Mtume Peter Abubakar afungua tawi jipya la kanisa lake.


Mtume Peter Rashid Abubakar ambaye ndiye mwanzilishi wa kanisa la Glory to God Miracle Centerm, amefungua tawi la kanisa lake Tabata Relini na kumsimika mchungaji  Alpha Patrick Chikoti kuwa msimamizi wa huduma hiyo mpya.
 Mtume Peter Rashid Abubakar ambaye aliokolewa na BWANA YESU kutoka katika uchawi na uganga kwa sasa anamtumikia MUNGU aliye hai katika viwango vikubwa sana.
Kwa sasa kanisa hilo lina matawi kadhaa na tawi jingine likiwa nchini Kenya.
Huduma hiyo imedhamilia kuongeza upelekaji injili kwa mataifa kama agizo la BWANA YESU linavyosema na ndio maana wamefungua huduma huko Tabata.
Agizo la BWANA YESU linasema ''Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.-Marko 16-15-18''

Agizo hilo sasa linatimizwa na huduma nyingi ikiwemo huduma ya Mtume Peter Rashid Abubakar.
Hizi hapa Picha chache za matukio katika huduma hiyo mpya ya kanisa la Glory to God Miracle Center.
Mtume Peter Rashid Abubakar akimtambulisha Pastor Alpha Patrick Chikoti kuwa ndiye atakayesimamia kanisa la Tabata Relini jijini Dar Es Salaa

Pastor Alpha Patrick Chikoti wa Glory to God Miracle Center (The House Of Prayer For All Nations ) akiwa amekaa na Dadake na Magdalena Rashid Abubakar(Hapo mwanzo aliitwa Saada but sasa ameokolewa na Yesu.
Mtume Peter Rashid Abubakar akiwa madhabahuni na Askari wake  Katika ibada jana Tabata Relini jijini Dar Es Salaam


 Binti Akishuhudia jinsi miguu yake ilikuwa imevimba kama matende but kwa maombi ya Mtume Peter Rashid Abubakar, Mungu amemponya Tabata Relini


Wakati wa maombezi.

Comments