WALINZI WA NGOME

 Na Mch ISAYA KILYINGA, UFUFUO NA UZIMA KILOMBERO.
Kuna mambo mawili, ngome na pili walinzi. Walinzi wanalinda chochote kisiingie au kutoka kwenye ngome bila ruhusa maalumu. Umeshindwa au kuteswa kwa muda mrefu bla kujua kwa nini, kumbe kuna walinzi wanaolinda ili usitoke.
Yoshua 2:1-3
1 Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.
2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi.
3 Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi.
Yeriko ilikuwa ni ngome iliyojengwa na kufungwa kwa sababu ya wana wa Israel na hakuna aliyeweza kotoka au kuingia. Ilikuwa ni kutumikishwa na kuteswa. Ngome hii ilijengwa kwa makafara, iliimarishwa na walinzi wa ngome, na yeyote aliyetaka kutoka ndani ya ngome walizuiliwa.
Ngome hizo ni mashetani yanakaa ndani yako ili kutawanya kila unachofanya,na maisha yako yasifike kule unapotaka.
Mwanzo 19:1-3
Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.
3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.

Shida uliyonayo inawezekana kuna ngome yenye walinzi wa kukuzuia usitoke hapo ulipo,wamekuwekea ngome iendelee kukulinda ili usifanikiwe. Ili ushinde lazima uipige ngome kwanza
1Samwel 13:3
3 Yonathani akaipiga hiyo ngome ya Wafilisti, iliyokuwako huko Gibea, nao Wafilisti wakapata habari. Naye Sauli akapiga tarumbeta katika nchi yote, huku akisema, Na wasikie Waebrania.

1Samweli 14:1
1 Basi ikatukia siku moja, ya kwamba Yonathani, mwana wa Sauli, akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na tuwavukie Wafilisti ngomeni, pale ng'ambo ya pili. Walakini hakumwarifu babaye.
6 Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini Bwana atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia Bwana asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache
11 Basi, hao wote wawili wakajidhihirisha mbele ya ngome ya Wafilisti, na wale Wafilisti wakasema, Kumbe! Wale Waebrania watoka katika mashimo walimojificha!
12 Nao watu wa ngomeni wakamjibu Yonathani na mchukua silaha zake, wakasema, Haya! Ninyi, pandeni juu hapa tulipo, na sisi tutawaonyesha jambo. Yonathani akamwambia yule aliyezichukua silaha, Haya! Panda nyuma yangu; kwa kuwa Bwana amewatia mikononi mwa Israeli.
13 Basi Yonathani akapanda kwa mikono na miguu yake, na mchukua silaha nyuma yake; na hao watu wakaanguka mbele ya Yonathani; na huyo mchukua silaha zake akawaua nyuma yake.

Ngome inajengwa ndani ya mtu kuhakikisha inasambaratisha ndoa inapiga mpaka ndoto zote zinapotea,jini linawekwa ndani ya mtu kuhakikisha huolewi. Ngome huwa iko ndani ,yenyewe inashambulia ndani kwa ndani usiweze kufanikiwa kwa mda unaotakiwa.Wengine unajengewa ngome ya umasikini ukianza biashara unaishia kula mtaji,ukianza kazi unafukuzwa ,jini linawekwa ndani linaambiwa hakikisha huyu hafanikiwi abaki kuwa masikini
2Wakorinto 10:3-4
3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
Wengine wanajengewa ngome ya magonjwa ili wawe wagonjwa miaka yote,walinzi wa ngome ni mashetani wadogo wadogo,wanapewa kazi ya kukulinda hawakuruhusu kabisa ufanye jambo lolote,wanakulinda usiweze kutoka na kuhakikisha lile tatizo ulilo nalo haliondoki. Kazi nyingine ya walinzi wa ngome ni kukukatisha tamaa,kukuletea hofu na mashaka,kuvuvia magonjwa ndani yako,kukuletea ndoto mbaya,kukuletea uzito unashindwa hata kusoma neno la Mungu,unashindwa kuomba,anahakikisha mambo ya Mungu unashindwa kuyafanya ,na hizi ngome zinapewa kafara ili kuendelea kuharibu maisha yako,na walinzi hawa hawaondoki bila kuipiga ngome,huwezi kufanikiwa,huwezi kumiliki mpaka utakapoibomoa ngome.

Comments