kile kilichonuizwa juu yako kinatokea vilevile.
Shetani anapokushtaki huandikisha hati ya mashtaka.  Imeandikwa katika 1 NYAKATI 4:33…[na vijiji vyao vyote vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya nasaba yao wanayo.]…  Hati ya nasaba ni sawa na kusema vinasaba (DNA). Hii ni hati ya damu ya mtu husika. Kwakawaida hayupo mtu anayeweza kumshaatki mtu au kumchhukua msuskule asiyekuwa na damu naye. Unaweza kufungwa kwa sababu yupo mtu aliyekamata hati ya nasaba ya ukoo wako. Katika mila  za kiafrika, mzee waukoo anakuwepo mwenye umri mkubwa kuliko wote na ambaye mara zote hata akienda waganaga wa kienyeji huenda  kwa niaba watu wa ya ukoo  wote. Baba wa ukoo afanyapo haya haendi kama yeye  bali kama mkuu wa ukoo wake.

Pengine hujawai hujiuliza maswali haya: Ni kwa nini  baadhi  ya  makabila Tanzania  huwasimika viongozi wa kisiasa na kuwafanya machifu wa kabila lao, na kuwapa mkuki, ngao na kuvishwa ngozi za wanyama? Fahamu ya kuwa kwa kawaida, uchifu hautolewi bila kufanyika kafara. Maana yake ni kuwa, kafara za wanyama hufanywa kabla ya kiongozi mhusika kusimikwa kuwa chifu na makabila husika. Maana yake ni kuwa, kiongozi wa aina hii, hutenda mambo kwa  niaba ya kabila lile alilosimikwa kuwa chifu wao.
Vifungo vya rohoni vipo vya aina nyingi sana. Vingine ni vya kifamilia, vingine ni  vya ukoo wako, vingine vya serikali yako ya mtaa, au jimbo  lako au vilivyosababishwa na rais wa nchi yako. Ukumbuke kuwa kila utawala huanzia rohoni kabla ya kudhihirishwa mwilini.  Leo ni lazima uazimie kujitoa katika magereza mliyoniweka kwa Jina la Bwana.  Leo ni lazima tutoke kwenye mashtaka yao na kwa kila jambo la kishetani walilonifanyia kwa Jina la Yesu. Hata hivyo, endapo mtu  hujaokoka siyo  rahisi kuweza kumshinda mshataki wa maisha yako. Ni vyema leo kufanya maamuzi ya kuokoka kwa kumwamini Yesu Kristo ili  awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

Comments