KUHANI WA MADHABAHU


Na Mchungaji Adriano Makazi, Ufufuo na uzima.
1 Samweli 1:1-17
“Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa Bwana, walikuwako huko. Hata siku ile ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, kumpa mkewe Penina sehemu, akawapa na watoto wake wote, waume kwa wake, sehemu zao; lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu Bwana alikuwa amemfunga tumbo. Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula. Elkana mumewe akamwambia, Hana, unalilia nini? Kwani huli chakula? Kwa nini moyo wako una huzuni? Je! Mimi si bora kwako kuliko watoto kumi? Ndipo Hana akainuka, walipokwisha kula na kunywa huko Shilo. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake penye mwimo wa hekalu la Bwana. Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana. Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe. Ikawa, hapo alipodumu kuomba mbele za Bwana, Eli akamwangalia kinywa chake. Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa. Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako. Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana. Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa. Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.”

Elikana alikuwa ana wake wawili ambao ni Penina na Hana, Penina alikuwa ana watoto lakini Hana alikuwa hana watoto, wote walikuwa na desturi kwenda nyumbani mwa Bwana na kukutana na kuhani ili awaunganishe pamoja na Bwana awatimizie haja yao. Biblia inasema hana alikwenda madhabahuni mwa Bwana na akawa anaomba mbele za Bwana lakini maombi yake hayakujibiwa mpaka kuhani akamwambia atakuwa mlevi hata lini aache hayo yote anayoyaomba lakini hana aliumimina moyo wake mbele za Bwana ndipo kuhani akamwambia “Bwana na akupe haja ya moyo wako” na akafanikiwa kupata mtoto.
Kuhani ni mtumishi wa Madhabahu. Zamani kuhani ndiye aliyekua akipokea sadaka ya kuteketeza pale watu walipokuwa wanakwenda kuzitoa mbele ya madhabahu ya Bwana. Ili madhabahu iweze kufanya kazi lazima awepo kuhani wa madhabahu hiyo anayemwakilisha Mungu wa madhabahu.
“Kuna kuhani wa madhabahu ya Yehova na kuhani wa madhabahu ya shetani.”

Kwa awaida kila madhabahu ina kuhani wake, ukifanikiwa kuibomoa madhabahu ya kichawi halafu hujamuua kuhani kuhani wake basi atakwenda kujega madhabahu mahali pengine.
Kuhani wa Bwana ni daraja la kuwaunganisha watu na Mungu kwa kupokea kutoka kwa Bwana na anachokipokea anakileta kwa watu wa Bwana. Maana yake ili Mungu akupe lazima awepo kuhani wa kutoa mahitaji ya watu na kuyapeleka mbele za Bwana na Mungu anatoa majibu palepale.

Huyu Hana alipokwenda shilo nyumbani mwa Bwana alikutana na kuhani wa Madhabahu ya Bwana ambaye aliona haja zake ni za ajabu akamfananisha kama mtu mlevi lakini kuhani alimwelewa na kumtamkia neno lililomsaidia kupata majibu aliyoyahitaji.
Tunajifunza kwamba kuna mtu ambaye anahitaji mambo fulanifulani ambapo ili kuyapata lazima aende kwenye madhabahu ili akutane na kuhani wa madhabahu.

2 wafalme 1:1-
“Ikawa, baada ya kufa kwake Ahabu, Moabu wakawaasi Israeli. Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu. Lakini malaika wa Bwana akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi sasa, Bwana asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Eliya akaondoka.”

Mungu aliamua kuwakomesha Wafalme ambao walikuwa awakienda kwa wachawi kuuliza kwa habari ya mambo yao. Kulikuwa na miungu ya Ekroni ambayo iliwafanya watu watatuliwe mambo yao. Mtu anayekwenda kwa kuhani wa kichawi anaweza kupata yale mambo anayoyahitaji laziki lazima ayalipie kwa kutoa kafara ya damu. Huyu shetani ni malaika na anawatu ambao huwa anafanya kazi pamoja nao ambao ni makuhani wa kichawi. Watu huenda kwa makuhani hao kutoa kafara kwenye madhabahu ya kuhani wa kishetani lakini huwa hawafiki mbali kwa yale wanaoyapata.
Mwanzo 12: 7 – 8
“Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea. Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli”

Mwanzo 8:20
“Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.”

Baada ya kutoa sadaka Mungu alisikia harufu, maana yake kuna sadaka ambayo lazima ikubalike na Bwana. Mungu aliamua kuchagua kabila la lawi ili watumike katika mahabahu yake kama makuhani ili watimize shughuli za kiibada, kikazi na nyingine za kikuhani ambazo ni kuongoza watu waweze kumfikia Mungu alipo, wengine walikuwa wanasafisha nyumba ya Bwana, wengine walikuwa wakipanga nyumba ya Bwana.
Kuna makuhani wa Mungu na makuhani wa kishetani, ukiangalia kwenye Biblia takatifu utaona kuhani ndiye aliyempaka mafuta Mfalme wa nchi.
1Samweli10:1-
1 samweli 16:13
“Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.”

