LIJUE NENO LA MUNGU LIKUWEKE HURU.


Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Karibu mpenzi mwana wa Mungu katika saa nzuri ya kujifunza Neno la Mungu.Ombi langu Roho Mtakatifu akufunulie kujua siri iliyoko katika Neno la Mungu, macho na masikio ya rohoni yatiwe nuru ili upate kujua kile ambacho Roho Mtakatifu anataka ujue.Amen
Mwl. na Mwnj Emmanuel
Redeemed Gospel Church
Kibaha-Pwani.
Tel.+255712-660766/+255758-103103/+255689-124215.
E-mail: ekamalamo@gmail. com

Somo letu linatoka kitabu cha Yohana 8:31-32. Maandiko matakatifu yanasema,,,"Basi Yesu akawaambiwa wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli , nayo hiyo kweli itawaweka huru"
Bwana Yesu asifiwe....! Mpenzi mwana wa Mungu najua hakua ambaye hajawahi kuusoma mstari huu; lakini nataka nikwambie jambo moja kwamba, Neno la Mungu ni jipya kila Siku. Upya wake ni nini?...Upya wako huja katika ufunuo mpya kupitia uvuvio wa Roho Mtakatifu kwa kukupa maana iliyompya kwa kona nyingine tofauti na kona uliyowahi kujifunza, na kona hiyo mpya ukupa msaada wa rohoni kukuvukisha katika moja kwenda jingine.
Hapa Tunaona Yesu akiwaambia Wayahudi waliomwamini; ya kwamba, "WAKIKAA KATIKA NENO" watukuwa wanafunzi wa Yesu, na kisha wataijua "KWELI" ambayo itawaweka huru.
Kwa picha iliyopo tunaona kulikuwa na Watahudi wa aina mbili, walio "MWAMINI" na ambao "HAWAKUMWAMINI". ingawa wote walikuwa wakisikiliza neno la Mungu alilokuwa ana hubiri Yesu. Najua utauliza umejuaje jambo hilo? soma biblia yako utaambiwa,,,"BASI IMANI, CHANZO CHAKE NI KUSIKIA; NA KUSIKIA HUJA KWA NENO LA KRISTO" hiyo utaisona Warumi 10:17.
Linganisha na maneno ya Yesu alivyosema,,,,"BASI YESU AKAWAAMBIA WALE WAYAHUDI WALIOMWAMINI" hapa utaona Wayahudi walikuwa wengi na wengi walisikia neno lakini baadhi yao hawakumwamini Yesu (yaani hawakuamini Neno) ambalo linawapa chanzo cha imani.

Sasa angalia Yesu alivyowaambia Wayahudi walioamini, alisemaa,,,,"NINYI MKIKAA KATIKA NENO LANGU , MMEKUWA WANAFUNZI WANGU KWELI KWELI" Unaweza kujiuliza kwa nini Yesu alisema,,"WAKAE KWENYE NENO" alisema hivyo ili wajue kukaa kwao katika Neno na si kusikia tu kutawapa nafasi ya kuwa "WANAFUNZI" na tunajua kabisa mwanafunzi hujifunza ili kupitia alichojinza kimsaidie kutoka katika shida ambayo asingeweza kutoka kama asingejifunza mbinu za kumtoa katika hiyo.
Ndiyo maana Yesu aliacha agizo hili kwa mitume akusema,,,"....MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI". hakusema wawe wafuasi wa dini flani au watu wa mtu flani bali wawe wanafunzi.
Wachungaji wengi hawawafanyi watu kuwa "WANAFUNZI" wanawafanya kuwa washirika wao ili kupitia wao wapate faida zao; maana hawawapi "MAFUNDISHO". yatakayo wasaidia kuwaweka huru weny ewe kupitia NENO.

