IMANI SAHIHI KATIKA MAOMBI YANAYOJIBIWA.

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU aliye hai.
Imani Ni Kuwa Na Uhakika Wa Kile Unachokitarajia.
Waebrania 11:1 ''Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.''

 Kwa Maneno Mengine Imani Ni Hati Miliki Ya Kitu Halisi.
Mfano Ukiwa Na Hati Miliki Ya Shamba Sio Lazima Ulione Shamba Kwa Macho Ndipo Usema "ni Mali Yangu".
 Unachohitaji Ni Kuwa Tu Ni Hati Miliki Halali Ya Kumiliki Shamba Hilo Tu. 
Imani ni muhimu sana, lakini pia kuna watu huitumia vibaya imani na kubaki hawajajibiwa maombi yao, japokuwa waliyaomba kwa imani.
Imani Sio Kubahatisha Wala Ubishi, Au Kung'ang'ania Mambo Kwa Jazba Na Kudhani Ni Imani. 
Huwezi Kukataliwa Na Mchumba Wako Na Wewe Ukaendelea kuomba  ukisema "kwa Imani Huyu Ni Wangu Tu Na Hatafika Popote Ila Atarudi Kwangu".
Ndugu Hiyo Wala Sio Imani Bali Jazba. 
Imani Sahihi Hupimwa Kwa Upendo, Adabu, Na Amani. 
Enenda Kwa Imani Si Jazba.

Waebrania 11:6 '' Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.'' 
-Imani sahihi ni kuamini MUNGU yupo na hujibu maombi hata yako. lakini pia huwezi kujiita una imani ya kupokea wakati humwitaji MUNGU na mpango wake.
Mpango wa MUNGU  kwako katika maisha yako ni Wokovu.
Wokovu ni mpango wa MUNGU kumtafuta mwanadamu. 
Tunza Kama Pesa WOKOVU wa BWANA YESU. 
Kumkataa YESU Ni Kukataa Uzima Wa Milele. 
Unaweza Ukadharau Lolote Kuhusu YESU Leo Lakini Haiwezekani Kuingia Uzima Wa Milele Bila BWANA YESU.
 Imani sahihi lazima iambatane na Wokovu. 
Maombi ya imani unatakiwa uyafanye ukiwa ndani ya wokovu.
Kuna aina nyingi za maombi lakini imani katika maombi hayo inahitajika sana kwa wewe uliyeokoka.

 Kuna Maombi Ya Kung'oa Milima Na Kuna Maombi Ya Kutikisa Tu Milima. Milima Ni Mahitaji Yako. 
Inategemea Imani Yako Katika Maombi Ya Kuong'oa Milima Au Una Imani Tu Ya Kutikisa Milima.
Mwombaji Lazima Aamini Kwamba Yote Yanawezekana Kwa MUNGU llakini mtu huyo lazima awe ndani ya Wokovu.
Luka 1:37 '' kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU.'' 

Jambo la kujua ni kwamba, Muombaji hatakiwi kumpangia  BWANA  Wala Kumwekea Mipaka. 
-Pia Kuna Matatizo Mengine Ili Kuyaondoa Lazima Ufunge Na Kuomba Lakini Wengi Hawajui Kuhusu Hili. 
-Pia Matatizo Mengine Yanaisha Baada Ya Kuomba Ukishirikiana Na Waombaji Wengine. 
-Na Kuna Matatizo Ili Yaondoke Lazima Kuwekewa Mkono Na Mchungaji Aliyeokoka. Mchungaji Anaweza Kupewa Password Ya Atm Yako, Atm Ni Mahitaji Yako Hivyo Akikuombea Utapata Nguvu Mpya Na Ushindi. 
Kwenye Maombi Kuna Hitaji Uongozi Wa ROHO MTAKATIFU Na Pia Lazima Uwe Na Maarifa, Mfano Una Jini Mahaba Harafu Unaomba MUNGU Akupe Mchumba, Ukiomba Peke Yako Utang'ang'ana Sana Maana Sharti Ufunguliwe Kwanza Wewe Ndipo Upokee Muujiza Wako, Ungemfuata Pastor Ungewekewa Mikono Na Jini Mahaba Angetoka Kwanza Kisha Ungeomba Na Kupokea.
 Mathayo 17:21 '' Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

 Mwili Ni Adui Wa Maombi, Mwili Ni Adui Wa Kufunga.
 Mambo Ya Mwili Humuondoa Mkristo Katika Kuomba. 
Watu Wengi Huona Kufunga Ni Jambo Gumu Kwa Sababu Tu Ya Kushindwa Kuuzuia Mwili. 
Matatizo Mengine Kwako Hayasababishwi Na shetani Wala Mapepo Bali Husababishwa Na Mwili. 
Mwili Umejaa Misukumo Mingi Ya Dhambi. 
Na Kama Mtu Hajaupeleka Mwili Wake Kikamilifu Pale Msalabani Na Kuusulubisha Mwili Huo Unaweza Kumtesa Sana Na Hata Kumkosesha Mbingu. Ndugu, Kumbuka Kwamba Mwili Huu Wa Sasa Hauwezi Kuurithi Ufalme Wa MUNGU, Huu Ni Mwili Wa Kufa Tu, BWANA YESU Atakapokuja Kulinyakua Kanisa Lake Mwili Huu Hautanyakuliwa Bali Utabadilishwa Na Kupokea Mwili Mpya Wa Kimbingu. 
Marko 11:24 ''Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. ''

 Ili kumiliki hatua zako kwa wakati inabidi
uamue mwenyewe kushindana katika
ulimwengu wa roho.

 Ndio maana kuna watu
wameokoka na wengine hawajaokoka ambao
waliwahi kutolewa unabii na kunenewa mambo
mengi na watumishi wa MUNGU lakini hadi leo
hayajatimia kwao; hii ni kwasababu ya
kutokuamua kupigana katika ulimwengu wa
roho. Na ndio maana Daniel alipogundua kuwa
siku za kukaa utumwani zimeisha aliamua
kuomba na kufunga ili kumiliki zile hatua
ambazo MUNGU amempangia.
Naamini Kuna kitu umejifunza sasa cha kukuvusha.


 Kufunga Sio Lazima Ila Kuna Vitu Huwezi Kufanikiwa Ila Kwa Kufunga Na Kuomba.
Hivyp maombi ya kufunga ni muhimu sana kwako.

Kuomba Ni Muhimu Sana Tena Ni Lazima Lakini Maombi Ya Imani Ndiyo Yanayoleta Majibu Sahihi.
Jambo la mwisho naomba utambue kwamba  ''Na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.-1 Yohana 3:22'' 

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke.
Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa
wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments