ZIJUE SIRI ZA UFALME WA GIZA!.

Na Nickoso Mabena

Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu Popote pale Ulipo, ninayo furaha leo hii kukuletea Ujumbe wa Neno la Mungu,
Ujumbe huu ni Muhimu sana kwa Kila Mwanadamu aweze kuupata.
Ninamshukuru Mungu pia kwa ajili ya watu wake aliowatumia kuniuliza Maswali, na wengine kunishauri niandae Somo kama hili, na hiyo yote ilikuja Baada ya Siku Moja kuandika Ujumbe Uliohusu UPASUAJI NA MATATIZO YA MATUMBO KWA WANAWAKE, na Niliandika kwenye ujumbe ule ya Kwamba hizo ni roho kutoka Kuzimu!.
Watu wengi walinitaka nielezee maana ya roho kutoka kuzimu..
Somo hili nimeliita Zijue Siri za Ufalme wa Giza, na leo hii nataka nianze na Utangulizi tu wa Somo hili, ili upate Picha japo kwa kidogo, vitu nitakavyofundisha!.
NAMUOMBA MUNGU KWA AJILI YAKO ILI UPATE UFAHAMU WA KIROHO!
👉Tunapaswa kujua ya Kwamba kuna Falme kuu Mbili katika Ulimwengu wa roho,
1.Ufalme wa Nuru
2.Ufalme wa Giza

Falme hizi zinatenda Kazi na kuratibu Mambo mengi sana tunayoyaona na kuyasikia katika ulimwengu huu...
Kwenye Somo hili, nitauzungumzia sana Ufalme wa Giza, Japokua ntakua nagusia pia Ufalme wa Nuru!.
👉Kwenye Somo hili nitafundisha Mambo yafuatayo:-
1.Uhalisia wa Ulimwengu wa roho (Huu ni Msingi wa Somo)
2.Waratibu wa Ulimwengu wa roho katika Ufalme wa Nuru na Ufalme wa Giza.
3.Watumishi Katika Ufalme wa Nuru na Ufalme wa Giza.
4.Jinsi Ufalme wa Giza unavyotenda kazi (Hiki ni kiini cha somo) 👉Nitaelezea roho kutoka kuzimu na jinsi zinavyofanya kazi!. 👉Ntatumia Shuhuda ninazoziamini!.
5.Vitu Vinavyotumika katika Ufalme wa Giza.
6.Sadaka Zitolewazo katika Ufalme wa Giza.
7.Sababu za Watu kwenda kutaka Msaada Kwenye Ufalme wa Giza.
8.Jinsi ya Kuingia kwenye Ulimwengu wa roho na Kupambana na Ufalme wa Giza na Kuushinda!.


1.UHALISIA WA ULIMWENGU WA ROHO!.
"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho". Efeso 6:12
Kwenye jambo hili, Lengo hasa ni upate kujua ya kwamba kuna ulimwengu, unaitwa ulimwengu wa roho.
Huu ni Ulimwengu Usioonekana kwa macho haya, Kwenye andiko hilo Paulo anatufundisha kwamba kuna kushindana, lakini Mashindano hayo hatuyafanyi kwenye ulimwengu huu, bali kwenye ulimwengu wa roho!.
Lazima ujue, Kila Jambo linalotokea kwenye Ulimwengu huu wa Mwili, limeanzia kwenye Ulimwengu wa roho!.
Paulo anataka Mawazo ya Watu wa Efeso, yahame kwenye Kutaka kuleta Mashindano Kimwili... lakini, fikra zao zihamie kwenye kuuwaza, na kutaka kuujua Ulimwengu Mwingine, ambao Unaitwa Ulimwengu wa roho!.
Mungu anataka tujue kwamba, kama tunataka matokeo kwenye ulimwengu huu, basi tukatafute kushinda kwenye ulimwengu wa roho, hata kama Vita ipo kwa jinsi ya Mwili.
Kwenda rohoni lazima, kuujua ulimwengu wa roho lazima pia!.
Kujua Uhalisia wa Ulimwengu wa roho nimeuita Msingi wa somo, kwani Mambo Mengi tutakayoyajadili yatakua kwa Jinsi ya rohoni.
Maana huwezi kuelewa Chochote, kama hujatambua Uwepo wa Ulimwengu wa roho!.
Pia, huwezi Ukapata Ushindi Juu ya Vita yako kama Hujaujua Ulimwengu wa roho,
Chukulia Mfano, Kuwe na Mechi ya Mpira wa Miguu, kati ya vipofu na watu Wanaoona, hivi timu gani itafungwa!?. Mimi nadhani timu ya vipofu itafungwa tu, na kwa sababu hawaoni, hawalijui goli lilipo, wala hawajui Mpira umeenda upande gani, Watacheza kwa hisia tu!.
Ndivyo ilivyo kwa mtu anayetaka kupambana na Ufalme wa giza, Wakati Haujui ulimwengu wa roho, lazima atapigwa tu.. Maana hajui chochote kinachoendelea, hajui mipaka ya adui yake, hatajua Mpinzani wake anakuja kwa Mbinu gani!.
2.WARATIBU WA ULIMWENGU WA ROHO.
Kwenye utangulizi, nilikwambia, Kuna falme kuu Mbili, Ufalme wa Nuru na Ufalme wa Giza, hizi falme zote zipo kwenye Ulimwengu wa roho, wanaotawala hizi falme ndio nawaita waratibu wa ulimwengu wa roho.
Hapa, nawazungumzia Mungu na Shetani,
Biblia imesema, Mungu ni Roho (Yoh 4:24), lakini Shetani Pia ni roho (Efeso 2:2).

Sasa naweza nikasema, Mfalme wa Nuru ni Mungu mwenyewe, na Mfalme wa Giza ni Shetani!.
Kwenye Sehemu zinazofuata za Somo hili, nitakua nakukumbusha tulipotoka, ndio Maana Mambo haya Mawili, nimeyatanguliza!.
KUMBUKA: LAZIMA UJUE KWAMBA, KUNA ULIMWENGU MWINGINE, UNAITWA ULIMWENGU WA ROHO, NA WARATIBU KWENYE ULIMWENGU ULIMWENGU HUO NI MUNGU NA SHETANI!.
...Somo litaendelea, Usiache kufuatilia....
Ubarikiwe na Mungu..
By Mwalm Nick
0712265856 Watsap#

Comments