CHEMSHA BONGO.



BWANA YESU asifiwe.
Siku moja nilipewa jukumu la kuwapima vijana kama wanaisoma Biblia kwa utafiti. Ilikuwa ni kwenye mkesha wa jimbo.
Niliandaa maswali haya ili nijue ni nani husoma Biblia na nani hasomi.
Vijana kwenye mkesha huo wa vijana walifaulu vizuri.
Jipime na wewe leo au uongeze ufahamu wako
Karibu.

📖
: Swali La kwanza:

Kuna aina ngapi za manabii ambazo Biblia inataja?
📖
: Swali la Pili.

Kitabu cha maombolezo kaandika nani?
📖
: Swali la tatu:

Katikati ya Biblia ni kitabu gani na unaweza kunipa andiko la katikati ya Biblia?
📖
: Swali LA NNE.

Rebeka mke wa Isaka na Naomi mama mkwe wa Ruthu ni nani kati yao aliyewahi kuishi duniani mapema kabla ya mwenzake?
📖
: Swali la tano:

Neno KRISTO maana yake nini?
📖
: Swali la sita:

Neno Pentecoste maana yake nini?
📖
: Swali la saba:

BWANA YESU alipokuwa anapaa kwenda mbinguni alipaa mbele ya watu wangapi waliokuwepo muda ule pale mlimani?
📖
: Swali la Nane:

Taja majina 7 ya makanisa 7 yaliyotajwa katika kitabu cha ufunuo?
📖
: Swali la Tisa:

Taja majina ya malaika 2 ambao Biblia inawataja kwa majina.
📖
: Swali la kumi:

Ni mtumishi gani aliambiwa "Lakini zikimbie tamaa za ujanani, Ukafuate haki, na imani, na Upendo na amani pamoja na wale wamfuatao BWANA kwa moyo safi?
Jipime na ubarikiwe sana.
Ni mimi ndugu yako Peter Mabula.
Mabula 1986@gmail.com
0714252292

Kama umefanya maswali haya basi hakikisha kwa majibu haya ambayo ni majibu ya maswali hayo hapo juu na nimejibu kama ifuatavyo, FUNGUA HAPA

Comments