JINA BANDIA, UMRI BANDIA, ELIMU BANDIA, MAHUSIANO BADIA, KAZI BANDIA, CHEO BANDIA, SUBIRI MBINGU BANDIA.

Na Godfrey Miyonjo.

BWAN YESU asifiwe sana,
Wapendwa katika Kristo Yesu, ninatambua kuwa tulio wengi tunatamani kuingia ndani ya mji ule mtakatifu (Yerusalemu mpya).

Wengi tumejizuia katika mengi, tumejifunga mikanda na kusimama kiume, tukijitahidi kwa msaada wa BWANA tusimtende Mungu dhambi, ili siku ile ikifika tusikataliwe.
Ni jambo jema, tena lakubalika kwa Mungu.
Leo nina neno moja tu ningependa kuwakumbusha wapendwa; ninyi mlio na nia ya kumpendeza YEHOVA,
Ni ahadi ya Mungu kwa wote wampendao kuwa atawakaribisha kwake,
Ni kweli kuwa Mungu siyo mwanadamu hata aseme uongo,
Ahadi za Mungu zote ni amini na ni kweli,
Yaani kile alichokisema Mungu lazima akitimize, na atakitimiza pasipo upendeleo.
Imeandikwa:

“Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo, na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo” UFUNUO 21:27.
Ni kweli tumeahidiwa kuingi katika mji mpya, lakini ijulikane kuwa;
Mji ule siyo mji wa waovu, siyo mji wa waongo, siyo mji wa watu wa mataifa, ni mji wa watakatifu.

Ni mji kwa ajili ya wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha Mwana-Kondoo,
Siyo mji wa kuingia holela, bali ili uingie ndani yake, sharti kwanza uitwe jina lako.

Na kama ni mji ambao watu watakaoingia ndani yake ni wale waliothibitika katika kweli, itakuaje kwa waongo?
Je! Ni kweli wataingia mbinguni au watakwenda jehanamu?
Hapa pasipo kupepesa macho wala kumumunya maneno ni kwamba Wote walio na majina bandia (majina ya uongo) watakuwa wameandikwa ndani ya kitabu cha baba wa uongo,
Wanaosema kuwa wapo single wakati wameoa?wameolewa hao watakuwa wameandikwa katika kitabu cha baba wa uongo,
Wanaosema kuwa wanasoma?wamesoma UD, UDOM, MZUMBE, SUA, N.K ilihali hawakusoma huko, tena pengine hata darasa la saba hawakuhitimu, hao wanaisubiri JEHANAM,

Ninayasema haya kwasababu ni ukweli kuwa Baba wa uongo (shetani) yeye hana mbingu, yeye hajaandaa chochote, bali ameandaliwa moto,
Yeye shetani na wafuasi wake wote ipo siku watatupwa jehanam (mbingu bandia).
Na mimi nipo hapa ili kuhakikisha kuwa watu hawaendi jehanam,
Yaani kila mwenye mwili anatubu dhambi na kujisalimisha kwa YESU,
Kwa maana Imeandikwa
“Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima na mafundisho, na ufahamu” MITHALI 23:23.
Na ndiyo maana
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
PATANA NA MUNGU WAKO LEO, KABLA HAIJAJA SIKU ILE.
Ni mimi ndugu yenu katika Kristo.
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu)
WhatsApp 0757649495

Comments