MATUNDA HUTUJULISHA AINA YA MTI, KAMA NI MWEMA AU MBAYA!.

Na Mwl Nickson Mabena


"Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakinu kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?. Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya." MATHAYO 7:15-18
Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu unayesoma ujumbe huu, ujumbe huu ni muhimu kwako kuusoma pia kuufanyia kazi. Naamini Roho Mtakatifu amekupa nafasi hii ya kuusoma, kwa sababu anakusudi maalumu!.
Unajua, Ukitaka Kujua aina ya Mti flani, Matunda yake ndio yatakujulisha kwamba huu ni Mti gani, na ule ni mti gani,
Wakati mwingine Majani, au matawi ya huo mti yanaweza yakakuchanganya kidogo, kujua aina ya huo mti!.
Vivyo hivyo ukitaka kujua Mtu flani ni wa aina gani, Je! Ni Mtumishi wa Mungu au wa Shetani, Je! Yesu yupp ndani yake au Anaigiza tu. Wewe usiangaike na Kingine, bali angalia Matunda yake!.
Yesu anatufundisha, jinsi ya Kuwatambua Manabii wa Uongo, anasema Kwa Matunda yao tutawatambua, Kwa Sababu Mti Mwema huzaa Matunda mazuri, na Mti mwovu huzaa Matunda mabaya.
Kwa hiyo, sipati tabu kumtambua Mtumishi wa Mungu wa kweli, na Wa Uongo.
Kumtambua Mtoto wa Mungu aliyezaliwa na Yesu Kristo, na Ambaye hajamwamini Yesu!.

NENO LA MUNGU LINASEMA,
"Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu yoyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake." 1YOHANA 3:9-10

Kumbe tunaweza kuwatambua watoto wa Mungu, na Wa Ibilisi nao.
MTI MWEMA HUZAA MATUNDA YAFUATAYO.
Galatia 5:
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Kama Roho Mtakatifu yupo ndani yako, Hayo ndio tumategemea kuyaona kwako, hayo ndio yatatujulisha kama Roho wa Mungu yupo ndani yako!.
MTI MWOVU HUZAA MATUNDA YAFUATAYO.
"Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;". MATHAYO 15:19
Pia,
GALATIA 5:

19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndio haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Kama unatenda Mambo ya jinsi hiyo hapo, Wewe ni Mti Mwovu, hata kama unaitwa Mkristo, au Mtume na nabii, Ndani yako hayupo Roho wa Yesu, yupo Shetani!.
Wakati Mwingine, Mtu akileta ubishani kwenye Mambo ya Mungu, au akiuliza Swali, mfano kwenye facebook, ili nijue Jinsi ya Kumjibu, napitia kwanza profile lake, nione amelike nini, au huwa anapost nini kwenye wall yake,
Hiyo hunisaidia kumjua ni Mtu wa aina gani,
Je! Anampenda Mungu, au Amelike page za Wasanii wa Bongo fleva tu, na Page za Ngono!?. Hiyo itanisaidia kujua jinsi ya kumjibu!.
Mtu mwingine, huwezi kumjua, hadi achokozwe, afanyiwe Ubaya flani utakaomuuma, ndio utajua ndani yake kuna nini!.
Baada ya Kusoma hayo, Je! Wewe ni Mti wa Aina Gani!?.
Ni Mti Mwema, au Mti Mwovu!?.
Ndani yako kuna Roho wa Kristo, au kuna roho nyongine!?.
TAFAKARI!.
NIKITAKA KUJUA UMEBEBA MTI GANI NDANI YAKO, SIANGALII DINI YAKO, BALI MATUNDA YAKO, MAANA MATUNDA YAKO NDIO YANANIJULISHA AINA YA MTI ULIO NDANI YAKO!!.
Mungu akubariki sana, uliyesoma Ujumbe huu!.
Kama Hujaokoka, na Ungependa kuokoka, nafasi bado ipo, lakini kumbuka Saa ya Wokovu ni Sasa!.
Fanya Uamuzi leo, Yesu yupo kwa ajili yako!!.
Asante, kwa kunisikiliza!!.
.....Amen, amen.
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments

Anonymous said…
AMEN