
Akizungumza
jana katika kanisa hilo lililopo Ubungo huku akishangiliwa na waumini
wake waliokuwa wakiimba; “mshenga, mshenga, mshenga...’ Gwajima alisema
kuna watu wanaodhani kwamba atazungumza masuala ya Dk Slaa kanisani
hapo.
“Leo
sitazungumzia masuala hayo hapa kwa kuwa hili si pango la wanyang’anyi
ila nitazungumza na vyombo vya habari Jumanne ijayo (kesho),” alisema.
Jumanne
iliyopita, Dk Slaa alimwita Gwajima kuwa ni mshenga akisema ndiye
aliyefanya mipango ya kufanikisha mkakati wa Waziri Mkuu wa zamani,
Lowassa kujiunga na Chadema kwa kumkutanisha na viongozi wa chama hicho.
Gwajima alikiri kuwaunganisha Chadema na Lowassa na kueleza kuwa amekuwa rafiki wa wote hao.
Gwajima
alisema mkutano na wanahabari utafanyika kesho saa 7 mchana katika
Hoteli ya Landmark Ubungo na utarushwa moja kwa kwa moja na televisheni
kadhaa.
“Kwa
hiyo hapa leo tusikilize neno la Mungu masuala mengine hapa si mahali
pake tusubiri siku hiyo nitakayokuwa Landmark,” alisema.
Alisema mkutano huo utakaochukua saa moja utaanza saa 7.00 mchana.
Comments