HATARI YA KURUDI NYUMA

Na Frank Philip Seth

"Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha BWANA. Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote. Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe. Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza. Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya" (Mithali 1:28-33).
Bila shaka kuna tofauti kubwa kati ya mtu aliyemfuata BWANA, kisha akarudi nyuma na mtu yule ambaye HAMJUI BWANA, kwahiyo hajamfuata bado.
KURUDI nyuma ni neno linaloonesha kwamba mtu alichukua hatua fulani na sasa amerudi nyuma; hafanyi tena MATENDO ya KWANZA (Ufunuo 2:1-7 ).
Mtume Paulo alitazama na kusema, "je! Ni kitu gani kinitenge na upendo wa Kristo? Ni upanga, uchi, nk. " Wala yaliyo chini, wala yaliyo juu, hakuna cha kututenga na upendo wa Kristo. Sasa tazama, je! Umerudi nyuma? Je! Unajua "kurudi nyuma kwa wajinga kutawaua?" Ni kitui gani cha thamani kuliko upendo wa Kristo? au je! Ni kitu gani BWANA ameshindwa kufanya maishani mwako hata urudi nyuma na kumwacha?
Nimejiuliza kwanini UJINGA unahusishwa na KURIDI nyuma. Angalia, ulimfuata BWANA wa mabwana, Mfalme wa wafalme na ambaye anashika HATIMA yako. Je! Si UJINGA kurudi nyuma, kumwacha na kumfuata mwingine?
Nikatazama tena, "kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza"! Je! BWANA AKUNYIME mafanikio ili uwe na NIDHAMU? Je! UKIINULIWA unashindwa kumtii BWANA kwa kuwa YOTE yako mikononi mwako?
Mkumbuke BWANA katika kufanikiwa kwako na MHESHIMU kwa mali zako (simaanishi habari ya utoaji tu), yaani, ukiwa na MALI, je! Katika hizo UTAMHESHIMU Mungu wako na kumcha? Je! Utasimama katika kusudi lake hata uwapo tajiri na mwenye jina kuu?
Frank P. Seth

Comments