UNAO MUDA MCHACHE, UTUMIE VYEMA.

Na Mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Nakuomba usome ujumbe huu hadi mwisho.
Karibu uijue na kuitambua kweli inayoweka huru watu walio tayari kuwekwa huru.
Usiichezee wala kuijaribu Neema ya MUNGU ndugu yangu.
Usione kwamba muda unao sana hata huoni umuhimu wa kuokoka leo.
Usipoteze muda wako katika mambo ambayo hayakujengi kiroho.
Kumbuka kwamba siku ya mwisho hata kazi yako haitakuwa na maana sana hata kama ilikupotezea muda mrefu.
''Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.-Mathayo 11:12''
-Wanaoupata ufalme wa MUNGU ni wale ambao wamewekeza rohoni na sio mwilini.
-Walioupata ufalme wa MUNGU ni wale waliompokea BWANA YESU na kuishi maisha matakatifu siku zote.
Inawezekana kabisa ka dhambi kadogo tu kamekushinda kukaacha na hujui hata kwanini huachi. Kumbe tatizo ni muda wako unautumia vibaya.
Huna hata dakika 50 kwa siku kwa ajili ya MUNGU lakini muda wa kuangalia filamu au tamthilia unao. muda wa kuangalia mpira au kusikiliza miziki ya kidunia unao.
Muda wa kufanya jambo lolote unao isipokuwa muda wa kwenda kanisani tu ndio huna.
Muda wa kila jambo ulitakalo unao lakini muda kwa ajili ya mambo ya MUNGU tu ndio huna.
Ndugu.
''Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.-Obadia 1:15''

-Neno la MUNGU lipo na halibadiliki.
Neno linasema siku ya BWANA i karibu, kila mtu atalipwa sawa na matendo yake yalivyo.
Kuna wakati natamani nimfuate kila mtu na kumwambia aokoke na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Kuna wakati natamani MUNGU ampe kila ndugu na rafiki yangu moyo wa toba.

Watu wengi leo hawataki neno la MUNGU la uzima.
Kuna wengine husikiliza neno la MUNGU la kweli kama hili lakini halifuati wala kulitii.
Kuna wengine hutii neno la MUNGU kwa sabab tu ya magumu wanayopitia lakini akipata hitaji lake anamsahau MUNGU.
Ni hatari sana.
Ndugu yangu, uzima wa milele n wako binafsi na sio wa jumuiya.
Kama mwenzi wako wa ndoa ndie chanzo cha wewe kumwacha YESU nakupa pole maana bado hujatambua kwamba uzima wa milele hamtashare bali kila mtu sawasawa na matendo yake.
Kila siku MUNGU BABA ananipa ujumbe ili tu ndugu yangu usikose uzima. MUNGU kila siku anawapa watumishi wake mbalimbali neno lake ili tu Mwanadamu usiende jehanamu lakini binadamu waliowengi wanaona kawaida kawaida tu.
Ndugu yangu, nakuomba uone kila kitu cha kawaida kawaida lakini sio Neno la MUNGU.
Anapofariki mtu tunalia na kuomboleza lakini ukweli ni kwamba zamu yake yeye amemaliza na ameenda ama mbinguni ama kuzimu kutegemea na matendo yake. lakini kifo chake ni taarifa kwetu kwamba ipo siku tena inakuja siku hiyo ambapo hata sisi tutaondoka duniani.
Shetani alivyofunga watu unaweza ukaona mtu analia msibani lakini akiondoka hapo anaenda kufanya uzinzi na uasherati.
Mtu analia msibani lakini jioni ya siku hiyo hiyo anaenda dhambi kama kawaida.
Ndugu zangu ni wakati wa neema lakini neema hiyo ina mwisho.
Mwenye sikio la kusikia na asikie leo.
Siku moja katika maono nilimuona BWANA YESU amesimama kwa mbali kidogo na pale nilipokuwa mimi na watu wengine wengi. akaniita nikaenda, nilipoenda alipo akanionyesha kitabu cha uzima, nikaliona jina langu humo na majina machache ya watu ninaowafahamu.
Baada ya kuliona jina langu BWANA akanituma niende nikawaambie wanadamu kwamba wampokee yeye na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Lilikuwa jambo la ajabu sana lakini kwenye maono nilijiona nikienda na kuwaeleza wanadamu, kuna ambao nilikuwa mpaka nawaambia na kuwalazimisha waokoke, niliifanya kazi hiyo kwa muda mrefu. kuna waliookoka na wengine hawakuokoka, baadae BWANA YESU akasema inatosha akaniiita niende alipokuwa amesimama yeye, nikaenda.
Ndugu nakushauri kumpokea YESU na kuanza kuishi maisha matakatifu kuanzia leo.
Hatuna injili nyingine zaidi ya Wokovu wa BWANA wetu YESU KRISTO aliye pekee na uzima wetu wa milele.
Wakolosai 3:5-10 '' Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya MUNGU.Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo.Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. ''
Ndugu yangu, tunapohubiri injili ya KRISTO inayookoka hatuhubiri jambo ambalo ni labda tu kuwepo, bali tunahubiri jambo ambalo ni ndio katika ndio tena ni kweli katika kweli zote.
Kama kweli wewe binafsi unautaka uzima wa milele nakushauri kimbilia kanisa la kiroho na ukaokoke kisha kuanzia leo anza kuishi maisha matakatifu.
Wokovu ni wako binafsi na sio wa ukoo wala familia yako.
Ukisema kwamba unafuata mila au taratibu za ukoo wako haitakusaidia.
Kama unasubiri hadi baba na mama yako waokoke ndio na wewe utampokea YESU hiyo haitakusaidia.
Neema ipo leo na neema hiyo nakuomba sana uitumie vizuri.
Heri kuokoka kuliko kujifurahisha kwenye dhambi kisha ukifa unaenda kulia milele jehanamu.
BWANA YESU anaokoka na ukimpokea leo hakika unaokoka.
Saa yako moja inaweza kuamua ni wapi utaenda baada ya kufa.
Muda wako wa leo ni muhimu sana kuliko muda wa kesho.
Itumie leo vizuri ndipo utakapoiona kesho yako ikiwa vizuri zaidi.
BWANA YESU amenituma kwa ndugu zangu wote na marafiki.
Mwenye sikio LA kusikia na asikie Leo na kuchukua hatua.
Jehanamu inawangoja watenda dhambi lakini ashukuriwe MUNGU maana mbingu inawasubiri watakatifu wa MUNGU.

Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO aliyenipa ujumbe huu ana
makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee
motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO
BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
MUNGU akubariki sana uliyesoma

Comments