USIHADAIKE NA MIJI HII YA DUNIANI


Na Abel Suleiman Shiriwa
Watu wengi hapa duniani utawaona wakikimbizana kwenda NCHI za watu,
MAREKANI
UINGEREZA
CHINA
UFARANSA
JAPANI
DUBAI
HISPANIA
SOUTH AFRIKA

Na miji mingine mingi mizuri, Lengo lao hasa ni kuishi katika ufahari wa miji mizuri, maana hata mtu akiwa tu Dar es Salaam hujiona ni mtu aliye juu sana dhidi ya mtu aishie VILLAGE (Kijijini) wengine hukimbia hata kwao ili mradi aende katika miji mikubwa, mizuri, yenye kupendeza, Wakidhani kwamba ni miji ambayo wataendelea kuiona milele:- kuhangaika kumtafuta MUNGU, ambae yeye haitazamii MIJI hii tuitazamiayo sisi.
Waebrania 13:14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.
15 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.
16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.
17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
MUNGU anatutaka sisi tuutazamie mji udumuo (YERUSALEMU MPYA) ambao unatoka kwake yeye.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
MJI huo ndiyo mji ambao unadumu milele na Milele. mji huo ndiyo ambao kila mtu yampasa kuukimbilia, achana na mawazo ya
NEW YORK
LONDON
PARIS
JOHANESBURG
SHANGAI

Ni miji isiyodumu, ni miji ipitayo kama upitavyo wewe mwanadamu;- lakini YERUSALEMU MJI WAKE BWANA, ni mji wa milele ambao wale watakaouingia watakaa ndani milele, Lakini miji hii ya duniani unayoionea fahari, inayokufanya ufanye anasa, ukajirushe CLUB, DISCO, kubadili mademu, Kubadili mabwana, ni miji ipitayo, hata walioijenga nao vile vile wameshapita na wataendelea kupita.
2 Petro 3:11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake
14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
SINA LENGO LA KUKUFANYA UIDHARAU MIJI HIYO, au usiende kuishi huko, hapana, lengo langu ni kukumbusha kuwa usijisahau kwa sababu ya miji hiyo, au usiwadharau wale ambao hawana uwezo wa kufika huko, maana wakifika au wasipofika hakuna faida watakayoipata baada ya kufa.... zaidi ya kwenda katika moto wa milele:- lakini wale wadumuo kutenda mema hata kama wanaishi katika nyumba za tope, nyumba zisizo na umeme, wanayo faida ya kuishi katika mji ambao watauingia watakatifu, mji ambao hauna giza.
Ufunuo 21:23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.
24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.
26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.
27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
TAFAKARI KISHA CHUKUA HATUA.

Comments