USITENGENEZE NDAMA, KWA PETE ULIZOTOKA NAZO MISRI.

Na Nickson Mabena

Bwana Yesu asifiwe, Karibu tena wakati huu tujifunze Ujumbe wa Neno la Mungu, Ambao Roho Mtakatifu ameruhusu tushirikishane!.
Natamani Mungu akufundishe Zaidi ya nilivyoandika hapa, kwani ni ujumbe Muhimu kwako, hasa kwenye Maisha yako ya Wokovu!.
"Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee. Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletes Haruni. Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe SANAMU YA NDAMA kwa kuiyeyusha;....". KUTOKA 32:2-4
Wana Wa Israeli walipoona Musa amekawia kushuka kwenye Mlima, Wakamfuata Haruni, ili awatengenezee miungu watakayoiabudu!.
Biblia inatuambia ya kwamba Haruni akawaambia Wavue Pete za Dhahabu zilizo katika masikio yao ili watengenezewe Sanamu ya Ndama, kisha waiabudu!.
Kumbuka, Pete za dhahabu zilizotumika kutengenezea Ndama, Walitoka nazo Misri. Pete hizo hazikua Chukuzo Mbele za Mungu, ndio maana Mungu aliruhusu waende nazo Kwenye Nchi ya Ahadi.
Siku zote Pete hizo zilikuwepo, Siku zote walisafiri nazo toka Utumwani, lakini hata siku moja hazikuwahi Kumchukiza Mungu.
Lakini siku walipoamua Kuzitumia kutengenezea Ndama, ndipo Zikageuka Chukizo Mbele za Mungu.
Ujue, Viko vitu umekua ukivitumia hata kabla hujaja kwa Yesu, Ulipokuja kwa Yesu bado vimekua na Matumizi mazuri tu,
Lakini, Usije hata Siku moja ukavigeuza vitu hivyo, vikawa NDAMA na Vikachukua nafasi ya Mungu kwenye Maisha yako!.
Mfano, Simu uliyonayo ni nzuri tu, tena hata kabla hujaja kwa Yesu ulikua unaitumia hiyo simu, lakini Hiyo simu inaweza ikageuka kuwa ndama, na Ikachukua Nafasi ya Mungu,
Ukatumia Mda Mwingi kwenye Matumizi ya Simu kuliko kwenye Mambo ya Mungu!
Ukatumia Hela nyingi kwa Ajili ya Vocha, wakati huo hata Sadaka Hutoi.
Kwani hujaona Mtu Haendi kwenye ibada kwa Sababu ya Filamu au Mpira!??.
TV yako yaweza kuwa Ndama, Kazi yako yaweza Kuwa ndama, Mke/Mme aweza Kugeuka ndama, Masomo yako Pia yaweza kua Ndama wako!!.
KITU CHOCHOTE KISICHUKUE NAFASI YA MUNGU KWENYE MOYO WAKO, KWANI HASIRA YA MUNGU INAWEZA KUWAKA JUU YAKO!.
Mungu akupe Neema ya Kugeuza Moyo wako kwake!.
By Mwalm Nick
0712265856 Watsap#

Comments