EWE KONDOO UNATAFUTWA.

 
Na Mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU apewe sifa ndugu yangu.
Namshukuru MUNGU wa mbinguni kwa siku hii njema ambayo nakuletea ujumbe huu.
Isaya 53:6A ''Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; ''
Bila YESU hakika tumepotea.
Kama unamkataa YESU hakika wewe ni kondoo uliyepotea.
-Kondoo wengi wamepotea, hawalitaki zizi wala hawamhitaji mchungaji wao pekee.
Mchungaji wa Kondoo ni mmoja naye ni BWANA YESU.

Yohana 10:7,9 '' Basi YESU aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.  Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. '' 

-Kuna kondoo wengi leo wamelihama zizi.
Kondoo wale wamepotea kabisa, wamerudi duniani, na anasa za dunia ndizo zinawachunga sasa baada ya wao kumkataa Mchungaji pekee wa kuwapeleka uzima wa milele.
BWANA YESU anasema;

'' kama vile BABA anijuavyo, nami nimjuavyo BABA. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.-Yohana 10:16 '' 

Kuna kondoo BWANA YESU anawatafuta, anawahitaji katika ufalme wake wa milele. Ni kazi ya Wateule kwenda kuwatafuta kondoo hao waliopotea na kuwarudisha zizini. 
Watafuteni Kondoo Wa MUNGU Waliopotea. 
Kuna Kondoo Yuko Porini Gizani Amefungwa Kamba Ya Uzinzi, Chatu(shetani) Anamtafuta Kondoo Huyo Na Yuko Karibu Kummeza ili aukose uzima wa milele. 

Kuna Kondoo Mwingine Aliyepotea, Huyu Amefungwa Kamba Ya Kuipenda Dunia, Kuna Hatari Nyingi Zinamfuata, Msaidieni Huyo Enyi Watumishi Wa BWANA YESU. 

 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.-1 Kor 6:9'' 

Kuna Kondoo Wamefungwa Kamba Za Utapeli Na Wizi, Kuna Kondoo Wamefungwa Kwa Kamba Za Ukahaba Na Pombe, Kuna Kondoo Wamefungwa Kamba Za Kuabudu Sanamu, Hawa Wote Ni Kondoo Na Tunatakiwa Tuwasaidie.
 Chatu Kuzimu Anakaribia Kuwakamata Kondoo Hawa Waliomtoroka Mchungaji Mwema YESU KRISTO. 
Waambieni Kondoo Hawa Warudi Kwa Mchungaji Mwema. Kuna Kondoo Waliopotea Na Wamefungwa Na Kamba Za Kuabudu Shetani, Kuna Kondoo Waliopotea Sasa Wamefungwa Kwa Kamba Uasherati. Wasaidieni Kondoo Hawa Waliopotea Ili Chatu Kuzimu Asiwameze. Wambieni Kondoo Hawa Warejee Zizini.
 Zizini Ni Kuokoka. 
Kurudi Zizini Ni Kurudi Kwenye Wokovu Wa BWANA YESU. Mchungaji YESU KRISTO Anawapenda Sana, Yuko Tayari Kuwapokea. 
Matendo  3:19 '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;''

 Kuna watu hujidangana wenyewe binafsi.
Unakuta mtu kila siku ni uzinzi tu harafu anasema "Naenda mbinguni"
Mbingu ipi?

Wewe ni kondoo aliyepotea na unatakiwa kugeuka na kutubu.
Tubu kwanza na kuokoka na kuanza kuishi maisha matakatifu ndipo utaanza kuhusika na mbingu.
Unakuta mtu kila siku wizi na uongo harafu nae anasema anaenda mbinguni.
Mbingu ipi?

Wewe ni kondoo aliyepotea na unatakiwa ugeuke na kutubu.
Tubu kwanza na kuokoka kisha anza kuishi maisha matatifu ndipo utaanza kuhusika na mbingu.
Wagalatia 5:19-21 ''Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.''
Wewe mchawi na msengenyaji unaesema unaenda mbinguni jichunguze na kujihoji unaenda mbingu ipi?
Kutubu na kuokoka na kuacha maovu ni Leo ndugu ndipo usema unaenda mbinguni.

Ewe kondoo unatafuta leo, geuka na kutubu na kuanza kuliishi neno la MUNGU.
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments