ZIJUE SIRI ZA UFALME WA GIZA(2)

Na Nickson Mabena
Mungu akubariki unayeendelea kufuatilia mfululizo wa Somo hili, Niliishia kukuchambulia kwa sehemu Mambo mawili kati ya Nane niliyosema nitayafundisha, Bado tupo kwenye Msingi wa Somo..
Wakati nafikiria kuendelea na jambo la tatu, ndani yangu nimepata Msukumo wa kukuchambulia Andiko lifuatalo:
"Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamusha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana na pendo lake". KOL 1:13
Kazi kubwa aliyoifanya Yesu kwa wanadamu ni Kuwahamisha, Kutoka Ufalme mmoja na Kuwaingiza kwenye Ufalme Mwingine.
Uhamisho huo hufanyika kwenye Ulimwengu wa roho, ujue Mtu yeyote duniani, Kama hayupo chini ya Ufalme wa Giza basi yupo Chini ya Ufalme wa Nuru. Hakuna Mtu anayekaa katikati!.
Kama Hujaokoka, Ujue Upo Chini ya Ufalme wa Giza, na Kama Umeokoka Ujue Upo Chini ya Ufalme wa Nuru!.
Ambapo, Kazi Anayoifanya Yesu siku unaokoka ni KUKUHAMISHA toka kwenye Utawala wa Giza na Kukuingiza kwenye Utawala wa Nuru!.

Kwa jinsi ya Mwilini wewe unabaki kuwa wewe, Pengine Nyumba unayoishi ni ileile, Unatembea vilevile, lakini katika Ulimwengu wa roho, wewe sio yuleyule, bali umehamishwa!.
Ndio Maana tunachotarajia kuona kwa mtu baada ya Kuokoka ni Kubadilika kwa mfumo wa Maisha yake, kwani tayari amehamishwa kwenye ulimwengu wa roho!!.
Unapokua umehamishiwa kwenye Ufalme wa Nuru, ule ufalme wa giza, unapanga mikakati ya Namna ya namna ya kukurudisha Kwenye himaya yao.
Kumbuka hizi falme Mbili hazipatani hata kidogo!.
Shetani Anapambana Usiku na Mchana, Kuhakikisha Watu walio kwenye himaya yake, Wanaendelea kubaki kwenye himaya yake, na Wote waliohamishwa wanarudi kwenye himaya yake!.
Kwa Sababu hiyo, anaandaa mikakati Mbalimbali ili kuhakikisha Lengo lake linatimia...
Lakini, Maadam Yesu yupo hai, Na Anatenda kazi ya kuwahamisha watu hata leo, Nasema hivi, Watu lazima wahamishwe toka kwenye Ufalme wa Giza, na Kuingizwa kwenye Ufalme wa Nuru katika Jina la Yesu!.
Mungu anatamani tushinde, na tusije tukashindwa na Shetani, ndio maana Neno la Mungu linasema "Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake". 2KOR 2:11
Kumbe ni lazima tuzijue fikira za Shetani (Siri za Ufalme wake), ili asipate Kutushinda!.


