ZIJUE SIRI ZA UFALME WA GIZA(4)

Na Mwl Nickson Mabena

Mungu ni mwema bado, tunaendelea na Somo letu, tupo kipengele cha Sita Kati ya vipengele nane, Ukitaka kujua Wapi tunaelekea basi tafuta Sehemu ya Kwanza ya Somo hili, ambapo niliweka utangulizi, na huo utangulizi wa Somo ndio Umekua Mwongozo wangu katika kuandika Somo hili!.
6.SADAKA ZITOLEWAZO KATIKA UFALME WA GIZA!.
Kwenye kipengele cha tano tuliangalia Vitu vinavyotumika kwenye ufalme wa Giza, na vitu hivyo wakati mwingine hutolewa Kama Sadaka..
Kwenye kipengele hiki cha Sita tunaziangalia baadhi ya sadaka zitolewazo kwenye Ufalme wa Giza, na tayari tumeshaziona Aina mbili ya Sadaka hizo, ambazo no:-
a)DAMU
b)VYAKULA NA POMBE
na Leo nakuletea sadaka nyingine, ambayo ni ya Tatu..
c) VIUNGO VYA WANYAMA/WATU
Kwenye Somo hili, hii itakua aina ya mwisho ya Sadaka.
Kwenye Ufalme wa Giza, viungo vya Wanyama au Watu vinaweza kutumika Kama sadaka..
Tuanze kwa kuyaangalia Maandiko kwanza.
Ezekieli 21:21
"Maana mfalme wa Babeli alisimama penye njia panda, penye kichwa cha njia hizo mbili, ili atumie uganga; aliitikisa mishale huku na huko, akaziuliza terafi, akayatazama maini."
Mfalme alipoenda kufanya Uganga, alienda na Maini, na Uganga wake alienda kufanyia njia panda, maana uchawi hufanyika Sana njia panda, Juu ya vilima, Chini ya miti.. Mara nyingi ndipo Madhabahu za Ufalme wa Giza huwekwa!!.
Ona, "Hutoa dhabihu juu ya vilele vya milima, na kufukiza Uvumba juu ya vilima, chino ya mialoni na milibua na miela, kwa kuwa uvuli wake ni mwema; kwa sababu hiyo binti zenu huzini na Bibi arusi zenu hufanya uasherati." HOSEA 4:13
Umeyaona hayo Maneno!?.
Viungo vya Wanyama vinaweza vikawa sadaka, huyo Mfalme wa Babeli alienda na Maini Kama sadaka. Sasa inategemea mungu wa hiyo madhabahu anataka kiungo gani!.
Ndio hapo utasikia Viungo vya Albino vikitafutwa Sana, hii ni kwa Sababu watu huenda kutafuta Msaada kwa waganga wa kienyeji, na waganga kuwaambia watu hao wakalete Kiungo cha Mnyama au Binadamu!.
Na kwa sababu watu wanataka msaada bila ya kujali utu, ndipo hutumia Gharama zozote ili apate kiungo cha Albino!!.
Hizo ndio aina sadaka zinazotolewa kwenye Ufalme wa Giza!.
Kumbuka Unapotaka Msaada kwenye Ufalme wa Giza, lazima udaiwe Sadaka, na Aina Ya Sadaka utakayodaiwa inategemea na Msaada unaouhitaji!!.

7.SABABU ZA WATU KUTAKA MSAADA KWENYE UFALME WA GIZA!.
Kwenye kipengele hiki nitatoa Sababu kadhaa, za kwa nini watu huenda Kutafuta Msaada kwenye Ufalme wa Giza, wakati Ufalme wa Nuru upo, pia kwa nini watu wengi hukimbilia huko wakati Mungu yupo, na Anawapenda watu wake, na Bado anaweza, tena kuliko Hata Shetani!!.
Pamoja na Kwamba, Watu wanajua kua si sahihi kwenda kwa Waganga, Au Mizimu kutaka misaada, Je! Kwanini bado watu wanaenda!??.
Zifuatazo ni Baadhi ya Sababu za watu kwenda kutaka Msaada kwenye Ufalme,wa Giza!.
i) KUKOSA UVUMILIVU!.
Watu wengi sana tuna mahitaji Mengi sana, tuna Shida nyingi sana, tena tungetamani shida zetu zingetatuliwa tangu Mwaka jana,
Sasa inapofika wakati Watu wakasubiri Msaada toka kwa Mungu, bila Mafanikio yoyote, ndipo Uvumilivu unawashinda, na Uvumilivu ukitoweka, Maamuzi yoyote Mtu anaweza kuyafanya..
Biblia inasema hivi,
"Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa Uzima".
Mithali 13:12
Moyo wa mtu unaugua, unakosa kusubiri, unakosa uvumilivu, endapo kuna kitu umekitarajia kukipata, na kikakawia Kuja!.
Mfano, Mtu anataka Aolewe, anaona miaka inaenda tu, wala haolewi, unajua kitakachofuata!??, Biblia inasema Moyo Huugua!!.
Au Mtu amesubiri kwa Mungu kupata Mtoto, na kwa Muda mrefu hajapata, Mtu huamua kwenda kwa Waganga kwenda kutaka Msaada...
Ndio maana wengi hukimbilia huko, kwa kukosa Uvumilivu huku!!.

Naomba niishie hapo,
Mungu akubariki Sana,
.....Somo litaendelea...

By Mwalm Nick
0712265856 WhatsApp#

Comments