JINSI YA MKE KUMBADIRISHA MUME ILI AOKOKE NA KUMTUKUZA MUNGU.


Na Mtumishi Emmanuel Kamalamo.
Bwana Yesu asifiwe!
Namahukuru Mungu tena katika siku nyingine tena ya leo ambayo Bwana ametupa.
Utukufu na heshima narudisha kwake.
Karibu katika somo hili ambalo Roho Mtakatifu amenifundisha, naamini ukilifutalia na kuliweka kwenye matendo utaona matokeo yake kuwa ni mazuri.Roho Mtakatifu akufunulie kuona kile kilichoko katika somo hili.

Mwl.na Mwnj.Emmanuel
Redeemed Gospel Church
Kibaha-Pwani.
The.+255712-660766/+255759-103103/+255689-124215.
E-mail: ekamalamo@gmail. com

Somo letu linatoka kitabu cha 1 Petro 3:1-4,7. maandiko matakatifu yanasema,,,,"Kadharika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwako wasioamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile NENO; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.....Kadhariki enyi waume kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu na warithi pamoja wa neema ya UZIMA, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe"
Hakuna asiyejua NDOA ni mpango wa Mungu aliyouweka tangu mwanzo ili kupitia ndoa Mungu atukuzwe kwa majukumu aliyoyaandaa katika ndoa.
Na ndoa siyo tu kufarahia tendo la ndoa la asha! bali kuna kusudi maalumu liliko katika Ndoa.
Ndiyo maana mwanamke anaitwa "MSAIDIZI" kwa sababu amewekewa kitu maalumu cha kumsaidia Mwanaume katika Majukumu au Kusudi la Mungu lililondani yake; sitaki niingie huko sana ebu turudi katika somo.

Kuna baadhi ya watu wameingia kwenye NDOA wakiwa hawajaokoka kabisa;na wanakuwa wamefunga ndoa kanisani. Sasa ikitokea akokoka mmoja basi huyo ambaye ameokoka utafuta sababu ya kumuacha mke au mume kisa hajaokoka hawezi kukaa na giza. Ok! n kweli nuru na giza havichangamani, je ni sahihi kumuacha mke/mme wa ndoa.
Yesu anasemaje, Soma na mimi Mathayo 19:9 maandiko yanasema,,,"NAMI NAWAAMBIA NINYI; KILA MTU ATAKAYEMUACHA MKEWE, ISIPOKUWA NI KWA SABABU UASHERATI, AKAOA MWINGINE, AZINI; NAYE AMWOAYE ALIYEACHWA AZINI." Hapa tunaona Yesu anasema huwezi kumuacha mke kwa sababu "HAJAOKOKA, ANENI KWA LUGHA, ATOI FUNGU LA KUMI AENDI KANISANI KAMA WEWE". bali kasema kama ni "MWASHERATI". hapo waweza kumuacha.
Mathayo 5:32 anasema,,,"LAKINI MIMI NAWAAMBIA: KILA MTU AMWACHAYE MKEWE, USIPOKUWA KWA HABARI YA UASHERATI, AMFANYA KUWA MZINZU; NA MTU AKIMYOA YULE ALIYEACHWA, AZINI" Bwana Yesu asifiweee...!

Nataka niweke jambo hili wazi kabisa mbele lako kama "UMEFUNGA NDOA" na mlikuwa hamjaokoka na wewe ukaokoka usijaribu kumuacha mke wako au mume wako wewe ukiwa na "NURU YA KRISTO"
Ndoa inaweza kukufanya ukaona MBINGU au ukakosa MBINGU. Maana Petro anasema,,,"...WARITHI PAMOJA WA NEEMA YA UZIMA..." kama mke na mume ni warithi wa uzima wa milele; nataka ujue jambo hili akikoka mmoja ujue wapili naye ataokoka..Utaniuliza, nimejuaje? Sikia nikwambie, kama mke na mume ni "MWILI MMOJA" hajalishi mke au mume hajaokoka; lakini yule mmoja atamvuta yule asiyeokoka kitakacho muokoa wa pili ni ile "NEEMA YA UZIMA" ambayo imewekwa kwa mke na mume.
ILI MKE AMBADIRISHE MUME MAMBO YAFUATAYO NI MUHIMU AYAFANYE.
Jambo la Kwanza.
*MKE ONYESHA UTII.
Maandiko yanasema "UTII NI BORA KULIKO DHABIHU, NA KUSIKIA KULIKO MAFUTA YA BEBERU"(1 Samweli 15:22)
Kama mwanamke Umeokoka na Mume wako hajaokoka hakikisha unaachilia "UTII" kwa mumeo hata kama anakufanyia mabaya usijaribu kuweka kiburi cha kumuonyesha wewe ni bora kuliko wewe kwa sababu wewe umeoka.
Swala la UTII liabaki pale pale kwa mmeo, Paulo anasema,,,"NINYI WAKE, WATIINI WAUME ZENU, KAMA IMPENDEZAVYO KATAKA BWANA."(Wakolosai 3:18)
Dada au Mama unapoachila utii hata Mumeo anakutendea mabaya uwe na uhakika utii wako utazidi kumuhukumu siku kwa siku na siku moja Roho Mtakatifu atamtembelea na atauachilia UPENDO kwako kukupenda wewe na kumpebda Mungu wako. Utashangaa uchunguuliokuwa ndani yake unatoka na anapokea NGUVU ya upendo utokao kwa Mungu.Ndiposa anatimiza agizo la ,,,,"NINYI WAUME, WAPENDENI WAKE ZENU MSIWE NA UCHUNGU NAO" Bwana Yesu asifiwe...!

Jambo la pili.
*TENGENEZA MWENENDO WAKO ILI KUPITIA HUO AVUTeWE.
Kama utamuhubira Neno kila siku wakati mwenendo wako ni mbovu kwake na kwa Jamii inayokuzunguka usitaraje kumbadusha.
Maandiko yanasema,,,"...WAVUTWE KWA MWENENDO WA WAKE ZAO, PASIPO LILE NENO" maana yake mwenendo wako utamvuta mme wako mbali na kumuhubiria kwa neno kila siku.
Lakini mwendo wako ukiwa mzuri kwa mume wako nakwambia mapema yeye mwenyewe atakwambia "mke wangu nipeleke kanisani kwako". kwa nini aseme hivyo? kwa sababu tabia zako zimekuwa nzuri kwake hata Kama hakupi hela ya mboga bado unamuonyeshea UPENDO , hata kama anakunywa pombe bado akirudi unampikea unamvua viatu unamkumbatia na unamuita (I love you my sweet...mmmwaaa) hahahahaha...Nakwambia atashangaa mwenyewe hata kama amlewa atahamu unachomfanyia bwana.

Jambo la tatu.
*KUWA NA ROHO YA UPOLE.
Hapa panahitajika tunda Roho Mtakatifu la upole.Kama Mama au Dada hutakuwa mpole bali unakuwa mkali kwa mumeo ujue itakuwa vigumu kumbadirisha mmeo.
Mmeo awapo mkali wewe weka upole,maandiko yanasema,,,"......ROHO YA UPOLE NÀ UTULIVU, ILIYO YA THAMANI KUU MBELE ZA MUNGU"

Naamini kuna kitu umedaka cha kukusaidia ;jarubu kuweka kwenye matendo utàona mbadiriko.

MUNGU AWABARIKI

AMEN

Comments