KUISHI NA KRISTO MOYONI MWAKO NI UZIMA.

Na Mtumishi Peter Mabula.


BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu katika ujumbe huu mzuri.
Kuishi na KRISTO moyoni mwako ni ulinzi na uzima .
KRISTO ataishi moyoni mwako kama tu utampokea.
KRISTO ukimpokea anamtuma ROHO MTAKATIFU kuja kwako na ROHO wa MUNGU  ndio msimamizi wa Wokovu wako. ndio maana ninasema
Kuishi na KRISTO moyoni mwako ni ulinzi na uzima kwako.
''Nawe utakuwa salama, kwa sababu kuna matumaini; Naam, utatafuta-tafuta kando yako, na kupumzika katika salama. Tena utalala, wala hapana atakayekutia hofu; Naam, wengi watakutafuta uso wako.-Ayubu 11:18-19''
Iko heri kuwa ndani ya BWANA YESU, uko ushindi na uzima, iko amani na baraka kuu.
''Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,-Zaburi 91:5''
Wakati wengine wakiogopa paka wanaolia usiku nje ya nyumba zao, wewe utalala salama maana BWANA anakulinda.
''Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. -Mithali 3:24''
Mtu wa KRISTO hulindwa na nguvu za KRISTO.
Damu ya YESU ni ulinzi mkuu sana.
Jina la YESU halijawahi kushindwa na ndio jina pekee ambalo wachawi, majini na kila wakala wa shetani huliogopa.
YESU haji kutusaidia bali huja kutushindia.
Kuishi na KRISTO moyoni mwako ni ulinzi na uzima.
''Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, BWANA, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama. -Zaburi 4:8''
Tunapompokea YESU tunapata kibali cha kiMUNGU.
Tunapompokea YESU majina yetu yanaandikwa katika kitabu cha uzima.
Tunapompokea YESU tunatengwa na uonevu wa shetani na sasa tunaanza kulindwa na MUNGU.
''Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.-Zaburi 3:5''
Kuna faida kuu kuwa ndani ya BWANA YESU.
Kuna amani kuu ukiwa ndani ya BWANA YESU.
Kuna furaha kuu ukiwa ndani ya YESU.
Kuna baraka na ushindi mkuu ndani ya YESU KRISTO.
Aliyetoka juu yu juu ya yote, na hakuna aliyetoka juu ila BWANA wetu YESU KRISTO.
''Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.-Yohana 3:31''
wa chini ni shetani  lakini aliyetoka juu mbinguni ni BWANA YESU na huyo ndio aliye juu ya yote. shetani hana nafasi ya ushindi hata moja kwa watu wa KRISTO.
shetani huliogopa sana jina la YESU KRISTO.
''Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA. -Isaya 59:19B''
Iko furaha kuu ndani ya jina la YESU KRISTO.
Kuishi na KRISTO moyoni mwako ni ulinzi na uzima.
''maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika MUNGU hata kuangusha ngome;tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya MUNGU; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii KRISTO;-2 Wakorintho 10:4-5''
BWANA YESU alikuja ili tu tuwe huru mbali na maonezi yote ya shetani.
Ndugu, ongeza imani yako katika BWANA YESU, omba na ushindi kwako ni lazima maana aliyetoka juu mbinguni ndiye aliye juu ya yote.
''Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika BWANA na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.-Waefeso 6:10-11''
Ni muhimu sana kuvaa silaha za MUNGU na ushindi kwako utakuwa ni lazima.
Silaha za MUNGU ni;
- Jina la YESU KRISTO.
-Damu ya YESU KRISTO.
-Neno la MUNGU.
-Maisha matakatifu.
-Utoaji.
-Moto wa ROHO MTAKATIFU.
-Kweli na Haki.
-Imani N.k.
''Naye BWANA, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike. -Kumbukumbu la Torati 31:8''
Kuna furaha na ulinzi katika BWANA YESU.
Mamlaka ya KRISTO ni kuu sana na haijawahi kushindwa popote na kama tukiwa na Jina la YESU hakika tutaishi maisha ya ushindi.
Maombi ya mteule mmoja yanaweza kuharibu mamia ya adui katika ulimwengu wa roho.
''Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, MUNGU wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.-Yoshua 23:10''
Kuishi na KRISTO maishani mwako ni ulzima na ulinzi mkuu.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine. Kama ulishindwa kumpokea BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili

Comments