1 samweli 15:32-
“Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa utepetevu. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka. Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za Bwana huko Gilgali. Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye Bwana akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.”

Samweli akuwa chini ya kuhani wa Bwana Eli na huko alijifunza kumtumikia Bwana mpaka akawa nabii na kuhani wa Bwana. Samweli aliwapaka mafuta Sauli japo sauli hakutenda lile kusudi ambalo Bwana alimwelekeza kulifanya.
1 Samweli 2: 34 – 35
Tunaona Kuhani wa Bwana ndiye anaumuhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Mara nyingi sana watawala wa nchi walipokuwa wanainuka walikuwa wanawauwa makuhani wa Bwana. Mfano mzuri Yezabeli alikuwa ni mwana wa kuhani wa madhabahu ya kishetani, siku mmoja alienda kwa mfalme ahabu na kumchochea mumewe ili awauwe makuhani wa Bwana. Alikuwa akiwakamata makuhani wa Bwana na kuwauwa na kubomoa madhabahu za Bwana kwasababu mahali ambapo makuhani wa Bwana walikuwa wanapatikana kulikuwa na uwepo wa Mungu, vilevile na mahala ambapo kuna makuhani wa kishetani mahali hapo kunakuwa na hali mbaya na ugumu wa maisha na matendo ya kichawi.Yezebeli alikuwa akikamata makuhani na kuwachinja. Kwasababu hiyo pia kuna makuhani wa upande wa giza ambao wanafanya mapeze ya kishetani.

Mungu ameweka taratibu za wanadamu wote kumwabudu yeye lakini shetani naye anapenda kuabudiwa ndiomaana anashindana kuwafuta makuhani wa Bwana wasiwepo kuwaongoza watu kumwabudu Bwana wa Majeshi badala yake wamwabudu yeye.
Ndani ya kila mwanadamu kuna kitu cha kumwabudu Bwana na ibada ikishuka vizuri magonjwa yanaondoka, mikosi na laana zinaondoka zote, taabu na dhiki zinaondoika zote, umaskini unaondoka wote kunakuwa na amani na upendo kwasababu Mungu anakuwa anatawala katikati ya wanadamu.
Kuna watu wenge ni makuhani lakini ukuhani wao umekamatwa na kuzuiliwa, kila mtu amepewa nafasi ya kuwa kuhani kulingana na nafasi yake.
Ufunuo 5:10
“ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”

Sisi ni wafalme na makuhani wa Bwana hapa duniani. Daudi alikuwa ni mfalme wa nchi na kuhani wa nchi.
Waamuzi 17: 7
“Alikuwako mtu mmoja hirimu aliyetoka Bethlehemu-yuda, wa jamaa ya Yuda, aliyekuwa ni Mlawi, naye akakaa huko hali ya ugeni. Mtu huyo akatoka katika huo mji, katika Bethlehemu-yuda, ili aende kukaa hali ya ugeni hapo atakapoona mahali; akafikilia nchi ya vilima vilima ya Efraimu katika safari yake, hata nyumba ya huyo Mika. Mika akamwuliza, Watoka wapi wewe? Akamwambia, Mimi ni Mlawi wa Bethlehemu-yuda, nami naenda kukaa hali ya ugeni po pote nitakapoona mahali. Mika akamwambia, kaa pamoja nami, uwe kwangu baba, tena kuhani, nami nitakupa fedha kumi mwaka kwa mwaka, na nguo ya kuvaa, na vyakula. Basi huyo Mlawi akaingia ndani. Huyo Mlawi aliridhika kukaa na mtu huyo; kisha huyo hirimu akawa kwake kama wanawe mmojawapo. Basi Mika akamweka wakfu huyo Mlawi, huyo hirimu, naye akawa kuhani wake, akakaa nyumbani mwa Mika. Ndipo Mika akasema, Sasa najua ya kwamba Bwana atanitendea mema, kwa kuwa nina Mlawi kuwa kuhani wangu.”

Mika alimwambia huyu Mlawi akae ili awe kwake Baba (Mwanzilishi) ili amlipe. Mika aliridhika kuwa Bwana atamsaidia sababu anamlawi ambaye ni kuhani wake. Ndivyo ilivyo kwenye ulimwengu wa sasahivi baadhi ya watu wana makuhani wao ambao ndio wanaowaongoza kwenye siasa zao, biashara zao, kazi zao, safari zao huchungulia kweye ulimwengu wa rohoni wajue pa kuepuka na pa kusimama ni wapi.
Wapo makuhani wa kichawi kwenye mabonde au kwenye mapori au milimani ambao wanakwenda kunuizia watu walale na kutokuamka na kusimamia mambo ya muhimu kwaajili ya nchi yao. Tumeona Kuhani ndiye anawaunganisha watu kwenye madhabahu husika, akili za watu, macho ya watu, mioyo ya watu, hisia za wato zinaungamanishwa kwenye madhabahu hizo na kumilikiwa. Makuhani wa kichawi hao husimamia madhabahu zao ili mungu wa madhabahu zao asimame. Madhabahu ambazo zinamiliwa na makuhani wa kichawi hulazimisha mambo ya kichawi Yazidi kuabudiwa.
Paulo aliingia mahali kuhubiri injili na watu wa mji ule walipoona anahubiri habari za Ufalme wa Mungu walifahamu mambo yao yataharibika ndipo wakaamua kumpiga kwa mawe.
Ufunuo2:12
“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.”

