NDUGU USINUNUE MOTO KWA PESA YAKO.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Namshukuru MUNGU wa mbinguni kwa neema hii.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

1 Kor 10:14-15 '' Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. '' 

-Biblia inatuamuru tuikimbie ibada ya sanamu. ibada ya sanamu ni pamoja na kutambika, kusujudia sanamu, kuabudu sanamu, unajimu, kuabudu majini, kuabudu wafu, usoma nyota, uganga wa kienyeji au kwa jina lingine wanaita tiba mbadala, waabudu shetani, rushwa  na kila jambo ambalo halitokani na MUNGU wa mbinguni.  Ibada ya sanamu inajumuisha vitu vingi sana.
Biblia inatuonya kuikimbia ibada ya sanamu kwa sababu wanaofanya ibada ya sanamu wako kinyume na BWANA YESU.
Wanadamu wengi bado wametekwa na machukizo, kuna wengine hata hutumia vipato vyao kununua moto kwa kufanya dhambi.
Ona mfano hai huu wa watu wa Sodoma na Gomora.

Yuda 1:7 ''Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.'' 


-Huu ni mfano tu wa waasi. Haya yameandikwa ili kutuonya sisi tuliofikiwa na zamani hizi.
Lakini wanadamu wengi katika zamani hizi hata hawana habari kama kuna adhabu ya milele kwa watenda dhambi. 
-Wanadamu wa leo Wa Ajabu Sana. 
-Kuna Watu Wako Tayari Kununua Moto Kwa Pesa Zao Wakati Uzima Wa Milele Upo Na Unapatikana Bure.
- Kuna Watu Hununua Jehanamu Kwa Pesa Zao Kwa Kwenda Kwa Waganga Wa Kienyeji. 
-Kuna Watu Hununua Jehanamu Kwa Pesa Zao Kwa Kulipia Gesti Ili Afanye Uzinzi. 
-Kuna Watu Hununua Moto Kwa Pesa Kwa Kutoa Mimba.
-Kuna Watu Hununua Moto Kwa Pesa Zao Kwa Kununua Pombe.
- Kuna Watu Hununua Jehanamu Kwa Pesa Zao Kwa Kwenda Disko Kumshangilia Shetani Na Wanaye. 
-Kuna Watu Hununua Jehanamu Kwa Pesa zao Kwa Kusema Uongo Baada Ya Kupewa Pesa. 
-Kuna Watu Hununua Moto Kwa Pesa Kwa Kutoa/kupokea Rushwa. 
Ndugu yangu kama unahusika na dhambi yeyote geuka leo na kutubu kwa MUNGU kupitia YESU KRISTO naye atakusamehe na kukupa haki ya  uzima  milele. Kama umewahi kununua moto kwa Pesa zako basi okoka leo na pesa zako hizo tumia kununua Biblia na vitabu ili ujifunze Neno la MUNGU, Tumia pesa hizo kwa kusapoti kazi ya MUNGU ili watumishi waende kuhubiri injili ya KRISTO ulimwenguni pote. Ndugu unayetumia Pesa zako kununua moto au kununua jehanamu bado hujachelewa, nakuomba geuka leo na kutubu na BWANA YESU atakupokea.

Ni Hatari Na Ajabu Mwanadamu Ananunua Moto Kwa Pesa Zake Ilihali Mbingu Ipo Na Inapatikana Bure Bila Kutoa Hata Senti 5. BWANA YESU Anaokoa Na Ukimpokea Leo Bure Unaokoka Na Huko Ndiko Kununua Uzima Wa Milele Bure.

Yohana 3-16-21 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU.''
-Kwa kusudi la ajabu sana BWANA YESU alikuja ulimwenguni ili wewe na mimi tusiende jehanamu.
yawezekana kabisa matendo yako yanakupeleka jehanamu lakini kama ukitubu leo na kumpokea BWANA YESU hakika wewe unakuwa wa mbinguni na sio motoni.
Kumpokea YESU ni kuupokea uzima wa milele na kuendelea kumkataa YESU ni kuukataa uzima wa milele.

 Matendo 4:12 ''Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ''

-Hakuna  uzima wa milele kwingine nje na BWANA YESU, ndugu mkimbilie leo na utakaa salama.
 -Ndugu, Leo Ndio Yako Itumie Kwa Kuokoka Maana Kesho Haijulikani Kama Ni Yako Au Sio Yako. 
-BWANA YESU Yuaja Na Atamlipa Kila Mwanadamu Sawa Na Matendo Yake. yeye BWANA YESU anasema 

 '' Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. Mimi YESU nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi. Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.-Ufunuo 22:12-17 ''

 Kuna Magari Mawili Yanayosafiri. Gari La Kwanza Linaelekea Mbinguni Na Gari La Pili Linaelekea Kuzimu. Kila Mwanadamu Yuko Katika Mojawapo Wa Magari Haya. Tiketi Na Siti Kwenye Gari Uliyopo Ni Matendo Yako. Gari La Mbinguni Kiongozi Wake Ni BWANA YESU KRISTO Na Gari La Motoni Dereva Ni Shetani. Nakushauri Kupanda Gari La Mbinguni Na Sio Gari La Jehanamu. 
 Kama Umepanda Gari La Motoni Hakikisha Unashuka Fasta Na Kama Umepanda Gari La Mbinguni Kwa Raha Zako Anza Na Kunywa Maji Ya Ujazo Wa ROHO, Hata Mimi Tuko Pamoja Kwenye Safari Ya Mbinguni Maana KRISTO Na Neno Lake Ni Ndio Katika Ndio Kwangu. 
BWANA YESU anasema 

''Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.-Mathayo 11:6'' 

 

KAMA UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO UKAJIUNGE NA KUANZA KUISHI MAISHA MATAKATIFU.

''BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele zako mimi mwenye dhambi, lakini leo nimetambua kosa langu na naomba unisamehe dhambi zangu zote, nisamehe dhambi ninazozikumbuka na pia zile ambazo sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike jina langu katika kitabu cha uzima. Neno lako katika Warumi sura ya 10 Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu '' . BWANA YESU mimi nimekuamini leo na hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na hakika nimeokoka. Kuanzia leo Naufunga ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa matendo mema na matakatifu. BWANA nipe ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda dhambi na anasa zote za dunia. Kuanzia leo mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU mwenye haki zote. ninafuta laana zote na kila roho ya shetani inayonifuatilia naiharibu kwa jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU linavyosema katika Yeremia sura ya kwanza mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana kwa kuniokoa. Yote haya kwa imani nimepokea na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU kunitumia. Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea Amen.
Kama umetubu toba ya kweli hakika wewe kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine. ulishindwa kumpokea BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments