WACHAWI WAUTUMA MKIA WA FARASI MKUTANONI KUMDONDOSHA MHUBIRI!


Mkia wa Farasi uliotumwa katika Mkutano wa injili, ambao ulikuja wenyewe katika mkutano huo wa injili, Mkia huo ulitokea angani.

Na Pst Peter Mitimingi.
Ni ajabu na kweli. Wachawi wa hapa Lindi baada ya kujaribu kutuloga kwa njia mbalimbali na kushindikana walituma mkia wa farasi ukiwa umefungwa kitambaa chekundu. Mkia huyo haukurushwa bali ukikuwa ukielea kutoka angani mpaka ukafika kwenye eneo la mkutano na kujichomeka wenyewe aridhini na kusimama. Tukio hilo liliwashangaza sana watu wote waliokuwa wamaketi chini kusikiliza neno la Mungu.

  Baada ya kudondoka kwa mkia huo watu wengi waliokuwa wamekuja kusikia injili walikimbia na kusimama mbali mpaka makomandoo wa VHM waliposogelea na kuushika mkia.
YESU AMEFANYA MAMBO MAKUBWA SANA VIJIJI VYA LINDI!

Hakika ilishangaza sana laki nguvu ya MUNGU ilikuwa kubwa na wachawi hao hawakufanikiwa.

Huduma hii ya injili vijijini inaendelea vizuri sana maana watu wanageuka na kumpokea BWANA YESU kama Mwokozi wao.
Katika moja ya mikutano ya injili vijijini huko Lindi inayoendeshwa na VHM.
YESU KRISTO anaokoa Lindi, ukiamini unaokoka.
Uchawi haukufua dafu katika mkutano huo maana Jina la YESU KRISTO ni ushindi wa milele.

Comments