![]() |
Haijajulikana ni nani anayechoma moto makanisa |
Makanisa
manne yameteketezwa katika mkoa wa Kagera, kaskazini magharibi mwa
Tanzania na kufikisha saba, idadi ya makanisa yaliyochomwa moto eneo
hilo mwezi huu.
Hadi sasa haijabainika ni kundi gani linalohusika na vitendo hivyo, kwa mujibu wa polisi.
Lakini baadhi ya viongozi wa dini wameambia mwandishi wa BBC Leonard Mubali kuwa huenda ni matokeo ya uhasama wa kidini.
Kuchomwa kwa makanisa hayo kumeongeza hofu kwa viongozi wa makanisa na waumini kuhusu usalama wao.
Mchungaji
Vedasto Athanasi ni Askofu wa kanisa la Living Water mkoani humo, ambaye
kanisa lake limechomwa kwa mara ya tatu sasa, ni mmoja wa walioingiwa
na wasiwasi.
“Kitendo
hakiwezi kukafanyika mara tatu, na hakuna hatua zinazochukuliwa. Naona
ufuatiliaji wa suala hili ni mdogo sana,” amesema.
Mkuu wa mkoa
wa Kagera, John Mongela, ameiambia BBC kuwa mazingira ya matukio hayo
yana utata kiasi kwamba ni vigumu kutambua mara moja kuwa yana malengo
gani.
”Kwa jinsi
ambavyo tuliona, hupati shida ya moja kwa moja, ujue kama ni siasa au ni
nini. Kwa sababu haya yanafanyika wakati hakuna watu,” amesema.
”Lolote lile ambalo litakuja upande wetu, tutalifanyia kazi na kuona kama litatusaidia katika kutuelekeza.”
Crodward
Edward, mwenyekiti wa muungano wa makanisa ya Kipentekoste mkoani
Kagera, anasema anaridhishwa na hatua za mamlaka za usalama na kuwataka
waumini kuwa watulivu kipindi hiki cha matukio haya.
Habari kuhusu Kuchomwa moto makanisa matatu ya mwanzo kama hukuisoma FUNGUA HAPA
Comments