![]() |
Na Mtumishi Peter Lukuta |
Maombi yameekuwa yanatafsriwa na watu mbalimbali viongozi wa dini mbali mbali na mathehebu mbali mbali kutokana na utashi wao binafsi na tafsiri hizo zimetokana na mitazamo ya watu waliyoshindwa kuyajua maombi hivyo wakaamua tu kurahisisha ili kuweka mambo sawa kulingana na udhaifu wa maththebu yao. ili tujue ukweli kuhusu maombi ni lazima tujifunze kwa Yesu mwenyewe, watu wengi wameyafanya maombi kama kitu cha ziada, au kitu kisicho na umuhimu wowote ule ambacho kinafanywa tu wakati ambao muda unapatkana, lakini leo nataka nikufundishe ukweli khusu maombi, Je unataka kuwa Shujaa wa maombi? Nifwate hadi Mwisho
UKWELI KUHUSU MAOMBI
Maombi nimtangulizi kabla ya mambo yote maombi ni TINGA TINGA linalotengeneza njia kabla ya vyombo vingine vya moto kupita, maombi ni BARUTI inayopasua mawe na miamba mikubwa ili kuleta urahisi wa kupata madini, Maombi ni TSUNAMI ambayo ikipita haibakishi kitu inazoa na kuteketeza kila kilichoko mbele yake na kuacha mahali ukiwa,, maombi ni MOTO unaolamba na kuteketeza msitu mkubwa na kubakisha majivu tu. Yesu anasema OMBENI NANYI MTAPEWA TAFUTENI NANYI MTAPATA>MATHAYO 7:7. kuna mambo ya kujifunza kwenye maneno haya ya Yesu kwanza amesema OMBENI linamaanisha kwamba Kuna kitu Yesu alikiona kwa watu kuna mataabiko aliyoyaona kwa macho yake kuwa watu wanataabika, lakini kutaabika huko kunatokana na uhaba wa kitu kinachoitwa maombi ambacho ndicho suluhu ya matatizo yahusianayo na maisha yao, wakati wao wanataabika sana Yesu aliona jawabu kwakuwa anmacho ya kuona na ufahamu wa kuelewa, lakini wao hawakuwa na ufahamu wa kuelewa wala macho ya kuona ndiyosababu hawakujua suluhu ya matatizo yao Hivyo basi Yesu aliowaambia OMBENI hii inamaanisha kwa mara ya kwanza ANAWAPA UFAHAMU NA KUWAFUNGUA MACHO WAJUE SULUHU YA MATATIZO YAO. tafsari rahisi ni hii, Msiumize vichwa kwamba mtapatapataje mnayoyataka jibu ni hili hayo yanapatikna kwa njia ya Maombi, hii ndiyo maana halisi yaliyoimaanisha Yesu aliposema OMBENI sasa wewe ambaye unamaswali meengi kuhusu maisha yako na mikwamo mingi ujue kuwa jibu la hayo ni maombi siyo sala na dua hapana ni maombi.
Yesu hakuishia tu kusema ombeni bali aliendelea na neno hili la ili akasema NANYI mtapewa sasa hili neno NANYI lina maanisha kuwa si kila mtu hapana bali ni kundi maalum tu, Yesu hakusema ombeni mtapewa hapana angesema hivyo ingekuwa na maana ni kwa wote yani kila anayeomba anapewa lakini kuna neno amelisema hapa katikati akasema NANYI yaani NYINYI TU NA SIYO WENGINE, wengine wataomba, watafunga watakesha watalia lakini kamwe hawatapata, isipokuwa ninyi mkiomba mtapata, Sasa hapa Yesu hakuwa anaongea na kila mtu bali alikuwa analenga watu fulani ambao walikuwa wanafuata njia zake, utaona kipindi Yesu anaanza kuhubiri hakusema maneno haya bali haya aliyasema baadae kipindi ambacho amepata wanafunzi ambao wanamfuta kila anapoenda kila njia anayopita waponaye hawamwachi, watu ambao akitukanwa waonae wanamuona Yeye kuwa ni bora kuliko vyote hawa ndiyo aliwaambia NANYI mtapewa hii inafundisha kwamba kabla hujaomba nilazima kutengeneza njia zako kujikagua ili kujua njia zako na kuhakikisha kwamba unaingia kwenye kundi la NINYI, ambalo ndilo limethibitishiwa kujibiwa maombi yake, siku hizi watu wengi hawajibiwi maombi yao wala hawapokei haja za mioyo yao indi wanapoomba wenyewe bali wengi hupokea pindi tu wanapo ombewa na sisi watumishi unakuta mtu ameokoka lakini hajibiwi kabisa maombi mpaka aombewe na mtu sababu zipo nyingi na siyo dhambi wala siyo tatizo kuombewa na mtumishi na haki ya mtu kabisa kuombewa na mtumishi wake alaiyemchagua awe kiongozi wake wa kiroho lakini hii ya kutojibiwa unapoomba mwenyewe inasababishwa na vitu vingi lakini kimoja wapo ni hii ya kutokuwa kwenye kundi la NINYI bali huyo aliyekuombea na ukafunguliwa yeye ndiyo yupo kwenye kundi la hao wenye sifa za kujibiwa. haiwezekani usijibiwe maombi kama umekidhi vigezo vyote vya kujibiwa ni lazima uokee majibu yako unapoomba kama uo sahihi maana Mungu si Muongo.
