MACHUKIZO YA YEZEBELI YANAYOANGAMIZA MAELFU YA WATU.

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe sana ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU.
Mimi Peter Siku moja Nilikuwa Naomba Usiku, Wakati Naendelea Na Maombi Ghafla Kwa Macho Ya Rohoni Nikaona Joka Kubwa Sana Limelala Ardhini Huku Limeachama Na Ndani Ya Joka Lile Kuna Barabara Pana Kama Ya Lami Na Upana Wa Barabara Hiyo Hata Magari Makubwa 4 Yanaweza Kupita Kwa Pamoja Lakini Ni Tumboni Mwa Joka, Kulikuwa Na Watu Wanatembea Mle Kwenye Tumbo La Joka na kwa nilivyowaona ni hakika hawakuwa wanajua hata kidogo kama wako tumboni mwa joka. Katika Wote Niliyemuona Kwa Uzuri Ni Dada Mmoja Kajipodoa Sana Na Ana Nywele Bandia pia kavaa kisketi kifupi sana.  Haikuwa ndoto bali live na nilipoona tu hayo Nilijikuta Nabadili Maombi Muda Ule Ule Na Kuanza Kuomba Maombi Ya Vita. Dada Yule Alikuwa Anatembea Tembea Huku Anashangaa Shangaa akiangalia juu maana ni kama kuna majengo marefu lakini mimi niliye nje ndiye ninayejua kwamba mle ni ndani ya joka. Dada yule alikuwa Kama Mtu Anavyoshangaa Ghorofa Lefu, Hakujua Kama Yuko Tumboni Mwa Joka. Ulikuwa Ni Ufunuo Mpya Kwangu, Kuona Tukio Hilo Huku Nimesimama Naomba Nikakumbuka Neno La BWANA YESU Kwamba "ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.-Mathayo 7:13-14 ". 

 Niliwaza  sana kwanini watu wale wanaotembea wakiwa ndani ya joka hata hawashituki, nilimtazama yule nyoka hadi macho yake mekundu sana lakini wanadamu walio ndani yake wanashangilia tu na kufurahi huku wengine wakivuta sigara zao na wengine wakinywa pombe zao na wengine wakivutana kwenda kuzini lakini kumbe wako ndani ya joka. Niliwaza sana siku hiyo baada ya maombi na nilitamani kila mtu aachane na njia pana ambayo ni shetani na aje katika njia ya mbinguni ambayo ni YESU KRISTO. Njia ya mbinguni ni wachache sana wanaoiona maana kuiona kwa njia hii ni kumtii tu YESU KRISTO na neno lake.
Siku za nyuma niliwahi kupost ujumbe wa kuhusu mapambo na madhara yake, na ujumbe ule  uliniletea maadui wengi sana,  wengi sana walini-unfriend na nilipigiwa simu na hadi na watumishi wakubwa wakinishangaa na kunisimanga, Lakini nilitamani tu ule mzigo wa injili alionibebesha MUNGU basi awape na wao ili tuheshimiane.
Kila mtu alisema aliloweza kusema lakini ndani yangu ROHO wa MUNGU alisema songa mbele na mweleze kila mtu maana ni siku za mwisho.
Ndugu Zangu Natamani Kila Ndugu Yangu Na Rafiki Yangu Waokoke Na Kujitenga Na Machukizo. 
Natamani kila ndugu ajue kwamba Nywele Bandia, kujichubua, mawigi, kuongeza matiti, kuongeza makalio, kuchonga pua, kupaka nywele dawa  Vyote Kwenye Mwili Wake Ni Pando La shetani Kuhakikisha Unatembea Kwenye Barabara Nzuri Ila Ni Ya Kwenda Jehanamu. Vitu hivyo ni roho ya yezebeli na ambayo sasa imeingia makanisani kwa kasi ya ajabu.

Ufunuo 2:20 '' Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. ''
-Anayeambiwa haya ni Kanisa la Thiatira ambalo ni kanisa la kinabii likichukua nyakati fulani ambayo watu wa kanisa wataishi. Kanisa linaambiwa kwamba linamkubali na kumpa nafasi Yezebeli na huyo yezebeli ni roho tu ya kishetani ambayo imetumwa na shetani ili kuwakamata wanadamu.
Thiatira wa leo inawezekana kabisa likawa ni kanisa kama la leo. 

