JINA LA YESU LINAFUNUA UWEPO WA YESU MWENYEWE!.

Na Mwl Nickon Mabena

Bwana Yesu asifiwe, karibu tujifunze somo hili ambalo Roho Mtakatifu ameliweka ndani yangu ili nikushirikishe!.
"Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao." MATHAYO 18:19-20
Kuna Mambo huwa yananishangaza sana, lakini jambo hili hunishangaza zaidi, kwani kwenye akili za kawaida, haliingii kabisa, Jina la Mtu limuwakilishe Mtu Mwenyewe!!!,
Kwangu hii ni ajabu aisee,
Yesu anasema, wawili wetu watakapopatana duniani, katika jambo lolote watakaloliomba, Watafanyiwa na Baba wa Mbinguni. Kwa sababu, walipo wawili, watatu wamekusanyika kwa JINA LA YESU, NA YESU YUPO KATIKATI YAO!.
Naweza kusema kwa Lugha nyingine, Walipokusanyika Watu kwa Jina la Yesu, kuna Uwepo wa Yesu!!.
Yesu ni wa ajabu sana eti!.
Sijawahi kusikia sehemu, watu wakusanyike kwa jina la Raisi, alafu Raisi awe katikati yao, au watu wakusanyike kwa Jina la Nabii na huyo Nabiii awe katikati yao.
Sijawahi ona, watu wamakusanyika kwa Jina langu, alafu mimi niwe katikati yao!!, hao wote, watakua katikati yao, kama wakiwa Katikati yao, wasipokua katikati yao, Hata wakikisanyika kwa Majina yao, wao hawawezi kuwepo kati yao!.
Sasa, naelewa Zaidi kwa nini Yesu alisema tuombe kwa Jina lake;
YOHANA 14:
13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
Kwa kuwa Jina la Yesu linamfunua Yesu mwenyewe, ndio Maana Yesu anasema, tuombe kwa Jina lake, maana tunapoomba kwa Jina lake, yeye Mwenyewe tunamuingiza Kazini haraka sana!!.
Ona, Kwa Jina la Yesu, tunatoa Pepo.
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;" MARKO 16:17
Pepo unapolikemea kwa Jina la Yesu, wewe unaona umelitaja Jina la Yesu, lenyewe halioni jina la Yesu, bali linamuona Yesu Mwenyewe, ndio Maana linatoka!!.
Ujue, Kutaja Jina la Yesu sio rahisi kiivyo.
Mtu hata kama anaitwa Mkristo, ukikutana naye kwenye Gari la abiria, au kwenye kusanyiko la watu, ukimwambia BWANA YESU ASIFIWE, utakuta anapoteza Ujasiri wa Kuitikia Amen!. Anaweza akaitikia Salama, au akajifanya hajasikia.
Maana kulitaja Jina la Yesu linamfunua Yesu mwenyewe, Mwenye dhambi anahukumiwa Moyoni!!.
Mioyo usipokuhukumu, una ujasiri kwa Mungu.
"Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu". 1YOH 3:21

Tafuta Ujasiri wa Kulitaja Jina la Yesu, Litumie jina la Yesu, kuna matokeo Makubwa kwenye kulitumia Jina la Yesu!.
Petro na Yohana kwenye mlango wa hekalu uitwao mzuri, walipomkuta yule ombaomba walilitumia Jina la Yesu!.
MATENDO 3:
3 Mtu huyo aliwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.
4 Na Petro, akimkazia machi, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.
5 Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao.
6 Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilichonacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
7 Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zakena vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
8 Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na Kumsifu Mungu.

HALELUYAA...
LITAJI JINA LA YESU, MTAJE YESU, HATA KWENYE MAGUMU UNAYOPITIA, LITAJE JINA LA YESU, YESU MWENYEWE ATAINGILIA KATI KUKUSAIDIA...

Watu tunapokusanyika kwa Jina la Yesu, Yesu mwenyewe anakua katikati, akituhudumia, kwa maana hiyo Jina la Yesu, linamfunua Yesu Mwenyewe!!.
YESU AKUBARIKI SANA....
AHSANTE KWA KUNISIKILIZA!!.

By Mwalm Nick
0712265856 (WhatsApp#)

Comments