SAUTI YA BARAGUMU

Na Mchungaji Mkama, Ufufuo na uzima Kigoma.

Ni sauti inayotangaza watu kufunguliwa na kuwa huru kutoka kwenye vifungo vya ibilisi sauti iliyosikiwa na manabii kwenye kisiwa cha patimo leo ni lazima tuyaambie mapepo yaliyotumwa ili kutuzuia katika maisha yetu, tunayaambia kwa sauti ya Baragumu; wana Israel walipiga kele ya Baragumu hadi ukuta wa yeriko ukaanguka na waliopo kwenye mashimo watakwenda kusikia sau
UFUNUO 11:15 Malaika wa saba akapiga Baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu zikisema ufalme wa BWANA wetu na wa kristo wake naye atamiliki hata milele.
Leo ipo sauti ya Baragumu ili ule ugonjwa uliokusumbua uuambie kwa yatosha tunakwenda kuyaambia nyamaza tunasonga mbele, hata ulete majambazi au polisi hatutanyamaza maana wamewekwa watu wa Mungu ili waseme kwa sauti ya Baragumu tuko kwenye kipindi cha malaika anayepiga Baragumu.
UFUNUO 11:13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile na waliosalia wakaingiwa na hofu wakamtukuza Mungu wa mbinguni
Sehem ya kumi ya mji wa kigoma ya mji wa kasulu tunaikomboa na kuilejesha, sehem ya kumi ya maisha yetu lazima itoke kwenye shimo la kuzimu, wengine wanaweza wakawa unaingia nao kanisani unasema nao BWANA Yesu asifiwe au utukufu lakini hao hao ndio wameshikilia sehemu yako ya mafanikio, sehemu ya kwanza hadi ya kumi iliyokufunga lazima iangamie kwa jina la Yesu.
YONA 2:5-7 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu, vilindi vilinizunguka mwani ulikizinga kichwa changu nalishuka hata pande za chini za milima hiyo chini na mapingo yake yalinifunga hata milele, lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee BWANA Mungu wangu.
Wale wanaoishi katika dunia ndio wanaoweza kukufunga wakaao katika dunia ambao upande wao wameutegemeza kwa shetani lakini leo tunawaambia waachie kwa jina la Yesu leo kwa sauti ya Baragumu lazima wachawi waachie sehemu yetu maana Yesu alisema yeye ni samba wa kabila la yuda. Ile vita iliyopiganwa mbinguni aliyepigana na joka alikuwa ni Yesu na ndiye aliyemtuma malaike apige Baragumu watu wafunguliwe, jehanamu ni hasira ya Mungu maana ndiye anampiga shetani, unapotaka kuuona ufalme wa Yesu wewe endelea kusonga mbele hata wakwambie sisi ni freemason usikate tamaa maana sisi siyo wakwanza hata yasu walimwambia anatoa pepo kwa beli-zebubu. Nabii YONA alisema amefungwa na nguvu za dunia ambazo wanaokaa ndani ya dunia ndio wanaweza kumfunga mtu kutokufikia mafanikio yake wanaipeleka sehemu yake ya mafanikio kwenye shimo la kuzimu.
KUTOKA 15:14-17 Kabila za watu wamesikia wanatetemeka wakaao ufilisti utungu umewashika.ndipo wajumbe wa dedomu wakashangaa watu wa moabu wenye nguvu tetemeko limewapata watu wote wakaao kanaani wameyeyuka. Hofu na wofa umewaangukia kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe hata watakapovuma watu wako Ee BWANA hata watakapovuma watu wako uliowanunua.utawaingiza na kuwapanda katika mlima wa urithi wako mahali pale ulipojifanyia Ee BWANA ili upakae pale patakatifu ulipopaweka imara BWANA wa mikono yako
Mungu anaponyoosha mkono wake juu ya watesi na maadui zetu upande wa manefili upande wa wafilisiti maandiko yanasema utungu unawashika maana BWANA anatangaza kwa sauti ya Baragumu, Asimamaye mbele yako kukuzuia au nyuma yako kukushika mwambie sikuogopi maana BWANA yukopamoja nami, wale wachawi wanaokutesa utungu unawashika maana BWANA ananyoosha mkono wake juu ya mfilisti anayejiinua. Leo wachawi wanaposikia tunapita tunaelekea kwenye Baraka zutu tunaamuru tetemeko liwashika wanatuma majambazi wanapeleka sumu lakini BWANA alitujua tangu tumboni mwa mama zetu na ametuweka juu ya mataifa aliyetuwekea sanda katika ulimwengu wa roho tunaivua kwa jina la Yesu. Kila aliye kinyume na mimi akaye kama jiwe na hofu imshike kwa jina la Yesu ili maadui wajue ipo sauti ya Baragumu inayonena ili kufungua watu.
ZABURI 59:12-13 Kwa dhambi ya kinywa chao na kwa neno la midomo yao wanaswe kwa diburi chao kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao, uwakomeshe kwa hasira uwakomeshe watoweke wajue ya kuwa Mungu atawala katika yakobo na hata miisho ya dunia,
Unaweza ukachukua maneno yale yale wanayonuiza juu yako ukamwambia Mungu waingie wenyewe, maana wachawi wanaposhidwa mipango yao ya rohoni wanaweza wakakujia mwilini lakini tumepewa mamlaka juu ya pepo wabaya, mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka wala madhara hayatatupata hata ukute wamepasua vyungu wewe kemea kwa jina la Yesu. Maandiko yanasema hakuna jaribu ambalo halina mlango wa kutokea na hakuna jaribu linalokuja zaidi ya kiwango chako cha imani labda Mungu awe anahitaji kufanya kitu cha tofauti juu ya maisha yako. Adui wanatakiwa wajue anayetawala ndani yako yupo mpaka miisho ya dunia wajue anayekulinda yupo pamoja na wewe, anayetawala ndani yako akisema neno linakwenda kutendeka kama ulivyosema na kiasi cha imani ulicho nacho kinaweza kusaidia uwaambie wanaokuzuia wakae kimya kiwango cha imani kikiwa kama punje ya haradani unao uwezo wa kuuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini ni lazima tuwasimamishe wachawi wawe kama mawe nasi tupite katikati yao sauti ya Mungu imekwisha kutamka waanguke mbele yako, uliyekwisha kuokoka umetangaza vita na anayepigana siyo wewe yuko pembeni yako anakutuma maana wakuu wa dunia wamekwisha kuanguka

YONA 4:5-7 Ndipo YONA akatoka mjini akaketi upande wa mashariki wa mji akajifanyia kibanda huko akakaa chini yake uvulini hata aone mji ule utakuwaje, na BWANA Mungu aliweka tayari mtango akaufanya ukue juu ya YONA ili uwe kivuli juu ya kichwa chake na kumponya katika hali yake mbaya basi YONA akafurahi sana kwa sababu ya ule mtango lakini siku ya pili kulipopambazuka Mungu akaweka tayari buu nalo likautafuna ule mtango ukakatika.
Watesi wetu wanapokuwa wametengeneza mambo yao wanakaa pembeni ili kuangalia yanayotokea, Mungu analitazama kanisa wachawi wanakutazama wewe ili waona waliyokufunga nayo wanakuangamiza lakini maandiko yanasema iko huruma ya Mungu ambayo anahurumia hadi wanyama. Wachawi wameketi pembeni ili waone tunavyoangamia kama YONA alivyokaa pembeni ili kuona kitakachotokea kwenye mji wa ninawi, mwambie Mungu wamekaa pembeni yangu ili wayaone waliyonifanyia.

Comments