NI MUHIMU KUISHI MAISHA MATAKATIFU SIKU ZOTE.

Na Mtumishi Peter M Mabula.

BWANA YESU Atukuzwe Ndugu Yangu.
Karibu Tujifunze Neno La MUNGU.
Leo Tunajifunza Ulazima Wa Kuishi Maisha Matakatifu.


1 Petro 1:15 "bali Kama Yeye Aliyewaita Alivyo Mtakatifu, Ninyi Nanyi Iweni Watakatifu Katika Mwenendo Wenu Wote" . 

Ndugu, Tumeitwa Na KRISTO Ili Tupate Haki Ya Kuingia Uzima Wa Milele.
Aliyetuita Ni Mtakatifu Na Agizo Lake Tuwe Watakatifu.
Sio Kwamba Tujiite Watakatifu Bali Maisha Na Matendo Yetu Yautambulishe Kwamba Sisi Ni Watakatifu.

Utakatifu Ni Jambo La Lazima Kama Kweli Tunautaka uzima wa milele.
Utakatifu Ni Kutengwa Kwa Ajili Ya MUNGU.
Moja Ya Sifa Ya MUNGU Ni Utakatifu.
Utakatifu Ni Kutengwa Mbali Na Dhambi.
Ukitengwa Lazima Uwe Tofauti.
Unatengwa Siku Ulipompokea YESU KRISTO Kama BWANA Na Mwokozi Wa Maisha Yako.
Utakatifu Hutafutwa Kwa Bidii. 


Waebrania 12:14 ''
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona BWANA asipokuwa nao; ''

-Biblia Inasema Hakuna Atakayemuona MUNGU Asipokuwa Mtakatifu.
Maana Ya Andiko Hilo Ni Kwamba Uzima Wa Milele Wataingia Watakatifu Tu.
-Ukitaka Kuwa Mtakatifu Kaa Na Watakatifu Na Jifunze Kwa Watakatifu.
-Watakatifu Ni Wa Thamani Sana.
-Watakatifu Wametakaswa Kwa Damu Ya YESU Na Wanaishi Kama KRISTO Atakavyo.
-Watakatifu Ni Chumvi Ya Dunia. 

Mathayo 5:13 ''Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. ''
 
-Watakatifu Ni Nuru Ya Ulimwengu.

Mathayo 5:14-16 '' Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze BABA yenu aliye mbinguni. ''
 
-Watakatifu Wanaumtii MUNGU.
-Watakatifu Furaha Yao Ni Kumcha BWANA Na Kumtii.
-Watakatifu Huikimbia Dhambi Na Machukizo Yote.

Ni Muhimu Sana Kila Mkristo Kuishi Maisha Matakatifu.
-Watakatifu Wanaishi Na ROHO MTAKATIFU Na Kumtii Siku Zote.
-Watakatifu Hawawezi Kumkana BWANA YESU Wala Kumsaliti Mwamba Wa Wokovu Wao

Warumi 8:38-39 '' Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa MUNGU ulio katika KRISTO YESU BWANA  wetu. ''
-Watakatifu Ni Waliookoka Na Sasa Ni Viumbe Wapya, Ya Kale Yamepita Na Wala Hawana Mpango Wa Kuyarudia tena
2 Kor 5:17 ''  Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. ''
 
Ndugu Yangu, Kuishi Maisha Matakatifu Inawezekana Kabisa Kama Ukiwaza Uzima Wa Milele.
Ya Dunia Yote Yatapita Lakini Ukimchagua YESU Na Ukauvaa Utakatifu Wake, Hakika Utaurithi Uzima Wa Milele.
-Kuishi Maisha Matakatifu Ndani Ya KRISTO Ni Jambo La Lazima Kama Unautaka Uzima Wa Milele.
-Kuishi Maisha Matakatifu Ni Lazima Wala Sio Hiari.
-Kuukataa Utakatifu Ni Kumpiga MUNGU Na Kumpinga MUNGU Ni Kuupinga Uzima Wa Milele. 

Pia jambo hili ni muhimu kulijua; Utakatifu wa kanisani tu huku mitaani ukiwa mpagani haufai.
BWANA YESU asifiwe inatakiwa iambatane na utakatifu. Sio BWANA YESU asifiwe nyingi lakini utakatifu 0% . Biblia inasema "kila alitajae jina la BWANA na auache uovu.


2 Timotheo 2:19 '' Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, BWANA awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la BWANA na auache uovu.''
 
-BWANA anawajua walio wake, na walio wake siku zote walio wake BWANA YESU

-sio wasanii wa ibada 
-sio wasanii wa matendo mema 
Bali huishi matendo mema daima. 
Ndugu yangu, nakuomba ujue kwamba kila ufanyalo linajulikana mbele za MUNGU. 
Na ingekua vyema sana kwa kila mtu kujua kwmba kuna Uzima na hata jehanamu pia Ipo. BWANA YESU yupo tayari kukuokoa kama tu Leo ukiufungua moyo wako.
Ni heri kuokoka na kuanza kuishi maisha ya wokovu katika KRISTO YESU.
Nakutakia mema ndio maana nakuonya.
Ubarikiwe na BWANA YESU KRISTO aliye hai.

Kumbuka Kwamba 
 "Heri Wenye Moyo Safi; Maana Hao Watamwona MUNGU-Mathayo 5:8".
Wenye Moyo Safi Ni Wakristo Watakatifu.
Hao Ndio Watamuona BWANA.
Ndugu, Chukua Hatua. Okoka Na BWANA YESU Ataweka Matengenezo Mapya Ndani Yako.

Naamini kuna kitu umejifunza.
Tii neno La MUNGU na utapata raha ya milele.


-Ndugu,Naamini umejifunza na utachukua hatua
njema ya kumpokea BWANA YESU kama
hujaokoka ili awe BWANA na MWOKOZI wako
tangu leo na utaanza kuishi maisha matakatifu


KAMA UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO
HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO
UKAJIUNGE NA KUANZA KUISHI MAISHA
MATAKATIFU.


''BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele
zako mimi mwenye dhambi, lakini leo
nimetambua kosa langu na naomba unisamehe
dhambi zangu zote, nisamehe dhambi
ninazozikumbuka na pia zile ambazo
sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu cha
hukumu na uliandike jina langu katika kitabu
cha uzima. Neno lako katika Warumi sura ya 10
Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa
sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya
kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka.
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata
haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu
'' . BWANA YESU mimi nimekuamini leo na
hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na
hakika nimeokoka. Kuanzia leo Naufunga
ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa
matendo mema na matakatifu. BWANA nipe
ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda
dhambi na anasa zote za dunia. Kuanzia leo
mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU
mwenye haki zote. ninafuta laana zote na kila
roho ya shetani inayonifuatilia naiharibu kwa
jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU
linavyosema katika Yeremia sura ya kwanza
mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana
kwa kuniokoa. Yote haya kwa imani nimepokea
na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU
kunitumia. Katika jina la YESU KRISTO
nimeomba na kupokea .
Amen.''
Kama umetubu toba ya kweli hakika wewe
kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa. Kwa sasa
naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza
tena siku nyingine. ulishindwa kumpokea
BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa
kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima
na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho
kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na
wewe, hataki upotelee motoni anataka uende
uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU
akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments