SHUHUDA KUTOKA UFUFUO NA UZIMA KIGOMA.

"ALIISHI NA GLOVES TUMBONI KWA MUDA WA MIEZI 3"

Anaitwa ESTA, anadai kuwa baada ya kujifungua na kuruhusiwa kurudi nyumbani, alianza kuona mabadiliko mwilini mwake, harufu mbaya ikautawala mwili na mazingira yote alipo kuwa. Ikawa kero kwa majirani na kwa kila mtu aliye pita karibu naye. Ndipo ESTA akarudi hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi kujua nini chanzo cha harufu hiyo. 

KUMBE! Gloves ilisahaulika tumboni wakati ma nesi wakimzalisha.
Jambo ambalo lilishangaza wauguzi wa pale na kusema Mungu wako unaemwabudu ndiye Mungu wa kweli kwani kwa hali ya kawaida usingepona.

Esta akishuhudia kanisani Ufufuo na uzima Kigoma.
 WAPATA MTOTO KWA NEEMA YA MUNGU.

Mr. & Mrs Emmanuel
Mr. & Mrs Emmanuel Haraka wakimshukuru Mungu leo katika madhabahu ya Ufufuo na Uzima Kigoma kwa kuwapa mtoto,
Kipindi cha ujauzito wake Mrs Haraka alipata misukosuko mingi; tangu ujauzito ukiwa na miezi 3 alianza kusikia machungu ya kujifungua, ujauzito ulipofikia kipindi cha miezi 5 alipimwa ikaonekaana kuwa kondo limetangulia mbele badala ya mtoto, hali hiyo iliendelea mpaka kipindi cha miezi 8 cha ujauzito wake.

Majeshi ya Bwana Ufufuo na Uzima yaliingilia kati baada ya kuona hali si shwari mpaka kondo likampisha mtoto na akazaliwa salama.
 

Comments