Yezebeli Ametanda Dunia Nzima.
-Yezebeli Ni roho Chafu Ya shetani. 
-Yezebeli Ndio Mwanamke Pekee Mpaka Wanja Aliyetajwa Kwenye Biblia
2 Wafalme 9:30 '' Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani. ''
-Yezebeli ndiye pia mwanamke pekee ambaye anaendelea kutajwa  kwenye Biblia aliye upande wa shetani tena ni roho kabisa ya shetani.
-Biblia inasema Yezebeli alikuwa akipaka wanja hivyo wapaka wanja kwa vyovyote vile mmemfuata Yezebeli maana hakuna popote Eva au Sara au Naomi au Mariam anatajwa akipaka wanja, je tujiulize mimi na wewe chanzo cha wanja ni nani? jibu lake ni Yezebeli na kanisa linaonywa lisiridhie mambo ya Yezebeli kwa watu wa kanisa.
Mapepo yanawatesa wanawake wengi sana leo kuliko wanaume lakini watu hata hatushituki kwamba huyo ni Yezebeli yuko site akifanya kazi. Hapa Tanzania hata wauzaji wengi wa vipodozi wala sio wakristo maana ukristo na Yezebeli hawana uhusiano.
Hata viwanda vingi vya kutengeneza mapambo haviko katika nchi ambazo Ukristo umekaa sawasawa, huyo ni Yezebeli yuko kazini.
Yezebeli alikuwa ni mwanadamu mwabudu shetani lakini leo roho ya Yezebeli ndio inafanya kazi kwa upande wa shetani.

-Yezebeli Alikuwa Mwabudu shetani Aliyepambana Na Nabii Eliya, 
Hii ni roho inayotesa wengi 
Ufunuo 17:1-5 '' Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake. Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. '' 
-Hii ni roho ya shetani inayowakosesha wengi.
Ni mama wa machukizo yote ya nchi.
Yezebeli Ndio Chanzo Cha Nguo Za Kikahaba
-Yezebeli Ndio Chanzo Cha Dini Wanaompinga BWANA YESU, Ufunuo 17 Inasema Jezebeli Amezini Na Wafalme Wa Dunia Maana Yake Ameingia Mapatano/ Nao Ili Waseme Kwamba Ushoga Ni Halali, Waseme Kwamba Kumwabudu Mariam Na Sanamu Ni Halali, Mapatano hayo kati ya shetani na wakubwa wa dunia yatazaa dhambi nyingi na uovu mwingi. Lengo tu kuhakikisha mwanadamu haendi uzima wa milele maana hakuna uzima wa milele nje na BWANA YESU(Yohana 14:6, Warumi 10:13, Matendo 4:12)

Ndugu Zangu BWANA YESU Bado Anasema Kwamba Tupite Kupitia Njia Iliyo Nyembamba Maana Njia Ya Upotevuni Ni Pana Sana. 
Kuna baadhi ya watumishi Leo Wako Tayari kuruhusu Mavazi Ya Kikahaba Kanisani Ili Tu Wasikimbiwe Na Waumini, Ukifunuliwa Ili Ulisaidie Kanisa Wanasema Kwamba Aliyekufunulia Sio ROHO Bali loho. Ok Tutafika Tu. Watu Hawataki Kuambiwa Kwamba Nywele Bandia Na Mawigi Ni Dhambi. MUNGU Anachukizwa.
Hosea 2:13 '' Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema BWANA.'' 
-Pete za masiko ndio heleni ambazo kuna watu akizikosa heleni zake hata kanisani haendi siku hiyo, Yezebeli yuko kazini.
 Mwanzo 35:1-5 '' MUNGU akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie MUNGU madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako. Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu. Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia MUNGU madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea. Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu. '' 
-Chochote ambacho kimeletwa na shetani hiyo ni miungu migeni na inatakiwa iondolewe itoke kwa wateule wa MUNGU.
-Ona hapo kwenye maandiko jinsi watu walivyompa Yakobo Miungu migeni na yeye akaitupa, miungu hiyo migeni ilikuwa mikononi mwao, na mingene ilikuwa masikioni mwao.
-Je kulingana na maandiko hayo tu unadhani ni lini hereni iliacha kuwa miungu migeni?
-Kwanini  wakati mwingine mapepo yanakataa kutoka kwa watu hadi wanapovuliwa hereni?
Ni mambo magumu sana lakini mwenye siko la kusikia anaweza kusikia vilevile leo.
-Kuna watu bila wigi anaona kama hajapendeza na anaweza hata akaarisha safari, hiyo ni miungu migeni.
Yezebeli anatesa wengi sana.
 Vitu hivyo vinaitwa miungu migeni maana vina roho ya shetani ya kutaka kuabudiwa. ona hapa
Kutoka 33:4-6 ''Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hapana mtu aliyevaa vyombo vyake vya uzuri. BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa vueni vyombo vyenu vya uzuri ili nipate kujua nitakalowatenda. Basi wana wa Israeli wakavua vyombo vyao vyote vya uzuri, tangu mlima wa Horebu na mbele.''
-Unadhani vyombo vya uzuri walivyoambiwa waisraeli wavivue ni nini?
Jibu ni mapambo  na  mapambo hayo hayo yaliwakosesha waisraeli hadi wakavua na kutengeneza ndama na kuiabudu, maana vitu hivyo ni miungu migeni na ina roho ya shetani ndani yake ambayo hutaka kuabudiwa  ndio maana watu wale wakaiabudu ndama ambayo imetengenezwa kwa miungu migeni waliyokuwa wanaivaa. MUNGU akasema kama akiwa katikati yao atawaangamiza kwa sababu ya mapambo yao ndio maana wakaamuriwa kuvua haraka. Ona jinsi mapambo hayo yalivyowakosesha;
Kutoka 32:1-7 '' Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee. Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana. Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze. BWANA akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, '' 
-miungu migeni ina tabia ya kutaka kuabudiwa na ni makao ya shetani akutipia mapepo.