Yesu akaendelea kusema kwamba MTAPEWA sasa hili Neno MTAPEWA ni la kiroho zaidi maana kuppewa siyo kupata hapana ok labda tufanye mfano huu Mimi niko Dar nikakupigia cm kwamba nimeamua kukupa gari sasa pamoja na mimi kukupa gari ni kweli gari limeshakuwa la kwako lakini bado hujalimiliki maana uko mbali nami sasa itakulazimu ufunge safari ili uje dari kulichukua umeona hapo kupewa ulishaewa lakini ulkuwa bado haujapata bali umepata baada ya kuja Dar maana yeke ni kwamba hukupata kwasabu ya kupewa no bali umepata kwasabu ya kuja na huko ndiko kutafuta, sasa tunaendelea Anasema MTAPEWA hii inamaana kuwa yupo mwenye kitu ambacho mwombaji anakihitaji lakini mtu hyu hatui kitu hicho mppaka aombwe kwanza na akiisha kuombwa huwa hakitoi moja kwaa moja mkononi kwa mwombaji no bali anakitoa kwanza kwenye ulimwengu wa roho kisha akiisha kukitoa kwenye ulimwengu wa roho itambidi sasa huyu muombaji akitafute na akiisha kikitafuta ndio atakipata, sasa hii inaonyesha kwamba hayahitajiki maombi tu no bali kunahitajika na macho ya kuona.
Hayahitajiki maombi tu bali kunahitajika na macho ya kuona sasa macho haya ni macho ya ndani ya moyo ambayo pia hupatkana kwa njia ya maombi>EFESO 1:18. Sasa kuomba kupewa macho ni muhimu sana kwasabu macho hayo ndiyo yanampa mtu kukiona kile alichokiomba kwamba kiko wapi aende wapi afanye nini ili aweze kukipata, kuomba na kutafuta ni kitu pacha ambavyo vinapatana, haviachani hata kidogo na kujaribu kuviachanisha ni kukosa maarifa na kutafuta kuangamizwa,
Yesu anasema KILA AOMBAYE HUPOKEA hii inamaana ya kwamba mtu akiishakuomba tu tayari amepokea lakini sasa hapa ndippo wengi hawajapaelewa hawajui kwamba kupokea kunakosemwa hapa si kupokea kule kwa mwilini no bali ni kupokea kwa rohoni maana yake ni kwamba Kila ukiomba Mungu kule mbinguni anaachilia kitu kije sasa kama utakaa tu kukisubiria kikufikie kamwe hutakiona na matokeio yake mtu anauna maandiko yanadanganya lakini kumbe ni yeye mwenyewe amekosa maarifa maana Yesu hakuishia tu kusema kila aombaye hupokea no bali alisema NAYE ATAFUTAYE ATAPATA>MATHAYO 7:8. angalia mwana wa Mungu iko hivi kupokea ulishapokea zamaani sana tangu ulipoomba lakini bado hujappata sababu hujatafuta, Mfano huwezi kuomba upandishwe cheo wakati hutakikuongeza elimu kwa kisomo huko ni kukosa maarifa unapoomba upandishwe cheo ujue kwenye ulimwengu wa roho tayari umeshapandishwa lakini unapaswa sasa kuchukua hatua ya kuongeeza kisomo ili uwe na haki ya kuandishwa cheo nakumbuka nilifundisha hapa fb maombi na haki ya kupokea nikasema Mungu hakupi kitu ambacho hana haki nacho, hivyo tafuta haki ndipo utapewa.
