UTUMISHI WENYE SURA YA MUNGU JUU YAKO NDIYO UNAWAVUTA WATU KWA YESU

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu siku zote anayetupa uzima na afya.Maana ni Neema yake tu ndiyo inayo tupa kuwa hai, na uhai huo una makusudi yake hapa duniani, ndiyo maana Muhubiri anasema,,,"Kwa kila jambo kuna kuna majira yake,Na wakati wa kila kusudi chini ya jua" (Muhubiri 3:1)
Hivyo tunapswa kutambua kwamba uzima tulionao una kusudi lake, inawezeka una kusudi la kukuvuta ili utubu kabla hujafa au una kusudi la kukufanya uendelee katika kusudi la kumtumikiao Mungu katika utumishi wake na utumishi wa kijamii.

Karibu tukajifunze somo hili na zaidi sana Roho Mtakatifu akufunulie siri iloyoko katika somo hili ili ujue wewe ni mtu wa namna gani na katika utumishi wako.
Unaweza kusema mimi si mtumishi maana si Mchungaji wala Mwinjilusti nk, sikia nikwambi, swala kiutumishi ni la kila mtu aliyeokoka, maana tuna agizo tumepewa ,,"BASI, ENENDENI, MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI" (Mathayo 28:19)
Pia siku ile ya hukumu ya watakatifu kazi ya kila mmoja itapimwa na kila mtu kupokea "TAJI" sawa na utumishi wake aliyoufanya hapana duniani, hapo hakuna cha Mtume wala Mchungaji taji hutolewa kulinga na utumishi wako uliofanya,,,,Bwana Yesu asifiwe!.

Somo letu linatoka 1 Timotheo 4:12 maandiko matakatifu yanasema hivi; "Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi".
Hii ni baru ambayo Mtume Paulo anamwandikia Timotheo ya kwamba awe na mfumo wa maisha ya "UCHAJI" wa ki Mungu, ambayo yamebeba "SURA YA MUNGU" siku zote na kuurudisha utukufu wa Mungu. Kwa njinsi hiyo basi, mtu awaye yote hawezi kuudharau ujana wake maana hawaioni sababu ya kudharau ujana wake katika utumishi wake.
Kuna mambo matana ambayo Paulo anamwambia Timotheo anapaswa kuwa nayo ili kupitia hayo awe "KIELELEZO" kwa wale wenzake waliookoka pia na wasio mjua Mungu na wao wamjue Mungu kupitia maisha yake.
Swali la kujiuliza mimi na wewe kabla hatujayaangalia mambo hayo matano, je, mimi na wewe utumishi wetu una sifa za kungumziwa vizuri katika ya jamii tunayo ishi? Au ujana wako umedharauliwa kwa Wakristo wenzako au kwa wasio wakristo pia? Na kama ujana wetu unadharauliwa tujue tunawafungia watu kuokoka, Yesu anasemaje?,,,anasema hivi,,,"OLE WENU WAANDISHI NA MAFARISAYO, WANAFIKI! KWA KUWA MWAWAFUNGIA WATU UFALME WA MBINGUNI; NINYI WENYEWE HAMWINGII, WALA WANAOINGIA HAMWACHI WAINGIE" (Mathayo 23:13) Kielelezo cha maisha yako katika utumishi kinaweza kuwazuhia wengine wasiokoke kabisa kwa sababu maisha yako yamedharauriwa, wanabaki kusema "Kama kuokoka ndiyo hivyo bora niache kuokoka" mtu huyo amezuhiliwa na maisha yako.

KIELELEZO ANACHOPASWA KUWA NACHO MTUMISHI WA MUNGU ILI WATU WAMFUATE.
Yesu alisema maneno haya,,"Na waachieni kielelezo" mana yake mnifuate mimi. Kama Paulo alivyomfuata Kristo naye akasema hivi; "MNIFUATE MIMI KAMA MIMI NINAVYOMFUATA KRISTO" ( 1 Wakoritho 11:1)
Ukisoma 2 Thesalonike 3:9 Paulo analiambia kanisa anasema,,,"Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate".

