HAKIKISHA UNAKUWA MSAFI WA ROHO NA MWILI.

Na mtumishi Peter M Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
Kuna Ndugu Mmoja Nilimkemea Kuhusu Jambo Fulani Akanijibu "MUNGU Anaangalia Roho Na Sio Mwili". 
Nilicheka Sana Na Hakika Nikagundua Kuwa Shetani Anadanganya Watu Wengi Sana, Na Watu Hao Hudhani Kwamba MUNGU Hashughuliki Na Mwili Ila Roho Tu.
 Huo Ni Uongo Wa Shetani. 
Warumi 6:1-2 ''Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?  Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?   '' 
 
Ndugu Yangu, Kama Na Wewe Unamtazamo Huo Badilika Leo. 
shetani ni muongo na anawadanganya maelfu ya watu kwa kuwaambia kwamba MUNGU anaangalia roho tu.
Biblia inasema matendo ya mwili ndio mengi yanayowakosesha wanadamu hata wakakosa uzima.
Wagalaria 5:19-21 '' Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.'' 

-Kumbe kwa mujibu wa Biblia baadhi ya matendo ya mwili yanaweza kuwakosesha watu uzima wa milele.
MUNGU siku zote anataka tuwe watakatifu wa roho, mwili na nafsi.

-Kuna Watu Leo Huvaa Nusu Uchi Wakikemewa Wanasema MUNGU Haangalii Mwili Bali Roho Tu. 
-Kuna Watu Huenda Nusu Uchi Kanisani Wakijidanganya Kwamba MUNGU Haangalii Mwili. 
-Kuna Watu Hutembea Matiti Nje Na Hata Wao Wanasema MUNGU Haangalii Mwili. 
Ndugu Zangu, Hayo Ni Machukizo Na Ni Dhambi Kama Dhambi Zingine. 
-Ni fedheha kusema kwamba MUNGU anaandalia roho tu.

Ndugu Zangu, Matendo Ya Mwili Ndio Yanayoongoza Kuwapeleka Watu Jehanamu. Mfano Uzinzi Ni Tendo La Mwili, Wizi Na Kuvaa Kikahaba Ni Matendo Ya Mwili Na Vyote Ni Machukizo. 
Kama BWANA Asingekuwa Anaangaliwa Mwili Basi Asingekuwa Anatuponya Miili Yetu Tukiumwa. 
Tabia Ya Kumtaka YESU Aangalie Mwili Tukiwa Tunaumwa Tu Haifai.
 MUNGU Anaangalia Mwili Na Roho. 
HAKIKISHA UNAKUWA MSAFI WA ROHO NA MWILI.

Kila mwanadamu amegawanyika katika sehemu 3 yaani Mwili, Nafsi na Roho.
1 Thesalonike 5:23 '' MUNGU wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake BWANA wetu YESU KRISTO.''
Ninachotaka ujue ni kwamba ''Makuzi na malezi kwa kila mwamini yanatakiwa yafanyike katika sehemu zote 3.''


-Usikubali kutunza mwili vizuri huku roho yako ni chafu.
-Usikubali kuongozwa sana na nafsi wakati roho haitaki.
-Usiuchafue mwili wako huku ukijidanganya kwamba MUNGU anaangalia roho tu.
- Ikiharibika Nafsi ni rahisi sana mwili kuharibika maana vinategemeana.

inayotakiwa kusaidiwa sana ni nafsi.
Nafsi inatakiwa ipate maarifa sahihi yaliyo katika neno la MUNGU.

1 Kor 3:3 '' kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?''

Nikiambiwa nitaje sifa 2 tu za Mkristo mcha MUNGU nitataja hizi;

       1. Ni yule anayeishi maisha yanayoongozwa na Neno la MUNGU.
      2. Ni yule ambaye kipaombele chake cha kwanza ni kwa mambo ya MUNGU.

Ni muhimu sana ndugu yangu kuishi maisha safi ya wokovu. Kila dhambi na kila uovu unaonekana mbele za MUNGU. hakuna pa kujifisha ila ni kutubu na kuacha kufanya mabaya kwa kigezo cha kwamba MUNGU anaangalia roho tu wakati sio kweli.
1 Kor 6:9-11 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la BWANA YESU KRISTO, na katika ROHO  wa MUNGU wetu.''

 Kuna watu hudhani kwamba Huduma zao ndio tiketi ya kuingia Uzima Wa milele.
Huvaa vimini ibadani na kwenye huduma, na kugeuka mitego ya shetani kwa wengine lakini bado hujiona salama, wakati ukweli wanahitaji kumcha MUNGU upya.
Watu Hawa kufanya maovu mengi wakidhani Huduma zao ndizo zitawapeleka mbinguni.
Ndugu zangu naomba tutambue kwamba hata wahubiri wanaweza kwenda jehanamu kama wanafanya dhambi.
Hata askofu, Papa au mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu anaweza kwenda jehanamu kama haishi maisha matakatifu.
Uhusiano wetu binfsi na MUNGU ni muhimu zaidi kuliko Huduma zetu na vipawa vyema.

Ndio maana ninasema ni muhimu sana kuwa msafi wa roho na mwili pia.
 Dhambi ni uasi, hivyo dhambi yeyote haijalishi imetendwa na mwili, nafsi au roho bado inabaki ni dhambi na dhambi ni uasi.
1 Yohana 3:4 ''Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.''
-Kujiwekea utaratibu feki huki ukijidanganya kwamba MUNGU ni wa utaratibu huko ni kujidanganya.
-Kujiwekea utaratibu wa kila weekend kwenda disko wakati unajua kabisa kule disko anatukuzwa shetani na malaika zake ni kujidanganya mwenyewe.
Kusema kwamba MUNGU hayaoni matendo yako ya mwili huko ni kujiibia akili zako mwenyewe.
1 Yohana 2:6 ''Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake(YESU), imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.''
 Utakatifu wa mwili na roho ni muhimu sana kwa kila Mkristo.
Kuishi maisha matakatifu ndio mpango wa MUNGU kwetu wanadamu.

Dunia na mambo yake yote yatapita.
Dunia isikufanye utende dhambi bali ishinde dunia kwa kuishi maisha mataktifu.
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke.
Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo yangu ambayo sasa yanafika 400 mtandaoni.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

0714252292.
mabula1986@gmail.com
 

Comments