APONA UKIMWI BAADA YA MAOMBEZI EFATHA.

Octavie Damas Akishuhudia kanisani jinsi alivyopona Ukimwi.

Naitwa Octavie Damas Kambadu napenda kumshukuru Mungu kwa maajabu yake, ni miaka mitano sasa imepita katika miaka minne amenitendea mambo makubwa sana, nilikuwa ni muathilika wa (H.I.V) ila sasa ni mzima namshukuru sana Mungu. Mara kwa mara nilikuwa ninamuona Mtume na Nabii Josephat Mwingira ananifuata kwenye ndoto kabla sijaokoka, siku moja kwenye ndoto akaniambia unataka nini? Nikamwambia, nataka nikae Efatha wakati huo nakaa Makongo Dar es salaam, Akaniambia anayestahili kuongea na wewe ni Mama Eliakunda. Baada ya kuamka nikawa naenda Kanisani ila baba yangu mzazi alikuwa ananipinga. 

Siku nyingine nikaota ndoto Mtume na Nabii Mwingira naongea nae, na mimi nikamuuliza unataka kunisaidia baba yangu? Maana baba yangu mzazi alikuwa Padri na mama yangu alikuwa ni sister wa Kanisa la Katoliki miaka kumi na saba walitumika huko, hivyo walinipata katika hali ya uovu Mtumishi akaniambia usijali. Baada ya hapo nilikuja kupata mtoto na sasa ana umri wa miaka mitano, nikaja kuambiwa kuwa nimeathirika na nina virusi vya Ukimwi, sikuamini.

Nikaenda kupima ila nilikuwa nina Amani na kuamini Uponyaji. Ilifika wakati wa kwenda Kusanyiko Kuu Kibaha Precious Center niliamua kufunga siku saba baada ya kusanyiko la mwaka jana nilienda kupima nikakuta nimepona sina tena Virusi vya ukimwi {H.I.V} nampenda sana Mungu wangu.

Nampenda sana Mungu na ninampenda sana mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Mwingira, sio kwamba nina danganya, Yesu wa Efatha anaponya na sasa nimepona sina ugonjwa.
Shukrani zangu kwa Mungu nimeamua kumtolea Mungu eneo la kuanzisha Kanisa {Kiwanja} Dodoma nitakwenda kuanzisha Kanisa la Efatha Wilaya ya Kondoa.

Hakuamini alivyopimwa na kukuta amepona Ukimwi.
Octavie Damas Akishuhudia kanisani jinsi alivyopona Ukimwi baada ya maombezi.

Comments