KIELELEZO CHA I.
USEMI
Usemi au mazungumzo yako ndiyo yatakuonyesha wewe umeokoka au hujaokoka.Maana kama huna mazungumzo mazuri watu watujua wewe "HUJAOKOKA" si mimi nimesema mandiko yanasema,,,"MTU HUYANENA YALE YAUJAZAYO MOYO WAKE" kama wewe uasema ni kijana umeokoka moyo wako ujazwa nini? ebu angalia "USIMI WAKO" je unawapa watu kuudharau ujana wako? maana maana moyo wako ukijaa masengenyo na matusi uwe na uhakika ndiyo utayangumza.
Petro walimtambua kuwa ni Mwanafunzi wa Yesu kwa sababu ya usemi wake. Mathayo 26:73 maandiko yanasema,,,"Punde kidogo, wale walioudhuria waamwwndea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe ni mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutamhulisha"....Bwana Yesu asifiwe! unaona maneno hayo? usimi wa Petro unamtambulisha kuwa na yeye ni "MWANAFUNZI WA YESU"

KIELELEZO CHA II.
MWENENDO.
Mwenendo wa aisha ya kijana ni mahubiri tosha ya kuwaleta watu kwa Yesu.Kama utawahubir watu na wakati huo wanatazama mwenendo wako uko tofauti ujue unawqpa watu "AUDHARAU UJANA WAKO" Mithali 20:24 maandiko yanasema,,,"Mwenendo wa mtu wa toka kwa BWANA" Mwenendo unatoka kwa Bwana unauwezo wa kuwavuta wengine waje kwa Bwana.
Mfano mwanamke ili amvute mume wake lazima awe na "MWENENDO MZURI KWA MUMEWE" 1 Petro 3:1 "Kadharika ninyi wake,watiini waume zenu; kusudi ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno" ebu ngalia hili neno,,"PASIPO LILE NENO" maana yake hata kama usipomuhubiria kuokoka lakini kwa "MWENENDO" wako mumeo atakupenda na mwisho wa siku anaokoka.

Kwa mantiki hiyo kijana wa kike na wa kiume chunga sana mwenendo wako maana huo ndiyo mahubiri tosha katika jamii yako.Lakini mwenendo wako kama hausomeki kwa watu "WALIOOKOKA NA WASIO OKOKA" lazima watakuwa na sababu ya kuuddarau ujana wako.
Paulo anasema,,"TUSIWE KWAZO LA NAMNA YOYOTE ILI UTUMISHI WETU USILAUMIWE"
Unaweza kusingiziwa kutenda mabaya, lakini mwenendo wako ukakutetea,,"Mwe na mwenendo mzuri kati ya mataifa, ili, iwapo iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

Fuatana nami katika vipengele vitatu vilivyobaki.
MUNGU AWABARIKI.
ekamalamo@gmail.com
[15:28, 6/11/2015] EV.EMMANUEL: UTUMISHI WENYE SURA YA MUNGU JUU YAKO NDIYO UNAWAVUTA WATU KWA YESU.

(SEHEMU YA PILI)
Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu kwa ajili ya siku ya leo ambayo ametuwezesha tena kupata nafasi ya kuzidi kujifunza Neno lake.Pia namshukuru kwa ajili yako kukuwezesha kupata nafasi ili ujifunze Neno lake.
Leo tunaangalia sehemu ya pili ya somo letu, uliweza kupata sehemu ya kwanza ya somo hili unajua ni wapi tunakwenda, na kama ndiyo ndiyo mara ya kwanza kulipata somo unaweza kulipata sasa kwa njia ya (WhatsApp) ukinitumia ujumbe wenye neno.."NENO LA UZIMA" kwenye namba 0712-660766 nawe utaunganishwa na kupata somo hilo na masomo mengine zaidi.

Tuendelee na somo letu sasa, omba Roho Mtakatifu akufunulie akili upate kuelewa na maandiko.
KIELELEZO ANACHOPASWA KUWA NACHO MTUMISHI WA MUNGU ILI WATU WAMFUATE.
Kama maandikiko yanavyotwambia jinsi Yesu alivyokuwa kielelezo na akatuachia kielelezo nasi tumfuate yeye. Kama Paulo alivyosema,,,"MNIFUATE MIMI KAMA MIMI NINAVYOMFUATA KRISTO" (1 Wakorintho 11:1)
Kwa hiyo kama tumeokoka sisi ni watumishi ambao tunabeba kielelezo ambacho watu waanio na wasio amini wanapaswa watufuate sisi kama sisi tunavyomfuata Kristo.

