KUMKIRI BWANA YESU NI JAMBO LA LAZIMA.

Na mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU apewe sifa ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kwa sababu Kusema Ukweli Sio Dhambi Ngoja Niseme Ukweli.
 Ukweli Ni Kwamba "Kila Akiriye Ya Kuwa YESU Ni Mwana Wa MUNGU, MUNGU Hukaa Ndani Yake, Naye Ndani Ya MUNGU- 1 Yohana 4:15. 
- Kukiri Huku Ni Kumkiri Kama Mwokozi Na Kisha Kumpokea Kama Wokovu Wako. 
Unadhani Ni Kwa Nini Ni Muhimu Sana Kumkiri YESU? 
-Ni Kwa Sababu Katika YESU KRISTO Unakaa Utimilifu Wote Wa MUNGU Kwa Jinsi Ya Mwili.
Wakolosai 2:8-10 ''Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya KRISTO. Maana katika yeye(YESU) unakaa utimilifu wote wa MUNGU, kwa jinsi ya kimwili.  Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.'' 

Ndio Maana Agizo La MUNGU Kwa Sauti Lilisikika Live Mbele Ya Wanadamu Kwamba "Huyu Ndiye Mwanangu, Mpendwa Wangu, Ninayetendezwa Nae; Msikieni Yeye-Mathayo 17:5". 
-Kumsikiliza YESU ni kumsikiliza MUNGU aliye hai.


- Ndugu Yangu Kumbe Usipomsikiliza Na Kumtii YESU KRISTO Hakika Hautakuwa Upande Wa MUNGU.
- Na Kama Wewe Hauko Upande Wa YESU Hakika Uko Upande Wa Shetani. 
-Na Upande Wa Shetani Hawahusiki na uzima wa milele, maana kama wasipotubu wakiwa hai basi hakika watakuwa Wanasubiri Jehanamu, Kwa sababu dhambi yako itakaa siku zote maana hawakuitubia.
Ndugu Geuka Leo Na Mpokee YESU KRISTO Na Anza Kutii Neno Lake. 
Nimesema Hapo Juu Kwamba Kusema Ukweli Sio Dhambi Na Ndio Maana Nimesema Ukweli Ili Maelfu Ya Watu Wapone. Naimani Ukweli Huu Utaufanyia Kazi Njema Ya Kumpokea YESU.
Unajua ni kwanini?
Ni  ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka.-Warumi 10:9-10,13'' 
-Ni muhimu sana kumkiri BWANA YESU na kuupokea wokovu wake.
-Kila mtu ana yule anayemkiri lakini kwa ajili ya uzima wa milele na kusamehewa dhambi ni lazima tumkiri BWANA YESU.
Unamkiri BWANA YESU na kuambatana na wokovu wake hata mwisho wako wa kukaa duniani.
Unamkri BWANA YESU na kusamehewa dhambi zako.
Unamkiri BWANA YESU na jina lako linaandikwa mbinguni kwenye kitabu cha uzima.
Kumkiri YESU ni muhimu sana maana hakuna uzima wa milele nje na YESU.
Kwa sababu maisha yanaendelea hivyo napenda ujue kwamba; 
Sio kwamba kukiri tu kunatosha kukupa uzima, bali ni kumkiri YESU na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Kuishi maisha mataktifu ndani ya YESU ni kudumisha ungamo lako kwa YESU siku ulipomkiri.
Waebrania 10:23-24 ''Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu; tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;'' 
-Ungamo letu linaanzia siku tulipomkiri YESU na kumpokea maishani mwetu ili awe mwokozi wetu milele.
-Kushika ungamo ni kudumu katika utakatifu, ni kuitendea kazi sala Ya toba uliyoongozwa na watumishi wa MUNGU siku ulipomkiri BWANA YESU. 
Ndugu, shika ungamo lako ambalo lilizaa agano lako na MUNGU kwa ajili ya uzima wako wa milele.
Kuishi maisha matakatifu ni uamuzi wako lakini kuacha kuishi maisha matakatifu ni uangamivu wako.
Ulipomkiri YESU KRISTO ili awe BWANA na MWOKOZI wa maisha yako, hukufanya jambo la bahati mbaya bali ulikuwa unaukiri uzima wa milele, hivyo unatakiwa sana kubaki kwenye ungamo lako.
Kwanini ni lazima kumkir YESU?
Biblia inatupa jibu zuri lifuatalo, Warumi 10:10 ''Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.''
-Kwa kinywa mtu anaweza kumkiri YESU na kupata Wokovu.
-Wokovu ni kuondolewa kwenye hali mbaya na kupelekwa kwenye hali nzuri. 
-Hakuna hali nzuri kama ufalme wa MUNGU.
Hakuna hali nzuri kama uzima wa milele ambao kupitia YESU KRISTO tu ndio tunaweza kuupokea.
ukiri wako kwa YESU ulikuwa ni muhimu sana maana ulikuwa unahamishwa kutoka kwenye kutawaliwa na shetani na sasa baada ya kumpokea YESU utaanza kutawaliwa na MUNGU aliye hai.
Kama Kwa neema kubwa BWANA YESU alikuhamisha kutoka gizani na sasa uko nuruni, ndugu Biblia inakuomba sana kuyashika maungamo yako kwa BWANA.
Hebu jiulize. kwanini kurudi nyuma?
siku ulipomkiri YESU ni siku pia uliyohamishwa kutoka kutawaliwa na shetani na sasa unatawaliwa na mfalme wa mbinguni.
Wakolosai 1:12-14 ''mkimshukuru BABA, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;''


Kujua kuwa unahitaji dhambi zisamehewe ni hatua ya kwanza ya kuanza safari ya kuutafuta Uzima WA milele.
Kutubu Kwa BWANA YESU na kumpokea ni hatua ya kwanza ya kuingia eneo kamili LA Uzima WA milele.
Kudumu katika Wokovu WA BWANA YESU huku ukiishi maisha matakatifu ni hatua ya kwanza ya kwamba wewe ni mwenyeji WA Uzima WA milele na unasubiri tu SAA ya kwenda huko.
Ndugu, kazi ya kwako kuamua Leo kuhusu hatima yako.
BWANA YESU anakungoja tu utubu na kuokoka ili Uzima WAke uwe kwako.

Matendo 3:19 ''Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;'' 
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. 
Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments