Na Pastor Bryson Lema, Ufufuo na uzima Morogoro. |
Utangulizi:Tunaposema
silaha, wengi wetu wanawaza sime,
bunduki, mishale n.k. Mwindaji anapokuja kwako, huja akiwa na silaha. Imani yake
mwindaji ni kuwa, kwa silaha aliyoibeba, wewe hutapita. Hata hivyo, Mungu wetu naye ameandaa silaha. Tatizo kubwa hapa
ni kuwa, silaha ya Mungu haionekani, kwa sababu Mungu wetu hubadilisha kitu
kulingana na matumizi. Mungu akimaua
kugeuka sime,anafanya hivyo.
AMOSI
3:5..[Je!
Ndege ataanguka mtegoni juu ya nchi, mahali asipotegewa tanzi? Mtego utafyatuka
juu ya nchi, bila kunasa kitu cho chote?]…. Hii ina maana kuwa, umuonapo ndege
kanaswa katika mtego, ujue kuna aliyeutega. Kila kitu na mtego wake, na kila
silaha na mtu wake. Mtego wa ndege haumasni swala, na mtego wa swala haumnasi
nyani.
Katika maisha
ya kawaida, ipo mitego na pia wapo wawindaji.
Katika Biblia, shetani anaonekana akizuia Ibrahimu asipate uzao kupitia
Sarah, kwa kuwa alishajua kupitia uzao wa Ibrahimu Baraka za Mungu zitafuatana
na uzao wake. Shetani alitengeneza silaha za kumzuia Ibrahimu kupata motto, bila
yeye na mkewe kujua. Mwishowe, baada ya
kukata tama kwa muda mrefu, hatimaye alipata mtotoo aitwae Isaka. Hata hivyo
Isaka naye alipitia kipindi kigumu kama hiki cha Ibrahimu, kwa sababu tumbo la
mkewe nalo lilifungwa asizae.
Hata uhai ulio
nao ni sehemu ya miujiza. Kumbuka kuwa, Bwana amekupitisha katika nyakati usizozijua na kukuepusha na mitego
mingi sana ya wawindaji. Kila jambo
ulionalo maishani mwako lina sababu yake. Kwa kadiri unavyopiga hatua za maisha
yako, ujue kuna ………….
Kupitia Isaka,
shetani aliwachonganisha Yakobo na Esau. Kupitia Yakobo, shetani alisababisha
asimuoe Raheli kwa sababu alishaona ndani
ya tumbo la Raheli angepatikana Yusufu, yaani mkombozi wa wana wa
Israeli, atakayewaokoa wasife kwa njaa. Hata baada ya Yusufu kuzaliwa, shetani alitengeneza mipango mibaya ili
Yusufu asifikie ndoto zake. Yusufu alitengenezewa mipango mibaya, pale ndugu
zake walipomuuza kwa wafanyabiashara wa Kimisri. Kumbuka lengo la shetani
siyo Yusufu auzwe Misri bali auae na afe. Hata Yusufu alipokuwa Misri,
bado shetani aliendelea kuandamwa na shetani kiasi kwamba alitupwa gerezani, na
hapo ikawa ndio mwisho wa ndoto zake.
Yusufu akiwa
gerezani, ndiposa Farao akota ndoto ambayo haikupata mtafsiri bali kwa kupitia
kwa Yusufu peke yake. Yusufu alipotoka gerezani alienda moja kwa moja kuwa
mtawala wa nchi ya Misri. Bwana atafungua mlango kwako
Baada ya
Yusufu kuimaliza kazi yake ya ukombozi, alilala na baba zake. Mwanzoni mwa
Kitabu cha Kutoka, habari za Mfalme mpya wa Misri asiyemjua Yusufu zinaelezwa. Kila vita husimama kwenye kila hatua. Wazalishaji wa Kimisri
wanaelekezwa wasiachie Waisrael kujifungua salama, na ikitokea hivyo,
watoto wa kiume wote wauae‼ kumbe
aliyekuwa anawindwa hapa ni Musa,
ili Israeli wasipate mtu wa
kuwaongoza watoke utumwani. Hata wazazi wa Musa nao walishindwa jinsi ya kumlinda, na kuazimia kumweka kando ya
mto na papo hapo Bwana akatengeneza njia
ya kumuokoa. Kumbe basi, wanaddamu hufika mwisho na wakawa hawawezi. Lakini ugumu wa wanadamu siyo ugumu wa Mungu Baba.
Usikate tama. Yamkini
upo mahali ambapo madaktari wamekuambia ugonjwa ulio nao hauna tiba, lakini Bwana Yesu yupo kwa ajili ya shida
yako, naye atafanya safina katika mito ya Misri. Kumbuka mwisho wa wanadamu
ni mwanzo wa Mungu. Katikati ya maadui,
Musa alikuzwa na kukua. Musa alikula mbele ya Farao, na kukulia ndani ya nyumba ya Farao. Mbinguni Mungu
alikuwa akijua huyu ndiyo mbabbe wa Farao.
Musa akakua katikati ya adui zake. Daudi akasema, “waandaa meza mbele zangu, machoni pa watesi wangu”. Ambaco Wamisiri hawakukijua ni kuwa, Musa
ni kutoka juu na yupo kwa kazi maalumu. Kuku ni kuku,hawezi kuwa tai hata siku
moja.
Comments