UTAJIJUAJE KAMA WEWE NI MZAZI UNAYELEA WATOTO WAKO KWA MABAVU?

Na Mchungaji Peter Mitimingi.

Unajaribu Kuwatia Aibu Watoto Wako Kwa Tabia Zao Mbaya.
1. Wazazi wanaolea kwa mabavu ni wakali, waweza kusema maneno kama “wewe sio msikivu” au “nirudie kukuambia mara ngapi jambo moja ?”
2. .
3. Wazazi hawa wanaweza kuwaita watoto wao majina ya wanyama tena wanyama wenye tabia mbaya.
Mfano: Nguruwe wewe, Ngombe mkubwa, Paka au Nyau wewe, nyani au wewe chizi nk.
4. Wazazi hawa hawajali kujenga au kutengeneza uwezo wa mtoto kujitambua wenyewe. Mtoto anakuwa hajajengewa uwezo wa kujitambua na kujikubali mwenyewe.
5. .
6. Kwa ujumla wanadhani kumdhalilisha mtoto ni njia nzuri ya kumfanya awe na ari ya kuwa na tabia njema hapo baadae kumbe ndio uua ule utu wa ndani wa mtoto "low self-esteem"
7. .
8. Wazazi wengine huwazalilisha kwa kuwasema vibaya mbale za watu au mbele za watoto wenzao au hata kuwaadhibu mbele ya watoto wenzao au kundi la watu.

Watoto Wanao Kojoa Kitandani na Kudharirishwa na Wazazi. (Kindumbwendumbwe)
Kwamfano kuna baadhi ya wazazi mtoto anapokuwa anatabia ya kukojoa kitandani huwapaka masizi na kuwavua nguo na kuwatembeza barabarani na watoto wenzao kuwaimbia "kindumbwendumbwe" huku kundi la watoto wa mtaani wakicheka na kumzungusha mtoto huku na kumwita kikojozi.
Huu ni uharibifu mkubwa sana katika moyo wa mtoto. Kama sio neema ya Mungu mtoto huyu anaweza kukua na kidonda hiki kwa miaka mingi sana kwa wengine ni kinyongo mpaka anaingia kaburini ingawa wengine wanakuwa hawasemi wala kuonyesha kinyongo hiki ila wanabakinacho moyoni. Ndio maana watoto waliolelewa katika malezi haya hata wakiwa watu wazima huwa hawana furaha wala mapenzi mema na wazazi wake maana walijeruhiwa jeraha kubwa sana.
Mfano:
• Mtoto alimuuza baba yake mzazi kwa 20,000Tsh kwa watu waliokuwa wakitafuta kununua viungo vya sehemu za siri za mwanaume.
• .
• Baba alikuwa anamchukia sana mtoto kiasi kwamba hataki apewe chakula. Mama yake alikuwa anamuibia chakula na kumuwekea kwenye banda la mbwa ili alie huko baba yake asije akamuona anakula chakula.


 ATHARI ZINAZOMKUMBA MTOTO ANAYELELEWA KWA MALEZI YA MABAVU.
Watoto wanaokuwa katika malezi ya kimabavu hujikuta wanafuata sheria kila wakati, hali hii inaweza kuwaletea matatizo mbalimbali kama vile:
1. Tatizo la kutokujiamini.
2. Tatizo la kutowaamini wengine pia.
3. Wakati mwingine watoto huwa na tabia za ukali.
4. Huwa na hofu na wasi wasi mara kwa mara.
5. Watoto kuwa na hali ya ukorofi hasa anapo kuwa nje na wazazi.
6. Kuwa na nidhamu ya uwoga akiwa mtoto na hata akiwa mfanyakazi.



WAZAZI WANAOJUA KUADHIBU TU WATOTO WANAPOKOSEA, LAKINI HAWAJUI KUMPONGEZA MTOTO ANAPOFANYA VIZURI!
Unapendelea Kutumia Adhabu Kuliko Kuwapongeza Watoto
Wengi wa wazazi wanaolea kwa kutumia nguvu, hawa amini katika kuwapongeza watoto wao kwa kufanya tabia njema. Wanawaza kuwa watoto wanatakiwa wawe na tabia njema na hawana haja ya kupongezwa kwa kufuata kanuni. Vile vile pale ambapo kanuni inapokuwa imevunjwa, athari yake huwa inaonekana mara moja.

Wazazi katika hundi hili:
1. Macho yao huona makosa tu.
2. Macho yao hayawezi kuona wala kumulika jema lolote linalofanywa na mtoto.
3. Ni wazazi ambao siku zote hutoa lawama tu kwa mtoto.
4. Ni wazazi ambao hakuna siku wanaweza kumpongeza mtoto kwa chochote hata pale ambapo mtoto anapokuwa amefanya vizuri.
5. Watoto wenye wazazi kama hawa huvunjika moyo na kujidharau sana.
6. Mtoto akifanya mambo mengi mazuri haambiwi chochote.
7. Mtoto akifanya jambo moja dogo baya linainuliwa kama bendera na mara kwa mara litakuwa linarudiwa rudiwa kusemwa semwa kama wimbo wa taifa.

Comments