TOFAUTI KATI YA ( KUUNGAMA DHAMBI, NA KUTUBU DHAMBI ) =

Na Mtumishi Moses Katindasa, Zanzibar.

Maneno haya , Kuungama dhambi, na Kutubu dhambi, ukiyachunguza kwa halaka halaka unaweza ukasema kwamba yanamaana moja, lakini sio kweli,
=
Kuungama dhambi, haimaanishi ni Kutubu dhambi, na Kutubu dhambi, haimaanishi ni Kuungama dhambi, haya ni maneno mawili tofauti, na pia yamaana zisizofanana,
=
NGOJA TUCHUNGUZE MAANDIKO ILI TUPATE KUFUNDISHANA VEMA
.
Tukisoma Biblia katika Kitabu cha
1YOHANA 1:9, imeandikwa => TUKIZIUNGAMA DHAMBI zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata ATUONDOLEE DHAMBI ZETU, na kutusafisha na udhalimu wote.
(zingatia maneno yaliyo katika herufi kubwa)
=
Ukisoma kwa sura ya Uchunguzi ktk andiko hapo juu, utatambua kuna maneno mawili ambayo ni Muhimu sana yaliyoibeba Sura hiyo,
(A) Tukiziungama dhambi zetu, na
(B) Hata atuondolee dhambi zetu.
=
Je, nini maana ya KUUNGAMA DHAMBI ?
.
KUUNGAMA DHAMBI ni kukubali, au kukiri kwamba wewe umetenda dhambi,
=
Je, nini maana ya KUTUBU DHAMBI?
.
KUTUBU DHAMBI ni kumwambia Mungu akuondolee , au akufutie dhambi ulizo zitenda baada ya wewe kukubali yakwamba ni kweli umetenda dhambi.
=
Mtoto mwenye adabu njema, anatambua kwamba amekosa, naye anaogopa kuadhibiwa kwa kosa alilotenda, humuendea baba, au mama, na kumwambia,
.
Baba, au Mama, Mimi nimeharibu kitu furani, lakini ni kwabahati mbaya, sijakusudia kuharibu, kwahiyo ninaomba Unisamehe.
=
Jambo la kwanza mtoto huyu amekiri (amekubali) kwamba yeye ndiye aliye haribu,
.
Na jambo la pili, ameomba msamaha ili asamehewe kwa kosa alilolifanya.
=
Kwahiyo,
Kuungama dhambi => ni kukubaliana na Mungu kwamba wewe ni mwenye dhambi, au umetenda dhambi,
.
Na Kutubu dhambi => ni Kumwambia Mungu, au kumuomba akuondolee (akufutie) dhambi ile uliyoitenda ambayo wewe umeikubali.
=
Kwanza Unakubali kwamba wewe ni mwenye dhambi, na baada ya hapo ndipo unatubia uovu wako,
.
Huwezi kutubu ikiwa umekataa kwamba wewe haukutenda kosa lo lote.
=
Ngoja tuangalie hapa kwa ufupi tu.
.
MITHALI 28, 13, Afichaye dhambi zake hatafanikiwa, Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba,
.
Mtu anayekataa kwamba yeye hakutenda dhambi, hawezi kusamehewa, huyo atabaki na dhambi zake, lakini Yule mtu anayekubali kwamba ametenda dhambi, na akaacha dhambi, huyo ndiye atakaye samehewa.
=

Comments