3.KWATUMISHI KATIKA UFALME WA NURU NA UFALME WA GIZA!.
Nataka niwaelezee tu watumishi wa hizi falme Mbili, Tulishawaona Wakuu wa Falme hizi, Sasa tuwaone watumishi kwenye falme hizi.
a)WATUMISHI KATIKA UFALME WA NURU.
Hawa ni watumishi wote wa Mungu aliye hai, Yaani Wote WALIOOKOKA!.
Biblia inasema hivi "Bwana akamwambia Musa, Ingia kwa Farao, ukamwambie, BWANA asema hivi, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia". KUT 8:1
Mungu analitaja Lengo la Kuwatoa watu kwa Farao kwamba ni KUMTUMIKIA, na hivyo ndivyo ilivyo kwenye Agano Jipya, Kwamba Yesu anawahamisha watu toka kwa Shetani, ili wapate kumtumikia. Ndio Maana nasema, Wote Waliookoka na Watumishi katika Ufalme wa Nuru!.
Pia, Malaika ni Watumishi katika Ufalme wa Nuru, Wakati Mwingine Mungu huwatuma Malaika kututumikia.
Mfano, "Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako. Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote." ZABURI 91:10-11
Soma tena Zaburi 34:7
Malaika Pia ni Watumishi katika Ufalme wa Nuru, Wao ni Viumbe vya kiroho, kwa hiyo hushughulika sana kwenye ulimwengu wa roho.
Nisiandike sana, kuhusu hao... sio lengo langu hasa kwenye somo hili!.
b)WATUMISHI KWENYE UFALME WA GIZA!.
Hapa nawaongelea WACHAWI, WAGANGA WA KIENYEJI, MAWAKALA WA SHETANI, na Wengine Wengi ambao Shetani anawatumikisha!.
Wapo wanaomtumikia Shetani kwa Kujua, na wengine kwa kutokujua!.
Mara nyingi Wachawi, Waganga, na Mawakala wote wa Shetani wanajua kwamba Wanamtumikia nani!.
Lakini Wapo ambao hawajui, hawa ni Watu watenda Maovu, na Hawajui kwamba Hawapo sawa, wanajiona Wanamtumikia Mungu, Kumbe Shetani!.
Pia, Ibilisi ana malaika zake, ambao wana Majina Mengi Mfano, Mapepo, Majini, Mashetani, roho Chafu, roho za uasi n.k!.
Ona, "Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;" Math 25:41
Hao Malaika wa Shetani, ndio aliotimuliwa nao Kule Mbinguni, Baada ya Kushindwa Vita. Kisa hicho kipo Katika
Ufunuo 12:7
"Kulikua na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake".

Hao Ndio Watumishi katika Ufalme wa Giza, Wakifanya Vituko vingi, wakiwatesa wengi, Wakiwafunga wengi, na kuwasumbua wengi!.

Wengi Wamelazwa Mahospitalini wakati hawaumwi Magonjwa ya Kutibiwa hospitalini, Wengi wanafanyiwa Upasuaji kwa Hila za Shetani, Wengine wamekatishwa Masomo yao, kwa Mipango ya Shetani....
Na Mengine Mengi yanayotokea, ambayo Adui Shetani amekua akiwaonea Watu, kwa Sababu hawajui hila zake!..
4.JINSI UFALME WA GIZA UNAVYOTENDA KAZI.
Jambo la Muhimu kujua ni kwamba roho haina Mwili, wala Mifupa. Yesu baada ya kufufuka aliwaambia wale waliokua hawaamini kufufuka Kwake, "Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo". LUKA 24:39
Kwa kuwa roho haina mwili, naweza nikasema Majini hayana miili, ila yana uwezo wa kuvaa mwili wowote!.
Ndiyo Maana Pepo linaweza kuingia ndani kwako hata kama mlango umeufunga kabisa, kwa sababu roho yaweza kupenya hata ukutani!.
Mchawi akitaka kuingia ndani kwako, haji kwa jinsi ya kawaida ya kibinadamu, bali kwa jinsi ya roho... kwa sababu hiyo anaweza kuja kukuchukua ndani kwako, na kwenda kukufanyisha Kazi bila Mtu Mwingine kujua.
Mapepo yana Majina yao, mfano Maimuna, Subiani, Makata, Latifa, Simba n.k
(Msiwape watoto wenu majina ya Majini).

Sasa, anachokifanya Shetani, anakaa na Watenda kazi wake, na Kupanga jinsi ya kuwatesa wanadamu. Miongoni mwa vitu anavyovifanya ni Pamoja na Kuleta
👉Magonjwa ya Ajabu, mfano wa Magonjwa hayo ni Ukimwi, Kupooza, Kansa, Uvimbe kwenye Kizazi n.k 👉Kuharibu Mimba 👉Utasa 👉Vifungo vya Uovu, 👉Uzinzi 👉Ajali 👉Kuibiwa Nyota na thamani. 👉Kafara n.k
Ili kuhakikisha wanafanikiwa, Shetani anatuma roho (Mapepo) kwa ajili ya kufanya kazi hizo, Mfano kuna pepo la kuharibu Mimba!.
Pepo hilo kazi yake ni kuhakikisha kila mimba anayoshika Mwanamke husika, iwe inaharibika!. Sasa mtu pasipo kuwa na ufahamu wa Mambo haya, anakimbilia hospitali kwenda kupata Matibabu, na Anashindwa kuelewa. kwa nini haponi.
Au, Unashangaa Mtoto amepotea kwenye Mazingira ya kutatanisha, kumbe anakua amechukuliwa kichawi!.
Pia, Utaona Mtu amepooza upande wa kushoto!, hivi umewahi kwa nini Watu wengi kujiulizawaliopooza, Wanapooza Upande Mmoja, tena huohuo!??
Alafu, kuna Jini linaitwa jini Mahaba, lenyewe hufunga ndoa na wanadamu. Mtu umelala Usiku unaota Ndoto Unalala na Mwanamke, au Mwanaume.... Kila Mara hiyo ndoto inajirudia, alafu huna hamu tena ya kuolewa au Kuoa!. Wengine hupewa hadi Pete ya ndoa, Kuna wengine Hadi Wamezaa na Majini katika ndoto..
Suala la Ajali, Mimi sitakagi kuamini ya kwamba Ajali zote ni Uzembe wa madereva , nyingi sana ni za kutengeneza... Majini chakula chao ni Damu, ndio maana hufanya hivyo ili kupata DAMU!.
Jua kwamba, Mapepo nayo hufunga ramadhani, ndio maana Mwezi wa ramadhani kuna matukio huwezi kuyasikia hovyo!. Hata Waganga Wengi wanapumzika kufanya kazi zao za kiganga!.
Jambo la kushangaza lingine ni hili, Kuna Mapepo hutumwa kwenda kupandikiza Uchawi kwa Watoto wadogo!. Hii nilikutana nayo Tanga Mwaka Jana, ilinitisha Sana... Mama mmoja Mchawi tulipomkamata kwenye huduma, vibaraka wake wakatueleza hayo...
Suala lingine ni hili, linawapataga wanafunzi mara nyingi, UTAKUTA MWANAFUNZI KILA IKIKARIBIA MITIHANI ANAUMWA, AU WENGINE HUANGUKA Kama Mwenye Kifafa, hizo ni NGUVU ZA GIZA TU, hamna ugonjwa hapo!!

Kama unakumbuka kwenye Utangulizi, nilikwambia kwenye kipengele hiki cha nne ntakueleza roho kutoka kuzimu, na pia ntatumia Shuhuda ninazoziamini ili kukuthibitishia Kile ninachokuambia! Pia Utajifunza kupitia hizo.
NIANZE NA SHUHUDA MBILI, MUNGU AKINIPA NAFASI NITAKULETEA NYINGINE, SOMO LETU BADO NI REFU SANA!.
Shuhuda 1,
Siku moja nilipata taarifa ya kwamba dada mmoja kila akishika ujauzito, Mimba zinaporomoka, hadi wakati huo napata taarifa hizo tayari Mimba Mbili zilikua zimeharibika, ikabidi nifunge safari niende alipo, kwani nilikua najua chanzo cha tatizo, japokua wao walikua hawajui!.

