WANATUMIA MALI ZA KUIBA

Na Askofu Dr Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima.

Daniel 1: 1-21
“Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, Nebukadreza mfalme wa Babeli,alikwenda Yerusalemu akauhusuru. Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake. Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao. Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme. Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria. Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danielii, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego. Lakini Danielii aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. Basi Mungu alimjalia Danielii kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi. Mkuu wa matowashi akamwambia Danielii, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme. Ndipo Danielii akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria, Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe. Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona. Basi akawasikiliza katika jambo hilo, akawajaribu siku kumi. Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme. Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu. Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto. Hata mwisho wa siku zile alizoziagiza mfalme za kuwaingiza, mkuu wa matowashi akawaingiza mbele ya mfalme Nebukadreza. Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme. Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake. Tena, Danielii huyo akadumu huko hata mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi.”

Wana wa Israeli walivamiwa na Taifa linaloitwa Babeli likachukua vyombo vya Mungu wa Israeli likavipeleka kwenye nyumba ya mungu wa babeli vikaanza kutumika , Mfalme wao akaona haitoshi akaamua awachukue na vijana wenye akili na wanaokula vizuri na uzao wa kiungwana na vijana wasio na mawaa na wazui wa uso na wenye vipaji na ubunifu. Mfalme akaagiza watafutwe na wazuri wa uso (shetani anatafuta wazuri na vizuri ili avitumie) halafu werevu kwasababu ya maarifa na wenye kufahamu elimu watakaoweza kusimama ya mambo ya kifalme.
Tunaona Chombo ambacho kilikuwa kinatumika kwenye meza ya Bwana kimechukuliwa na kwenda kutumika kwa shetani. Mfalme wa babeli aliwachukua watu hao akaamua kuwabadilisha majina ili awatumie kwa makusudi yake. ‘Vyombo vya Bwana ambavyo vilikuwa vinatumika kuujenga ufalme wa Mungu vilikubali kutumika kwa shetani na kujenga ufalme wake’, watu walewale ambao walikuwa wanatakiwa watumike kwaajili ya Bwana walikubali kutumika kwaajili ya shetani na kubadilishwa majina yao (shetani anatabia ya kuchukua vitu vya Bwana Mungu na kuvibadilisha majina na kuvitumia kuujenga utawala wake) unaweza kuwaona wanamuziki wanaimba vizuri sana nyimbo za kidunia na ukajiuliza hawa kwa sauti zao hizi wangekuwa wanaimba kwaajili ya Mungu wangeimba nyimbo tofauti na nzuri sana. Fahamu kwamba wakina danieli walikubali kubebwa vilevile na ufahamu wao na werevu uleule na maarifa yaleyale kwaajili ya mapenzi ya kishetani na napoyaona mabaa haya na watu wenye akili wanafanya mambo ya ajabu fahamu kwamba wanatumika kwaajili ya mapenzi ya kishetani hivyo wameibiwa na vipawa vyao ndivyo vinavyotumika.
Nchi ya Israeli ilivamiwa na vijana wake wakaibiwa na ule uwezo wao wa kubuni vitu ili ukatumike kumjengea adui na himaya yake, zile akili zao zilichukuliwa zikamjenge adui, ule ubunifu wao na uzuri wao ulichukuliwa ukamjenge adui kwaajili ambaye ni babeli.
Kazi ambazo vijana hawa walikuwa wanafanya kwenye ufalme wa babeli ilikuwa kutumika kutafsiri ndoto, danieli alichukuliwa kupanua ufalme wa giza kwa kutumia vipawa vyake, (Mungu akikupa kipawa amekupa wala hana majuto, hatakama ukikitumia vibaya hakunyanganyi. Mungu akikupa zawadi sio kama mwanadamu hakunyanganyi hata ukikitumia vibaya) hiyo hekima aliyowapa wakina Danieli aliwaona na wakichukuliwa nayo wakaenda kuitumia kwaajiliya Ufalme wa adui. Chochote cha kidunia unacho kiona iwe ni taifa au mipango vimejengwa kwa akili hizihizi tulizo nazo. Danieli alitumika kwa uwaziri mkuu akiwa bado anatumika na vipawa vyake, aliibiwa kutoka kwenye taifa la Mungu akaenda kutumika kujenga kwa adui, unaweza kuwaona watu wanaringa na kukemea watu na kuendesha magari na kujisifia na kutamba kila mahali kumbe wametumia za watu kwa kuiba vipawa vyao na kuvitumia kujinufaisha wenyewe.

Sasa hivi kuna mtu anatengeneza uwaziri mkuu mahali kwa kutumia akili na vipawa vya watu, kuna mtu anatengeneza kampuni mahali kwa kutumia ufahamu wa mtu na hii inathibitisha kwamba watu waemibiwa na kutekwa na kufanywa mawindo na watarudishwa kwa jina la Yesu.
Wakina Danieli alitumika kuwa wakuu wa wilaya ya Babeli japo walitakiwa watumike kwaajili ya Israeli. Mungu anapokupa akili, hekima, maarifa anakupa ujenge ndani ya Ufalme wake. Na ukiibiwa vipawa hivyo na wewe pia fahamu kwamba vinakwenda kutumika kujenga sehemu ilipokusudiwa amapo ni kwa aduni shetani. Danieli alikuzwa akawa mkuu wa waganga wa kienyeji na wachawi kwasababu ya kipawa chake cha kutafsiri ndoto za Mfalme, Danilei alitafsiri ndoto tena na tena moja wapo ikiwa ni ile ya “MENEMENE TEKELI NA PERESI” lakini alikuwa bado yuko kwenye himaya adui anatumia kipawa chake huku akipandishwa vyeo mbalimbali. Unaweza ukawa unapandishwa cheo lakini unatumika na vipawa vyako kufaidisha wengine.
Wakati hawa wana wa Israeli wanaibiwa mfalme alikuwa Nebkadreza na akafa akaja Mfalme mwingine aliyeitwa Belheshaza na akafariki akaja mwingine anaitwa Dario naye akawatumia wale vijana na vipawa vyao akafa ndipo alipokujaa mfalme mwingine anaitwa koreshi na alipokuwa anamalizia utawala wake akawaruhusu wale vijana walioibiwa waende nyumbani kwao wakajenge nchi yao.
Zamani nchi ikivamiwa wavamizi wanaharibu nchi yenu na kukata miti na kila kitu ambacho kinaisaidia nchi kustawi na kuwachukua watu wenye vipawa na kuondoka nao, unaweza kujiuliza kwanini kwenye mataifa ya Marekani, na Ulaya kuna watu weusi ni kwasababu kuna wakati walihitaji watu wa kufanya kazi fulani na wakaona watu hao wanapatikana Afrika na wakaja kuwachukua, baadaye walipokuja kuanzisha biashara ya viwanda na kutosheka wakaanza kuacha biashara ya utumwa. Sasahivi baada ya biashara ya kuuza madawa ya kulevya biashara ya pili ni kuuzwa kwa watu kwa maana ya kufanya kazi za ndani na nyinginezo, watu hudanganywa kwa kulipwa vizuri lakini baada ya kufika kule hukutana na vitu tofauti na kuchukiliwa paspoti zao na kupelekwa kufanya kazi za ajabu na kuzeekea hukohuko sababu hushindwa kurudi nyumbani na hii biashara inafanyika mwilini lakini rohoni napo ni vilevile.
Rohoni inakuwaje?
Rohoni mtu anapotea ama anaondoka ama anauzwa ama anajiuza, mtu unaweza kusema unaumwa au unabalaa lakini sio hivyo umeibiwa mikono yako au uso wako wa upendeleo, au miguu yako ya Baraka au kinywa chako cha ushawishi na kinatumika mahali fulani kunufaisha watu fulani. Tabia moja wapo za kichawi ni kuuza na kunua watu.

“Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.” 2 Wafalme 17:17
Walianza kuwatoa watoto wao kwa kuwachoma kwenye moto kama sadaka na kuuza nafsi zao, mojawapo kati ya tabia za kichawi ni kuwauza watu au kujiuza au kuwatoa watu kafara.
“Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani.” Zaburi 106:37

Inamaana kuna meza ambayo watu wanaweka sadaka za kishetani.
“Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.” 1 wakorintho 10: 20
Sio kila anayetoa anatoa kwa Mungu lakini wengine wanatoa kwa mashetani sababu kuna meza ya Bwana na Meza ya Mashetani.
“Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake; wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja. Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.” Ufunuo 18: 9 – 13