Antipa alikuwa ni kuhani wa Mungu wa Yehova aliyekuwa akisimama. Kwenye Biblia makuhani wa Mungu walikuwa wakitafutwa na kuwauwa na kuvunja madhabahu zao ili kukomesha kueneza Ufalme wa Mungu lakini haikufanikiwa.
1 Wafalme 13:1-2
“Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba. Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako. Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika. Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena. Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana. Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.
Mtu wa Mungu alisimama akaamua kutoa unabii na Yeroboamu akisema atazaliwa mtu atawauwa makuhani wa mahali pa juu.”

2wafalme 23:20
“Akawaua na makuhani wote wa mahali pa juu waliokuwako huko, juu ya madhabahu, akateketeza mifupa ya watu juu yake; kisha akarejea Yerusalemu.”

Leo tunatakiwa twende mpaka mahali zilipo madhabahu zinazotulaza na kuiba nyota zetu tuzivunje kwa jina la Yesu, zipo madhabahu ambazo zimewashikilia watu.
2 wafalme 2: 8
Yoashi alikuwa akifanya mambo mema machoni pa Bwana sababu alikuwa akielekezwa na kuhani wa Bwana, unaweza kuona
Ili uweze kupata unachokihitaji lazima awepo mtu wa kukusaidia kupata unachokihitaji, unaweza kumpata mtu sahihi au ukampata ambaye siyo sahihi na akakurudisha nyuma.
Kwenye Biblia Mfalme mmoja alipoona hawezi tena akuamua kwenda mpaka kwa kuhani akatuma ujumbe ili amsaidie.
Hesabu 22:6
“Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.”

Kuhani huyu ani wakala wa giza wa kuharibu maisha ya mtu, biashara ya mtu au kazi ya mtu kwa kulaani, kuna watu huwaendea kamuhani wa madhabahu za kishetani ambao wanawafuata ili kupata umaarufu, kushinda kwenye uchaguzi, kupendwa nk lakini sasa ni wakati wa kuwaangamiza makuhani hao wa kishetani na kuzivunja madhabahu zao kwa jina la Yesu.
Unapoanza kuomba kwa mamlaka ya Jina la Yesu ninazivunja madhabahu za makuhani wa kishetani, makuhani hawa huongeza damu za kafara ili kuzidisha vifungo vyao walivyovitega jii yako lakini ipo damu ya mwanakondoo ambayo hufuta na kunyamazisha kafara zote na ndiyo tunaitumia kama silaha ya kuwaangamiza makuhani hawa kwa jina la Yesu. Kumbuka wewe ni Rungu la Bwana na silaha za Bwana za vita.
Yeremia 50:20
“Katika siku hizo na wakati huo, asema Bwana, uovu wa Israeli utatafutwa, wala uovu hapana; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki.”

Unapojitambua kuwa wewe ni nani basi hakuna jambo lolote ambalo watalifanya juu yeko sababu sisi ni silaha za bwana na tukipiga tunawaangamiza na kubomoa madhabahu zao. Watu wengine ni wabishi hawataki kuwaacha watu wa Bwana waende zao hao dawa yao ni kuwaangamiza, imeandikwa “ashindanaye na Bwana atapondwa kabisa”.
Kuna kuhani wa nchi ambaye anawamiliki watu ili wawe na hali ngumu, wawe na unafuu kidogo, wawe na mikosi sababu ya madhabahu zao, kuna vitu kwenye ulimwengu wa rohoni ambavyo vinawazuia watu wasimiliki na kuwaweka chini.
Maombi;
Katika jina la Yesu leo ninawaendea makuhani wa kichawi ninawafyeka kwa jina la Yesu, ninaziendea madhabahu zao ninazivunja kwa jina la Yesu, nazibomoa madhabahu za makuhani wa kishetani zinazoshikilia akili za watu ninazivunja kwa Jina la Yesu, ninatumia mamlaka ya Damu ya Mwanakondoo Yesu kristo kunyamazisha kafara zote, katika jina la Yesu ninawafyeka makuhani wote waliofanya maisha yangu kuwa magumu, makuhani wa kichawi waliochukua nyota yangu, wanaoshindana na watu wa Mungu ninawafyeka nawakamata makuhani wa kichawi wanaotesa familia yangu ninawateketeza kwa jina la Yesu kristo (endelea kuvunja madhabahu za makuhani wa kichani na kuwafyeka makuhani hao kwa jina la Yesu). Amen.

Comments