MAOMBI PEKEE HAYATOSHI KUMPELEKA MTU IKULU AWE RAIS BALI PIA KURA YAKO INAHITAJIKA TAR.25 OCT.2015

Mch.Gasper Madumla.
Na mchungaji Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
Kupiga kura ni haki yako ya msingi,usithubutu kuipoteza haki hii. Usiwe mmoja wa watu wenye kulalamika kutwa nzima kwa kuwasema vibaya viongozi wa serikali kwamba ni wabaya,hawafai! kumbe haukuusika kupiga kura. Sasa,unafikiri kama utaishia kuomba tu,ni nani atakuchagulia yule umtakaye?
Mch. MadumlaTuache mawazo haya yasiyokuwa na maana bali tushiriki sote katika zoezi la kiga kura. Kumbuka ukikaa kimya pasipo kupiga kura,wenzako wajanja watapiga kura na kukuletea rais wamtakao wao. Tusiangamizwe kwa kukosa maharifa (Hosea 4:6)
Kumbuka mpendwa,ukikataa kuitii mamlaka iliyowekwa na serikali yako mfano ukikataa haki yako ya msingi ya kiserikali ya kupiga kula ni dhambi kabisa. Maana kila atakayeikiuka mamlaka iliyowekwa na serikali~hakuikiuka serikali tu,bali amekiuka sheria ya Mungu,maana mamlaka iliyopo imeamriwa na Mungu. ( Warumi 13:1 )
Huu sio wakati wa kulia lia tena,bali ni wakati wa kuwaweka viongozi sahihi madarakani. Sisi watu wa imani katika Kristo Yesu,tumepewa mambo mawali ya kufanya katika uchaguzi mkuu 2015. Mambo hayo ni kama ifuatavyo;
01) Kuombea amani taifa letu,na kuomba kumpata rais bora.
02.)Kufanya maamuzi sahihi ya mwisho kwa kupiga kura.
Ikiwa wewe utashindwa kuyatimiza hayo mawili basi wafanya vibaya mno maana mawili hayo yanategemeana. Mtu akiomba pasipo kupiga kura,basi imani ya mtu huyo inahitilafu,alikadhalika mtu akipiga kula pasipo kuomba,imani yake inaitilafu. Biblia imejaribu kutueleza vizuri jambo hili,tunasoma;
Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,
ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.” Matendo 1:23-26
Mitume waliomba kwanza kabla ya kupiga kura,maana kupitia maombi yanatupelekea kumpata rais bora. Mara tu ya kuomba,mitume wakapiga kura na hatimaye kura ikamuangukia Mathiya. Labda waweza kujiuliza kwamba kwa nini mitume wasingeomba tu,alafu wakakaa kimya,kisha Mathiya akapatikana automatically. Haikuwa hivyo kwa sababu hiyo sio kanuni ya Mungu ya kumpata kiongozi.
Hivyo basi kwa mitume tunajifunza kwamba,ingawa waliomba lakini walihitajika kupiga kura. Ikiwa mitume waliomba na kupiga kura wewe ni nani hata ukatae? Tena kumbuka hawa mitume walikuwa ni wapakwa mafuta wa BWANA lakini hawakuona ile namna ya kuwa mitume ni kitu cha kuchukuliana nacho,bali walishiriki katika yote .
Sababu kama  wangejihesabia haki kwa utume wao,basi labda wangeweza kuomba kisha wawatume watu wengine ndio wapige kura kwa niaba yao. Lakini haikuwa hivyo.
Bali mbali na kuomba,wakashiriki wakatia mikono yao katika zoezi la kupiga kura. Ninajua kuwa Mathiya hakuwa kiongozi wa siasa kama hawa tunaokwenda kuwachagua katika taifa letu,bali alikuwa mtu wa imani kuishika nafasi ya mtume Yuda aliyoikosa~Sasa hata kama ni hivyo bali ishu ya msingi ni ile njia iliyotumika ya kumpata Mathiya kama kiongozi ,ambapo njia yake inafanana na njia yetu ya kupiga kura.
Nami nakusii leo,uende ukajumuike na watanzania wote kupiga kura. Wapendwa,maombi peke yake hayatoshi bali kura yako inahitajika.
Kwa huduma ya maombi nipigie kwa +255 655 11 11 49.
Mchungaji Gasper Madumla.
Beroya bible fellowship church(Kimara,Dar,TZ)
UBARIKIWE.

Comments