ndugu yangu, Hukumu Ya MUNGU Haina Rufaa. Fanya Machukizo Leo Ukidhani Utapona Siku Ya Mwisho. Biblia Iko Wazi Kabisa Kwamba Watenda Dhambi Wote Wataenda Jehanamu. Ni Heri Kutubu Leo Na Kugeuka Ndipo Utapona Na Moto. BWANA YESU Yuko Tayari Kukupokea Leo Kama Ukimpokea Na Kutubu.
Baada ya ujumbe wa kwanza kuhusu vitu bandia ambao niliupost mwanzoni mwa mwaka 2014, watu wengi sana walinichukia na hata kuwa wananitumia sms mbaya za kunitukana lakini miezi kadhaa baadae watu wengi sana tena waliomba sana nirudie kufundisha somo hilo. MUNGU amenipa somo jingine  na ambalo ni hili na  nimefafanua zaidi.
Ndugu yangu ni jukumu lako kujichunguza kama unampendeza MUNGU au unamchukiza MUNGU wa mbinguni.
Kumbuka kwamba  nywele za marehemu wa mataifa makubwa zisikufanye unajisike kwa kuzivaa.
Nywele zilizotolewa sadaka kwa mashetani hata kama zimepita kiwandani kunyooshwa bado ni miungu migeni tu na haitakiwi kwa watu wa MUNGU.
Mbinguni kila mtu ataenda kivyake, ukimfuata sana rafiki yako au mtumishi furahi huku ukijua kabisa kwamba yale ni makosa haitakusaidia.
Baada ya ujumbe wa kwanza niliulizwa sana swali hili ''Mbona mama wachungaji huvaa kila jumapili''
Niliwaambia wamtii MUNGU na sio mama mchungaji maana mama mchungaji ni mwanadamu tu na yeye anahitaji neema ya MUNGU kama wewe.
Mithali 14:12 '' Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.''
-Iko njia  kwako ni kama ni sawa tu lakini inaweza kukuletea matekeo mabaya.
Hata hayo niliyoyasema hapo juu yanaweza kuonekana tu mazuri tu na hayana madhara lakini chunguza neno la MUNGU ndio utajua kwamba yana madhara na ni hatari.
Hata kama mama mtumishi fulani anavaa naomba wewe usimuige maana hana mbingu ya kukupeleka.
Mtii BWANA YESU maana yeye ndiye pekee aliye na uzima wako wa milele.
 Ndugu, Je wewe uko njia mbaya na njia nzuri kulingana na ulivyojifunza somo hili? 
wewe ndiye mwenye majibu yote, mimi kazi yangu ni kukushauri tu.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi
tutajifunza tena siku nyingine.na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea
ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika
jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza
kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki
upotelee motoni anataka uende uzimani aliko
KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments