Kanisa la Pentecostal Assemblies of God (P A G) Kawe jijini Dar es salaam  chini ya Mchungaji kiongozi Elly Botto sasa limefungua tawi Kinondo barabara ya Wazo hill. na kufikisha matawi mawili baada ya tawi la kigamboni.
P A G Kawe ambalo ni maarufu kwa jina la Kawe Pentecostal Church linakua kwa kazi na BWANA YESU anatwaa utukufu katika ibada ya huduma kwa ujumla.
Kama vijana wa kanisani tulishiriki katika hatua ya ujenzi wa jengo hilo jipya la kanisa ambapo tuliambata na mchungaji Botto na vijana wengine wa kanisani.
Hii ilikuwa ni wiki iliyopita lakini wiki hii ujenzi umefikia hatua ya kuwekwa bati. ashukuriwe MUNGU BABA maana injili ya KRISTO inafika kila mahali. zifuatazo ni picha katika matukio ya siku hiyo muhimu kwa ajili ya kujenga jengo la kanisa tukishirikiana na wana kanisa wenyeweji ambao wanaongezeka kila kukicha.
Nikiwa na Mchungaji kiongozi Elly Botto na vijana wengine kutoka Kawe Pentecostal Church.

Ujenzi wa jengo la kanisa.



Issa Danda kutoka Kawe Pentecostal Church.

Paulo Kusayo kutoka Kawe pentecostal Church.



Nikiwa na watoto wa kanisa husika.

wageni wakipewa zawadi



Baada ya kazi ni msosi.

Comments