Nilipofika nikataka kusikia kutoka kwake huyo dada ili nianze kumsaidia, Alianza kunieleza, kwamba zikifika tarehe fulani katika mwezi, usiku anaota kwamba amezungukwa na watoto, Akishtuka usiku huo tumbo linaanza kumuuma sana,
Ilimsumbua ile hali, ikabidi atafute msaada sehemu mbali mbali, akaenda hadi kwa waganga wa kienyeji bila mafanikio, ikabidi atafute Msaada wa kitaalamu, Akaenda kwa wataalam wakamfanyia vipimo, na kumpa dawa za awali, ili baadae akapate zingine, kusema kweli, zile dawa zilikua ni za bei mbaya saya sana, na ilikua ngumu kidogo kwa wao kuzipata hizo pesa!.
Alipomaliza kujieleza, nikamfungulia Maandiko, yanayoeleza Jinsi Yesu anavyoweza kutenda kazi.. Nilimsomea andiko hili, 1YOH 3:8b
".......Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi."
Nikamwambia Yesu alikuja kuzivunja kazi za Ibililisi, lakini cha Kwanza lazima Umkubali, UOKOKE!. Akakubali, nikamuongoza Sala ya Toba hapohapo!.
Ile naanza kumuombea juu ya Ugonjwa wake, Akaanguka Chini, Nikaendelea Kuomba, Mapepo yakalipuka!. Nikayabana sana ili nijue kwa nini yamemfunga Kizazi huyo Mwanamke...!.
Kumbe, Bibi yake alimchukua huyo mwanamke kichawi, na Kumfungia kwenye Chumba chake, Akamchukulia Watoto wake pamoja na Nyota yake, akavifungia kwenye Chupa, ili huyo Mwanamke Asizae Milele, kwa hiyo zile dawa zisingefanya kazi.
Baada ya kujua hayo, nikaamua Kuvunja ile chupa kwa njia ya Maombi, Chupa ikavunjika, Nikatumia Mamlaka ya Jina la Yesu kumrudisha huyo Mwanamke, yule bibi yake alilia sana, Ila nilimzidi nguvu akamuachia, akarudisha nyota yake, na watoto wake (KUMBUKA HAKUNA UMBALI KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NDIO MAANA ILE CHUPA ILIVUNJIKA KWA NJIA YA MAOMBI).
Yule mwanamke akafunguliwa, yale madawa aliyopewa kwa mganga nikaenda kuyachoma moto......
baada ya mda kidogo akapata Ujauzito, na Sasa Amejifungua Mtoto wa kike!.
Yale madawa ya bei mbaya yakageuka mapambo tu!.
Shuhuda 2,
Kuna Dada aliniambia kwamba, ana mdogo ake ambaye kila ikikaribia Mitihani anaumwa sana, na ile hali inamtesa mdogo wake huyo, akasema ana hitaji Maombi,

Nikamwambia anipe namba za Huyo Mdogo wake, nikawa nawasiliana naye, akanieleza mengi sana, nikapanga Mda wa kuomba naye kwa njia ya simu, kutokana na sheria za Shule kibana sana, huyo kijana ilibidi niwasiliane naye saa nane za usiku...
Niliongea naye, Nikamsomea maandiko, Ila alikataa kuokoka tu, Nikaomba naye kwa Njia ya Simu, kwa Kua hakuna Umbali kwenye Ulimwengu wa roho, yule kijana alikiri tatizo kupungua usiku ule baada ya Maombi,
Baada ya siku chache akafunguliwa kabisa, na Kipindi cha Mitihani hakuumwa tena, Akamaliza mitihani yake salama kabisa!.
Magonjwa kama haya yamekua mtaji kwa watumishi wengine, Utasikia Watu wakijigamba na kusema UKIJA KANISANI KWANGU KAMA HUNA MTOTO LAZIMA UPATE MTOTO..'..
Kumbe ni vitu vidogo sana ambavyo Mkristo yeyote anaweza kuvifanya Sio lazima awe mtume wala nabii!.
Kumbuka: "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele." YOH 10:10
YESU ANAO UZIMA, UZIMA HAUPO KWA MTUME WALA KWA NABII YEYOTE, AMUA KWENDA KWAKE KWA UJASIRI!!.

By Mwalm Nick 0712265856 Watsap#

Comments