JINSI YA KUTOKA KUTOKA KATIKA VIFUNGO KWA KUPITIA NENO.
Jambo la I.
Tafuta Neno ambalo limebeba msaada unaolingana na Tatizo lako.
Ukisoma kitabu cha Isaya 55:11 maandiko yanasema,,,"NDIVYO LITAKAVYOKUWA NENO LANGU, LITOKALO KATIKA KINYWA CHANGU; HALITANIRUDIA BURE BALI LUTATIMIZA MAPEBZI YANGU, NALO LITAFANIKIWA KATIKA MAMBO YALE NILIYOLITUMA" Bwana Yesu asifiwe....! Huwezi kujua jambo hili kama huna "KWELI" (neno la Mungu)
Kama unapita katika shida ya UGONJWA wowote huna haja ya kuambiwa njoo na PESA, CHUMVI,MAJI, nk. Lakini kama umepita katika shule ya Yesu ukawa"MWANAFUNZI" ooooh!...sikia nikwambie uanafunzi wako utakuweka huru kweli kweli; maana utatafuta mstari katika Biblia yako kuhusu ugonjwa uwe na uhakika Roho Mtakatifu atakupitisha Mathayo 8:17 atakwambia,,,"....MWENYEWE ALIUTWAA UDHAIFU WETU, NA KUYACHUKUA MAGONJWA YETU" nenda na mstari huu mbele za Bwana; na kwa kuwa Mungu amesema analiangilia NENO oooh!....uwe na uhakika utawekwe huru kweli kweli Bwana Yesu asifiweeee!

Hata kama wewe ni TASA miaka yote tafuta shule uliyojifunza ukawa "MWANAFUNZI" chuku mastari bwana nenda mbele za Mungu mwambie, umesema,,"HAKUTAKUWA NA TASA WALA MWENYE KUHARIBU MIMBA" nakwambia kwamba Mungu hatakuwa hana njia yoyote ya kushindwa kukupa motto maana amesema mwenyewe bwana...lazima Mungu alifungue tumbo lako; hajarishi umezaliwa TASA au umerogwa naraka nikwambie madamu wewe ni "MZAO WA JIFALME" basi ujue katika uzao huo hakuna kurogwa wa utasa; kamuuluze Hana atakwambia Samweli alimpatia wapi? uwe na uhakika atakwambia "Madhabahuni" kwa njia ya maombi.
Hata kama ni UMASIKINI tafuta andiko linalozungumzia kutolewa katika umasikini.Maandiko yanasema,,,"YESU ALIFANYIKA MASIKINI ILI SISI TUWE MATAJIRI KWA UMASIKINI" (2 Wakorintho 8:9)
Chukua buashara yako au kitu chochote ambacho unafanya kiweke mbele za Bwana, hata kama ni kidigo bend a na NENO,,,"UKIWA WEWE U SAFI NA UELEKEVU; HAKIKA YEYE SASA ANGEAMKA KWA AJILI YAKO, NA NA KUYAFANYA MAKAZI YA HAKI YAKO KUFANIKIWA" Anglia mstari unaofuata anasema,,,"TENA UJAPOKUWAKUWA HUO MWANZO WAKO ULIKUWA MDOGO, LAKINI MWISHO WAKO UNGEONGEZEKA SANA" (Ayubu 8:6-7)
Unapokwenda na mstari kama huu mbele za Bwana na huku ukijua kabisa uko sawa na Mungu rohoni lazima "UFANIKIWE KATIKA MAMBO YOTE KAMA ROHO YAKO IFANIKIWAVYO" Ndiposa Mungu atakuja kila unachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake ndani ya Kristo.

Ninayo mengi ya kusema lakini kwa leo tuishie hapo naamini umwpata kitu cha kukusaidia kutoka imani kwenda inani.
Weka mazoea ya kuishi kwa Neno na si kuishi kwa kuweka tunaini katika vitu vinavyooneka, maana Vitu vinapita bali Neno linadumu milele.

Somo hili pia utalisikia live J.nne hii inayokuja katika WAPO RADIO 98.1 Hapa Dar Es Salaam kuanzia saa 8:00 Mchana.
Nawatakia mchana mwema.
MUNGU AWABARIKI

Comments