VITABU VYA KUKUSAIDIA KUJUA MAMBO MENGI YA MUNGU NA KUTEMBEA KATIKA KUSUDI LAKE.


Vitabu hivi vinapatikana kila sehemu Tanzania, nunua kwa ajili ya kujifunza.
Ubarikiwe sana.




TUNYOSHE MIKONO
Bwana Yesu alisema, "mkinipenda, mtazishika amri zangu (Yohana 14:15.) kisha akatuagiza, "mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote... mpende jirani yako kama nafsi yako... basi enendeni mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi wangu... na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi..." (mathayo 23:37-39, 19:-20.)
Ni wazi kwamba Yesu anataka watu wote wakiwemo Waislamu wawe wanafunzi wake. Waislamu hawatakuja makanisani mwetu, sharti tuende kwao. Mara nyingi Wakristo husita-husita kuwaendea Waislamu kwa sababu hawawafahamu Waislamu na imani yao.
Kitabu hiki kitakusaidia ufahamu tofauti iliyoko kati ya Ukristo na Uislamu, madai ya kimsingi ya Waislamu dhidi ya imani ya Kikristo na jinsi ya kuyajibu kwa upole na upendo madai hayo. Kitabu hiki kitakuandaa ili uwe tayari kueneza Injili kwa Waislamu. Huu ni msaada mkubwa kwa kila Mkristo anayewapenda na kuwajali Waislamu.

MUINJILISTI
Hii ni kosi kwa njia ya posta kwa ajili ya kuwaandaa Wakristo wanaonuia kueneza Injili kwa Waislamu. Kosi hii yenye masomo ishirini inaguzia maswala mengi yanayohusiana na uenezaji wa Injili kwa Waislamu. Katika kila somo kuna makala kuhusu Uislamu, Utetezi, mawasiliano na mengine mengi.
Tuna pia makala ya uchambuzi wa vitabu ili kuwafahamisha wanafunzi wetu vitabu vipya. Barua kutoka kwa wanafunzi wengine wakielezea yale Bwana anafanya katika huduma ya kuwafikia Waislamu zimechapishwa ili kuwahimizana.

KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA UISLAMU
John Gilchrist ambaye ni wakili anayeishi Afrika Kusini, ana uzoefu wa miaka mingi katika huduma ya uinjilisti kwa Waislamu. Amefanya mihadhara na wasomi mashuhuri wa kiislamu kama vile Ahmed Deedat, Adam Peerbhai, Basheer Vania na Yusufu Buckas. Katika mihadhara hii, karibu hoja zote zilizomo katika kitabu hiki zilijadiliwa. Isitoshe, Bwana Gilchrist pia amewatembelea Waslamu wengi manyumbani mwao na kuwaelezea habari za Injili. Hivyo amezisikia hoja hizi moja kwa moja kutoka kwa Waislamu na kutoa majibu mwafaka ya Kikristo dhidi ya hoja hizo.
Kukabiliana na hoja za Kiislamu ni kitabu kinachofaa sana na kinachoshughulika na hoja za kawaida ambazo Waislamu hutoa ili kupinga wainjilisti wa Kikristo. Katika historia ya Uislamu, hoja zinazotolewa kupinga ukristo zimekuwa sawa. Wakristo wanaowashirikisha Waislamu injili watahitaji kujua ni hoja zipi zinazoleta utata na pia jinsi ya kuzijibu kikamilifu. Kitabu hiki kinatoa majibu kamili yanayothibitishwa na ushahidi madhubuti. Muhimu ni kwamba kitabu hiki msomaji ataona pia jinsi hoja hizo za kiislamu zinaweza kutumiwa kama jukwa la kuwaelezea Waislamu ukweli na kuwashirikisha injili.

MAISHA YA MILELE HUTEGEMEA NINI?
Kila mtu anahitaji rafiki ambaye anaweza kuhusiana naye kikamilifu. Waislamu si tofauti. Wao pia wangependa kuwa na uhusiano na watu waaminifu, wenye upendo na huruma. Je, umewahi kumwomba Mungu akuongoze kwa mtu ambaye anataka wewe uwe rafiki wa kumpa manufaa ya milele? " Maisha ya milele hutegemea nini " kinakusudia kukupa mbinu tofauti za kuwafikia Waislamu unaokutana nao kila siku ili waje kwa Kristo.

KANISA LA AFRIKA LINAANGALIA MAKUSUDI YA UISLAMU
Kitabu hiki kimenuiwa kutumiwa kama mwongozo kuhusu uinjilisti kwa Waislamu. Kinaweza kutumiwa na viongozi wa Kikristo makanisani, vikundi vya kujifunza biblia manyumbani, katika ushirika wa wanafunzi shuleni na hata katika mashirika ya Kikristo. Kitabu hiki kina sehemu tano. Baada ya kila sehemu, kuna maswali kwa ajili ya majadiliano. Majadiliano haya yatasaidia sana kuwawezesha Wakristo wafahamu Uislamu na Waislamu. Pia, kinatoa mbinu mwafaka za jinsi ya kuwashirikisha Injili wao 'walio nje' kwa hekima na ujasiri. Inafaa pia ikumbukwe kwamba mara nyingi hao walio nje huenda wasiwe na ujasiri wa kuja makanisani ili waweze kusikia ujumbe wa Injili. Hivyo itabidi sisi tuende kwao. (Kol. 5:5)

KUWASHIRIKISHA WAISLAMU UPENDO WA MUNGU
Je, ni vigumu kuwafikia Waislamu na Injili? Tutajuaje ikiwa hatutajajaribu!
Waislamu wengi wana tashwishi na maswali mengi dhidi ya dini yao na wanatafuta majibu. Kwa kawaida Waislamu hawaruhusiwi kuuliza maswali dhidi ya dini yao. Watafahamuje upendo wa Mungu ikiwa sisi Wakristo hatuwakaribii na kuwaeleza Injili? Kristo alikufa kwa ajili ya watu wote, wakiwemo Waislamu, hivyo ni jukumu la kila Mkristo kuwaelezea Waislamu, "habari za tumaini tulilo nalo". (1 Petro 3:15)
Utaratibu uliotumiwa katika kitabu hiki unamfaa Mkristo yeyote anayetaka kuwafikia Waislamu na Injili. Ombi letu ni kwamba wote watakaokisoma kitabu hiki watafumbuliwa macho yao ili waanze kuwaelezea Waislamu habari njema. Waislamu wamepuuzwa kwa muda mrefu na Wainjilisti wa Kikristo. Hali hii sharti ibadilike.

NANI ANAYEJALI
Wito huu umenuiwa kuwafumbwa macho wachungaji na Wakristo kwa jumla ili waone changamoto ya Uislamu na jinsi tunavyoweza kuwafikia Waislamu na ujumbe wa Injili. Kitabu hiki kinaonyesha wazi kwamba kuwashirikisha Waislamu Injili ni changamoto maalum inayoitaji mhudumu Mkristo ajiandae vema. Usaidizi upo kwa ajili ya maandalizi kwa kazi hii. Sote tuna jukumu la kuitikia wito huu kwanza kibinafsi na pili kwa pamoja kama kanisa la Bwana Yesu.

Comments