![]() |
Apostle John Komanya enzi za uhai wake. |
Siku ya Jumapili hii imekua ya majonzi
kwa ndugu jamaa ,marafiki familia na waumini wa Mtume na nabii John
Komanywa ambaye alifariki asubuhi ya siku hiyo akiwa katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili ambapo alikua akitibiwa matatizo ya kiafya yaliyokua
yakimsumbua.
Chanzo kilichopelekea umauti wake kwa
mujibu wa dada wa marehemu ameelezea kwamba Apostle Komanywa alipatwa na
tatizo la mishipa inayopeleka Oksijeni kwenye Ubongo kushindwa kufanya
kazi ghafla na hivyo mwili mzima ukajikuta umeishiwa nguvu na kuanguka
ambapo baadae alikimbizwa Hospitali na baada ya vipimo madaktari
walieleza kua mishipa hiyo ilifeli ghafla lakini pia kulikua na tatizo
la Kisukari ambalo lilikua limeshakua kubwa.
Wimbo bora kabisa ulioimbwa na Apostle Komanya ni huu.
Wimbo bora kabisa ulioimbwa na Apostle Komanya ni huu.
Mwili wa apostle Komanya utazikwa kesho jumatano .
Tazama Video inayomuonesha Dada wa marehemu akielezea kwa urefu zaidi kuhusu chanzo cha umauti huo na mipango ya mazishi
Comments