Hapo ineonekana roho na miili ya wanadamuinauzwa na wafanya biashara, Leo kuna watu wagonjwa, wanabalaa, wameibiwa, wamefeli kwenye maisha lakini wao wanawaza ni mambo ya kawaida ya kibinadamu kumbe sio kweli wameibiwa. Kila mtu anacho kitu kinachomfanya afanikiwe kwenye maisha na hicho ndicho kinachomfanya mtu huyo astawi.
Wachawi ni binadamu wenye uwezo wa kusoma alama za rohoni. Mchawi akimwangalia mtu aliyepewa kipawa na Mungu cha akili ya kujenga viwanda anafahamu kabisa.
Kwenye ulimwengu wa rohoni wachawi waweza kuangalia akili ya mtu na wanachukua akili yake na kuanza kuitumia. Shetani na wachawi hawana cha kwao lakini wanaweza kubaini mtu aliyezaliwa ana kipawa gani, wanachukua ule ubunifu wake kwenye ulimwengu wa rohoni na kwenda kutengeneza mahali, tumbo lako wachawi wakiliangalia wanaona linaweza kuzaa raisi na watawala na wanalichukua mahali kwenda kuzalisha, wanachukua macho, masikio, akili, wanachukua kinywa cha mtu mwenye mamlaka ya kukemea na kwenda kukitumia mahali. Mtu huyo ambaye ufahamu wake umechukuliwa au ubunifu wake umechukuliwa au akili zake zimechukuliwa au kinywa chake, tumbo lake limechukuliwa anaanza kuwa mgonjwa ili kusudi waendelee kuvitumia vipawa vyake na visirudi kwake tena.
Mfalme wa babeli ambaye ni shetani unakuta amechukua vipawa hivyo na kuvitumia kutengeza utawala wake, unakuta mtu aliyechukuliwa vitu hivyo anaanza kupatwa magonjwa, balaa, matatizo, sababu vipawa vyake havipo na wamemwekea mashetani ya magonjwa na kujikataa. Watanzania wengi wana vipawa na akili sana lakini wameibiwa. Hao waganga wa kienyeji ni watumishi wa Mungu kwa asili lakini wameibiwa wanatumika kuuendeleza utawala wa giza.

Elimu ni tochi ya kuyatafuta maisha, elimu inatakiwa kuendeleza kipawa ulichopewa na Mungu. Mungu amekupa wewe vipawa ambavyo ndivyo inavyokupa mafanikio, inawezekana ufahamu wako umebuni vitu mahali lakini yule mtu aliyekuibia anafaidika na wewe umebakia na magonjwa.
“Kwajina la Yesu watu wanaotumia mali za kuiba wamejenga makampuni kwa akili ya kuiba, wamejenga mabenki kwa aklili za kuiba ninaamuru kuanzia sasa mali zote zilizojengwa kwa akili yangu na ufahamu wangu njoo kwa jina la Yesu njooo kwa jina la Yesu”
Shadrak meshak na Abednego walitumika na vipawa vyao kujenga babeli na babeli ikawa kubwa kuliko mataifa yote duniani na wewe pale ulipo yawezekana umeibiwa vipawa vyako ndiomaana una magonjwa, mikosi, balaa na hali uliyo nayo hivyo sasa unatakiwa uvirudishe njoo kwa jina Yesu
Walipandishwa vyeo na kuwa mawaziri na wakuu lakini walikuwa wanatumika na wafalme, akili zao na maarifa yao na ubunifu wao zilikuwa zinatumika lakini wakati wa utawala wa tano Mungu akaamua kuwarudisha wakajenge utawala wa kwao na wewe unatakiwa urudishe kwa jina la Yesu wakati wa utawala wa Tano lazima akili za watanzania na vipawa vyao vilivotumika wakiwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi, mawaziri ziachiliwe kwa jina la Yesu.
Kile kilichojengwa unakiona wewe kwa macho yako akili ya mtu imekijenga, wewe unajiona ni maskini lakini wewe sio masikini bali vile vipawa vyako ndugu yako au mtu fulani anavitumia kutajirika mahali fulani huku wewe ukiwa maskini.Hakuna mtu maskini kwenye dunia hii bali watu wameibiwa na kutekwa.
“Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” 2Wakorinth 8:9
“Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu” Mwanzo 13:2
Ibrahimu hakuwa maskini bali alikuwa tajiri na Mungu wa Ibrahimu ndiye Mungu wetu tunaye mwabudu.
“Nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.” Isaya45:3
Fursa zinatokana na Ustawi wetu na vipwa wetu, Biblia inasema nitakurudishia hazina na mali za gizani zilizoibiwa. Nitakurudishia miaka yako iliyoliwa na nzige, inamaana ipo miaka iliyoibiwa, miaka ya kuteseka sababu vipawa havipo na kuhangaika iliyoibiwa na shetani, Mungu anakurudishia sasahivi kwa jina la Yesu.
“Nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli. Luka 10: 9
Mtu yeyote aliye mpokea Yesu amepewa mamlaka na amri ya kuangamiza nguvu zote za shetani na waganga wa kienyeji na wasoma nyota na wachawi wote hawa hawana nguvu juu ya mtu aliye na Yesu na ndani yake wala hawawezi kumloga akalogeka kwahiyo wewe uliyeokoka unazo nguvu za Mungu za ajabu na unauwezo wa kurudisha vyote vilivyoibiwa kwa jina la Yesu.
“Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu” Marko 6:7

Una amri juu ya mamlaka ya kurudisha vyote viliyoibiwa kutoka kwako kwa jina la Yesu anza kurudisha sasa kwa mamlaka ya Jina la Yesu.

Comments