MOMBI TANGULIZI KABLA YA TUKIO
Yesu hakufanya jambo lolote kabla ya kuomba bali aliomba kwqnza ndipo akafanya kabla ya kuwachagua mitume aliomba kwanza kwa muda wa masaa 12 na baada ya hapo alichagua mitume 12 hii inaonyesha ya kwamba ilimgharimu Yesu maombi ya lisaa limoja kwaajili ya kumpata mtume momoja Yesu alikubali kugharimika kwenye maombi kuliko kugharimika kwenye kuchagua mitume unajua kazi ya kuchagua mitume ilikuwa ni ngumu sana lakini ilirahisishwa na maombi ya Yesu kwakuwa aliomba sana ndipo akachagua mitume unaona kuwa alipowachagua hakuwalazimisha wala hakuitisha barua za maombi ya kazi kama wafanyavyo makuhani wetu wa leo wanatumia akili nyingi za kibinadamu wakdhania kuwa wanchagua kiongozi wa kibinadamu, wanaacha kuingia rohoni kwa maombi mazito kwsabu wanakwepa gharama matokeo yake wanatuchagulia viongozi wakanisa WAZINIFU WAKUBWA MATAPELI, WACHONGANISHI, WAMBEA, WANAFIKI WAKUBWA, hii yote Yesu aliiona ndiyo maana alitumia muda mwingi kuomba kabla ya kuwachagua na usifikiri kwamba ilikuwa ni kazi rahisi kwa wateuliwa kukubali wito huo mgumu sana ni wazi kwamba kibinadamu haikuwa rahisi wao kukubali uteuzi huo, kwasabu Shetani alikuwa kazini kuhakikisha kuwa akina Petro hawatakubali uteuzi huo au watakubali lakini si kwa moyo ila kwa shinikizo lakini Yesu alitanguliza maombi kwanza na kuiharibu mipango yoote ya Shetani.
Yesu alipoingia yale maombi ya kuomba kwaajili ya kuwapata Mitume hakupanga kuomba kwa masaa yote 12 na ndiyo maana hata alipopanda kwenda mlimani kuomba hakwenda maandiko hayasemi kwamba alienda kukesha no bali yanasema kwamba alienda kuomba na akakesha huko usiku kucha>LUKA 6:12-16. Hii inaonyesha kwamba Yesu hakuwa na ratiba ya kwenda kukesha mlimani kwasabu hakuaga kwamba naenda kukesha kama kawaida yake maana Ilikuwa ni kawaida yake kuaga kama anaenda kukesha sasa hapa Yesu alikuwa anaenda kuomba tu lakini alipokuwa kwenye hayo maombi alikutana na vita kali sana na upinzani mzito wa Shetani kutokana na kile alichopanga kukifanya yani uteuzi wa mitume na hali hiyo ikamfanya afanye maombi marefu ambayo hakujua yataisha saangapi lakini mpaka vita ile ilipoisha na Yesu kuishinda ilimchukua masaa 12 hivyo Yesu alishashinda vita rohoni kwa kuyatanguliza Maombi na baada ya maombi hayo ndipo lakafwata tukio la kuwateua Mitume hapa ndipo tunasema MAOMBI TANGULIZI KABLA YA TUKIO.
Maombi yanatengeneza njia ambayo itapitisha kitu flani sasa siku zote gari linapojaribu kupita mahali pasipo na barabara ambapo bado Tingatinga halijapita kutengeneza ooh niwazi kwamba hilo gari litakwama, na hii ndvyo ilivyo mtu anapotanguliza kufanya kitu chochote kabla ya kuomba ujue ni lazima atakwama maana Tinga Tinga la maombi ambalo ndilo hutengeneza barabara halijapita bado.
TAFAKARI TUKIO LA KUZALIWA KWA YESU MWANA WA MUNGU
Yesu ni mwana wa Mungu aliyetokea mbinguni na upako wa kuweza kuokoa ulimwengu sasa jiulize kama hata Yesu tu mwana wa Mungu mwenyewe mwenye nguvu zote, haikuwezekana kuzaliwa mpaka pale Ana binti Fanueli alipoomba ndipo Yesu akazaliwa>LUKA 2:36-38, Sasa je wewe utafanikiwaje pasipo kuomba? kunalolote utakaloliweza pasipo kuomba?
Kama lipo basi wewe utakuwa na nguvu kuliko Mungu maana hata Mungu mwenyewe alimweka Na ili akeshe na kuomba miaka kwa miaka kwaajili ya ujio wa Yesu maana hii ni kanuni sasa kama Mungu mwenyewe anatanguliza maombi mimi sijui wewe unayeyapuuza maombi unamwabudu Mungu yupi.
Yapo mengi ya kufahamu juu ya maombi lakini kwa leo naishia hapa Kwa Ushauri Na Maombezi Tuma Masage Kwenye Whtsapp au Telegram kwa Namba 0767 503054 Pia karibu kwenyewe Group letu la FUNGUO ZA UFALME ni Group la Whtsapp ukipenda nikuunganishe nitumie Masage Kwenye Whtsapp au Telegram ya 0767 503054 nitakuunganisha
Kwani niaba ya Mke Wangu sote tunasema TUNAKUPENDA ZIDI KUTUOMBEA
ZIDI KUBARIKIWA
Comments