MAKANISA MATATU YACHOMA MOTO MKOANI KAGERA.



WATU wasiojulikana wamechoma moto makanisa matatu ya Kipentekoste katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, usiku wa kuamkia jana. Makanisa hayo yaliyochomwa moto ni Pentecostal Assemblies of God (P.A.G) lililoko eneo la Buyekera, kata ya Bukoba, Living Water International na Evangelical Assemblies of God (E.A.G), yote yako katika eneo la Kashura.

Akizungumzia tukio hilo, Mchungaji wa Kanisa la Living Water International, Vedasto Athanas alisema saa 10 alfajiri alipigiwa simu na jirani yake kuwa kanisa linaungua moto na kukimbia kwenda eneo la tukio.

Waumini wa <b>makanisa</b> hayo wakiwa wamekusanyika kushuhudia tukio hilo. Mchungaji Athanas alisema baada ya kufika eneo la tukio alikuta moto mkali ambao wasingeweza kuuzima na kuwa vitu vyote vilivyokuwa vimebaki kanisani humo viliteketea kwa moto, ikiwamo viti 60, meza, benchi, vifaa vya ujenzi na madhabahu.

Alisema hawajafahamu akina nani wamehusika na tukio hilo, lakini alidai waliponusa baadhi ya vitu walisikia harufu ya mafuta ya taa, hali iliyowafanya wahisi kuwa wachomaji walitumia mafuta ya taa kuliteketeza.

<b>MAKANISA</b> <b>MATATU</b> <b>YACHOMWA</b> <b>MOTO</b> BUKOBA - Global Publishers Alisema kuwa hili ni tukio la tatu la kuchoma makanisa ya Living Water International na kuwa kanisa la kwanza lilichomwa Septemba mwaka 2013 na jingine likachomwa Aprili 2014.

Kwa upande wake, Mchungaji Alistides Kabonaki wa E.A.G, alisema saa 11.50 asubuhi aliitwa na msichana wake wa kazi za ndani na kumweleza kuwa kuna moto katika kanisa lao. Kabonaki alisema kuwa kanisa lake lote limeteketea pamoja na mali zilizokuwemo na kuwa hajafahamu waliohusika na uchomaji huu.

Alisema tayari wametoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa na Polisi na kuwa wanasubiri hatua za kiuchunguzi za jeshi hilo ili kubaini waliohusika na sababu za kufanya hivyo. Alisema kabla ya uchomaji huo watu wasiofahamika walivamia kanisa lao na kuiba baadhi ya mali zilizokuwemo ikiwamo viti na vitambaa vya madhabahuni.

Mwananchi ambaye ni jirani wa Kanisa la E.G.T, Regina Bakera, akizungumzia tukio hilo alisema yeye kama muumini amesikitishwa na matukio hayo na kuwa hawafahamu yanasababishwa na nini.

Bakera alisema matukio hayo yanadhihirisha kuwa kuna kikundi kilichoandaliwa kwa ajili ya kuchoma makanisa na kuiomba serikali kuyashughulikia kwa kufanya upelelezi wa kina. Kutokana na uchomaji wa makanisa hayo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wachungaji katika Mkoa wa Kagera, Crodward Edward alisema wamepanga kufanya maandamano ya kulaani kitendo hicho.

Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi alisema kwa sasa yuko safarini na kuwa atatoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo baadaye akisharejea Bukoba.

Comments