Ndiyo maana Paulo anamwambia Timotheo achuke sana mfumo wa maisha yake yawe "KIELELEZO" kwa wale anaowaongoza, kwa nini awe kielelezo? Kwa sababu wasiudharau ujana wake ambao umebeba utumishi wa Mingu ndani yake.
KIELELEZO CHA III.
UPENDO- Mtumishi ambaye ameitwa na Mungu lazima upendo kwa watu uwe kielelezo.Kama utakuwa ni mtumishi alafu huna "UPENDO" wewe hujavaa sura ya Mungu, maana maandiko yanasema,,,"..MUNGU NI UPENDO, NAYE AKAAYE KATIKA PENDO, HUKAA NDANI YA MUNGU, NA MUNGU HUKAA NDANI YAKE" (1 Yohana 4:19)
Upendo huu ni upendo wa (AGAPE) usiopenda kwa mipaka au mpaka kutendewa jambo jema, la asha! hata ukitendewa baya upendo huu hauwesabu mabaya, ndiyo sura ya Mungu inapaswa kuoneka kwa mtumishi.
Lazima tuuonyeshe "UKAMILIFU" wetu wa utumishi wetu kwa njia upendo tunapowapenda wengine hata wapotukosea. Wakolosai 3:14 maandiko yanasema,,,"Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndiyo kifungo cha ukamilifu" Saa angalia hili neno,,,"UKAMILIFU" maana yake ni kuenenda sawa na mapenzi ya Mungu, ambayo yamefungwa katika Neno moja lina UPENDO.
Kama huna upendo dhambi itatawala ndani yako na utaitenda lazima, Sema kwa nini? Nisikilize, "UPENDO" una sitiri wingi wa dhambi, iko hivi, kama una upendo mwenzako akiwa hana chukula na na wewe unacho utampa, akiwa uchi utamvika, lakini usipofanya hivyo maana yake "DHAMBI" imekuwa wazi kwako, yaani umetenda kwa sababu upendo hauko ndani yak kukusaidia kusitiri dhambi ambazo ungezishinda pale ambapo ungewasaidia "YATIMA,WAJANE, MASIKINI NK"
Hapa ni lazima utumishi wako utadharauliwa na watu wote.

KIELELEZO IV
IMANI-Hii siyo imani ambayo kila mtu anaitumia kwa njia ya maombi ya kutarajia mambo yajayo (Waebrania 11:1) Bali imani hii ni Kisto ambayo inawaokoa watu wote.
Yuda 1:3 anasema,,,"Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliokabidhiwa watakatifu mara moja tu." Hiki ni kielelezo cha Kijana ambaye ni mtumishi anaswa kuwa nacho siku zote kusimamia "IMANI SAHIHI" isipotee na watu kuamini imani zingine zisizoleta ukombozi kwa mwanadamu.
Lazima uitetee hii imani kama Antipa "SHAHIDI" mwaminifu wa Yesu alivyokufa kwa kuitetea "IMANI" ya kweli ambayo shetani aliipinga lakini Antipa aliisamimia kikamilifu.

Kijana unaweza ukaletewa imani zisizo sahihi ili uikane imani yako ili sahihi na kama hujasimama kikamilufu uwe na uhakika "PESA" ikija mbele yako unapoteza imani iokoayo uliyopewa mara moja.
Sikia nikwambie ningekuwa sijui "UTHAMANI" wa imani hii niliyo nayo pesa ingenikamata mapema, maana natangaziwa dau la pesa niiche "IMANI" hii nayo ihubiri nifuate imani isiyo sahihi kisa pesa....oooh! sikia nikwambie kijana nimepangua nia zao nikasema,,,"Siwezi poteza uzima wa milele kwa pesa" maana dunia inapita pamoja na mambo yake yote, bali yeye afantaye mapenzi ta Mungu adumu milele.....Bwana Yesu asifiweeee!

KIELELEZO V
USAFI-Huu ni usafi wa Roho, Mwili.
Mithali 22:11 anasema,,"Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake" Moyo usipokuwa msafi huwezi kuwa kielelezo kwa watu na Mungu hawezi kuwa rafiki yako.
Pia usafi wa Mwili ni muhimu kwa kijana ili awe kielelezo kwa wengine.Kijana kama hutaweza kuuweka mwili wako katika usafi watu wataudharau ujana wako. Upaswi kuvaa nguo chafu zinatoa harufu alafu unawaongoza watu unawapa makwazo kwa harufu yako, soksi ina mwezi haijafuliwa na unaingia ndani mwa mtu kupeleka injili soksi zinatoa uvundo unamfanya mtu akuzarahu.
Nywele unyoi kichwani zimejisokota, dada naye anaimba sifa amevaa brauzi kwapa zote nje msitu si msitu sasa sikilizia harufu ya hapo alafu unasema wewe kielelezo.

Kama hutaweka usafi wa mwili kaka au dada hutaweza kuchumbiwa wala kuolewa maana wakikusogelea tu mmmmh! mtu anatama ibada ishe aondoke kwenye kiti, au ukiongea tu harufu inayotoka si ya kaida, sasa hapo ni vigumu kijana kuwa kielelezo kwa wengine na wala hawawezi kukufuata maana wakikaa na wewe unabadirisha hali ya hewa.
Hakikiksha unakuwa kielelezo katika usafi wa mwilu na roho.

KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA BAADA YA KUFA HUKUMU.(Waebrania 9:27)
MUNGU AWABARIKI.
ekanalamo@gmail.como

Comments