CHEMSHA BONGO KWA VIJANA WAKRISTO.

Na Mtumishi Peter M Mabula.
BWANA YESU asifiwe.
Siku moja nilipewa jukumu la kuwapima vijana kama wanaisoma Biblia kwa utafiti. Ilikuwa ni kwenye mkesha wa jimbo.
Niliandaa maswali haya ili nijue ni nani husoma Biblia na nani hasomi.
Vijana kwenye mkesha huo wa vijana walifaulu vizuri.
Jipime na wewe leo au uongeze ufahamu wako
Karibu.


      1.    Kuna aina ngapi za manabii ambazo Biblia inataja?

Jibu. 

Manabii WA kweli na manabii WA uongo. 
Kuna ndugu wamejibu kwamba manabii wakubwa na manabii wadogo hilo sio jibu maana hakuna popote kwenye Biblia palipoandikwa nabii mkubwa au nabii Mdogo.
Kuna manabii tunawaita manabii wakubwa ni kwa sababu tu vitabu vyao vina maandishi mengi na hao ni 4 na kuna manabii tunawaita wadogo kwa sababu tu ya maandiko yao kuwa machache ukilinganisha na WA kwanza lakini hiyo ni kanuni ya nje ya Biblia na sio ndani ya Biblia yenyewe. Manabii hao wadogo ni 12. Kanuni hiyo ni nzuri ili tu kutusaidia kuelewa kwa urahisi zaidi



       2.   Kitabu cha maombolezo kaandika nani?

Jibu ni Nabii Yeremia


     3.   Katikati ya Biblia ni kitabu gani na unaweza kunipa andiko LA katikati ya Biblia? 

Jibu.
Kuna sura au milango 594 kabla ya Zaburi 118
na kuna sura au milango 594 baada ya Zaburi
118. na ukijumlisha hizo sura 594 + 594 unapata
sura 1188 na ukiongeza na hiyo sura ya katikati
ya BIBLIA unapata sura au milango 1189..
Hivyo BIBLIA ina sura au milango
1189.
Sura ya katikati ya BIBLIA ni
Zaburi 118.
Mstari wa katikati ya BIBLIA ni
Zaburi 118:8 unasema ''Ni heri kumkimbilia
BWANA Kuliko kuwatumainia wanadamu. ''
kwa kuongeza ufahamu jifunze haya.
Sura/mlango/chapter fupi
kabisa katika BIBLIA ni Zaburi 117
inayosema ''Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni
BWANA, Enyi watu wote, mhimidini. Maana
fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na uaminifu wa
BWANA ni wa milele''.
Sura ndefu zaidi katika BIBLIA
ni Zaburi 119 ambayo sura hii au mlango
huu una mistari 176.

BIBLIA ina mistari au aya
31,102 kutoka MWANZO hadi
UFUNUO
Mstari wa kwanza kwenye
BIBLIA unasema ''Hapo mwanzo
MUNGU aliziumba mbingu na
nchi'' mwanzo1:1 na mstari wa
mwisho kwenye BIBLIA unasema
'''Neema ya BWANA YESU na iwe
pamoja nanyi nyote.Amina.''
ufunuo 22:21
BIBLIA ina vitabu 66 ambavyo
ni 39 Agano la kale na 27 Agano
jipya. na Sura ya katikati ya BIBLIA ni Zaburi
118.




     4.   Rebeka mke WA Isaka na Naomi mama Mkwe WA Ruthu ni nani kati yao aliyewahi kuishi duniani?

Jibu. Ni Rebeka
Iko hivi ibrahim alimzaa isaka na isaka akaja akamuoa Rebeka baadae Rebeka akamzaa Yakobo baadae wana wa Yakobo wakaenda kuishi Misri miaka 430 hapo bado Naomi hajazaliwa. Baada ya waisraeli kutoka misri Yoshua akawaongoza miaka mingi baadae wakaanza kutawala waamuzi zaidi ya 10 ndipo katika mwisho WA kutawala waamuzi ndipo Naomi anatokea hivyo iko tofauti ya miaka zaidi ya 600 katiya kuishi kwa Rebeka na Kuishi kwa Naomi Duniani.



      5.   KRISTO maana yake nini?

Jibu:
Neno KRISTO linatokana na neno Messiah la
Kiebrania.
Kwa Kiarabu ni Masih.
Shina la neno ni m-a-s-a-h-a, maana yake ni kupaka mafuta ya kipekee.
Zamani Makuhani na wafalme walipakwa
mafuta kabla ya kusimikwa katika
nyadhifa zao. Lakini kwa tafsiri ya
Kigiriki, neno hili linaonekana kuwa mahususi,
kwa ajili BWANA YESU tu.
MASSIAH la Kiebrania, kwa Kiingereza, maana
yake ni Anointed (aliyepakwa, aliyetiwa mafuta).
Christos maana yake ni ALIYETIWA
(ALIYEPAKWA) MAFUTA, au mpakwa mafuta maana yake ya MTEULE
(ALIYETEULIWA).



    6.    Pentecoste maana yake nini?
Jibu.
Pentecoste ni Siku ya 50 baada ya pasaka ya kiyahudi. pentecoste ni Siku ya ROHO MTAKATIFU alipowashukia mitume Mara baada ya BWANA YESU kwenda mbinguni.



    7.   BWANA YESU alipokuwa anapaa kwenda mbinguni alipaa mbele ya watu wangapi waliokuwepo muda ule pale mlimani?

Jibu. 

Ni mitume 11 ilo Marko 16:14-20.

8. Taja majina 7 ya makanisa 7 yaliyotajwa katika kitabu cha ufunuo?

Jibu. 

Ni Efeso,Smirna, Pergamo, Thiatira,Sardi, Filadefia na Laodokia.
Siku nyingine nitafafanua maana ya makanisa haya ya kuinabii.


     9.  Taja majina ya malaika 2 ambao Biblia inawataja kwa majina.
jibu ni 

Ni Mikaeli ( Yuda 1:9)
Na Gabrieli ( Luka 1:19)



    10.   Ni mtumishi gani aliambiwa "Lakini zikimbie tamaa za ujanani, Ukafuate haki, na imani, na Upendo na amani pamoja na wale wamfuatao BWANA kwa moyo safi?


Jibu. 

Ni Timotheo na iko 2 Timotheo 2:22.

MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
mabula@gmail.com.
0714252292

Comments

Unknown said…
Ubarikiwe mnooo na huyu Mungu wa mbinguni