NI WAKATI WA KUJITAFAKARI, JE UNAKUWA KIROHO AU HUKUI?

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Ni Wakati Wa Kujitafakari, Je Unakua Kiroho Au Hukui?
 Kama Hukui Kiroho, Je Ni Kwa Nini? 
Kama Umedumaa Kiroho Unadhani Ni Kwa Nini? 
Kama Unakuwa Kiroho Je Unajuaje? 
 Warumi 6:13 ''wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa MUNGU kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa MUNGU kuwa silaha za haki.''
-Andiko hili linaonyesha kwamba kwamba kumbe mabadiliko lazima yatokee, kama zamani tulivitoa viungo vyetu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, basi sasa tunatakiwa tuvitoe viungo vyetu kuwa silaha za haki huku tukiishi maisha matakatifu. hayo ni mabadiliko na huko ni mwanza wa kukua kiroho yaani umejitenga na dhambi.

Tangu Ulipompokea YESU Lazima Kuna Mabadiliko Mazuri Yametokea Kwako. Kama Hakuna Mabadiliko Mazuri Kuna Haja Ya Kujitafakari. 
-Mabadiliko Ni Gharama Ya Mtu Mwenyewe, Mabadiliko Sio Kushinikizwa Na Mtu. 
-MUNGU Hufanya Mabadiliko Kama Ukiamua Wewe.
BWANA anasema 
''Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;-Mathayo 7:24'' 
-Kumbe ili kukua ni muhimu kuyasikia maneno ya MUNGU na kuyafanyia kazi.
-Lengo letu la kumpokea YESU na kisha kuanza kujifunza neno la MUNGU ni ili tupate uzima wa milele.
-Kujifunza neno na kulitendea kazi ndio huzaa kukua kiroho. 
Kumbe ni muhimu sana kulisoma neno na kulitakari kwa kina kisha kulitendea kazi maana hivyo ndivyo tutakavyokua kiroho.
Kwanini ni lazima kukua kiroho?
Ni kwa sababu;
 Tunatazamia Kule Mbinguni Kwa BABA Kwenye Makao Yale Ya Milele Aliyoyaandaa.
Yohana 14:1-3'' Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi. Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.'' 
-Hii ni ahadi njema sana ya BWANA YESU kwetu lakini katika safari yetu ya duniani tunatakiwa sana tukue kiroho ndipo itakavyokuwa rahisi kwetu kuingia katika uzima wa milele, maana adui naye hutaka kuwakosesha wanadamu kuingia uzima wa milele hasa wale ambao wameshindwa kukua kiroho. Biblia bado inasema kuhusu ahadi ya ajabu ya uzima wa milele kama tutashinda ya dunia.
 Tito 2:13 ''tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU mkuu na Mwokozi wetu;   ''
-Je ukijitafakari unaona umekua kiroho au hukui kiroho?
Kama hukui je ni kwanini?

Kuna watu hata hawajampokea BWANA YESU na hawa ili ahadi ya uzima wa milele iwapate ni lazima kwanza waokoke na kisha baada ya kuokoka wanatakiwa wakue kiroho ili kuweza kuhimili changamoto za duniani.

 Neema Ya Wokovu Bado Ipo. 
Ukiambiwa Neema Bado Ipo Maana Yake Ipo, Siku Hiyo Neema Itakuwa Haipo Ndio Maana Wakati Huu Ndio Wakati Pekee Wa Kuingia Kwenye Wokovu. Ni Saa Ya Kuokoka.
 Tukio La Kumpokea YESU Na Kuanza Kuishi Maisha Matakatifu Limefungwa Kwenye Muda, Huo Muda Ukiisha Ndugu Hautakuwa Tena Duniani. 
 Mithali 28:13 ''Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema'' 

Fanya Utani Kwenye Vyote Lakini Sio Uzima Wa Milele. 
Neno Kama Hili Linaweza Kuwa Shahidi Siku Ile,  Lakini Kwanini Uende Sehemu Mbaya Wakati BWANA YESU Yupo Kwa Ajili Yako? 

Ndugu, kutubu Na Kugeuka Na BWANA YESU ni jambo la lazima

Hakuna haja ya  Kung'ang'ania Dhambi Maana Dhambi Huzaa Jehanamu. 
 2 Kor 5:17 ''Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya''.
-Baada ya kukoka mwanadmu anakuwa kiumbe kipya na  upya huo huambatana na kuishi maisha mataktifu na ukikuwa kiroho itakusaidia zaidi katika maisha yako ya wokovu.
Usikubali kuwa kama Kaini 

Kaini Aliambiwa Na BWANA "Ukifanya Vyema Hutapata Kibali?" Kumbe Ukifanya Vyema Kwa Kuamua Vyema Unapata Kibali Na Haki Ya Uzima Wa Milele lakini pia ili ukue kiroho ni muhimu kujiunga na kanisa la kiroho.
 Waefeso 4:22-24 ''mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli'' 
Leo sina mengi sana ila naamini kuna kitu umejifunza.

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.


Comments