OLE WAO WAJASILIADHAMBI

Na Godfrey Miyonjo.

“Ole wao wavutao uovu kwa kamba za ubatili, na dhambi kama kwa kamba za gari”
ISAYA 5:18.
BWANA YESU asifiwe sana.
Siku ya leo nimepata msukumo mkubwa sana wa kuzunguzia UJASILIADHAMBI,
Nianze kwa kutoa maana/tafsiri japo siyo rasmi sana ya UJASILIADHAMBI,
UJASILIADHAMBI ni kitendo cha mtu kuanzisha biashara ya dhambi.
MJASILIADHAMBI yeyote huwa anatafuta fursa ya DHAMBI na kuitumia.
Mtu anatafuta nafasi ya kuwa mahala flani ili atende dhambim
Nimewaona WAJASILIADHAMBI wengi sana chini ya jua, na ndiyo maana Roho wa Mungu amenisukuma kulisema hili.
Kuna wajasiliadhambi wadogo, wakati na wakubwa pia,
Hii hutokana na kila mmoja na fursa/nafasi aliyonayo.
Biblia inasema
“Kwa kila jambo kuna majira yake;
Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”
MHUBIRI 3:1
Mhubiri anayasema haya akimaanisha kuwa kila mwanadamu aliye mahali popote, na wakati wowote, hayupo pale alipo kwa bahati mbaya.
Lipo kusudi la Mungu lililomfanya awepo mahala pale kwa wakati huo ili alitimize.
Lakini kama inavyojulikana kuwa shetani ni mwongo, tena ni baba wa uongo, mara nyingi hugeuza neno la Mungu (kusudi la Mungu) na kuwapotosha watu wasio makini,
Yaani wakati Mungu amemweka mtu mahala Fulani ili alitimize kusudi flani, mtu huyo hudanganywa na shetani kisha kuitumia fursa hiyo kufanya UJASILIADHAMBI.
Katika biblia kuna mifano mingi ya watu waliopewa fursa na Mungu ya kuwa mahali flani,ili wayatimize mapenzi ya Mungu lakini wao badala yake waliyatimiza mapenzi ya shetani (walifanya UJASILIADHAMBI),
Nitoe mifano michache kutoka katika biblia.
Katika kitabu cha MWANZO 2:15.
Mungu alimweka mtu katika bustani ya Edeni ili alime na kuitunza.
Kusudi la Mungu lilikuwa mtu huyo alime na kuitunza bustani.
Lakini matokeo yake ndani ya biblia tunaona mtu huyo akiwa katika bustani ya Edeni anatokea kiumbe mwerevu, ambaye ni nyoka (shetani) na kumdanganya mtu huyo na kumfanya awe MJASILIADHAMBI kwa kutekeleza majukumu yaliyo kinyume na maagizo ya Mungu.
Na mtu huyo baada ya kukiuka agizo la Mungu na kufanya UJASILIADHAMBI, Mungu alimwadhibu
MWANZO 3:1-19.
Vilevile katika kitabu cha samweli wa kwanza, sura ya 2 mstari wa 12 hadi 17 tunao vijana wa mzee Eli ambao walipewa nafasi na Mungu kwa wakati ule wao kuwa makuhani,
Na wao kwa kupotoshwa na shetani waliitumia nafasi (fursa) hiyo vibaya wakafanya UJASILIADHAMBI.
Nao pia mwisho wa siku Mungu akawaadhibu.
1SAM 4:1-11.
Pia katika kitabu cha matendo ya mitume, sura ya 5 mstari wa 1 hadi ule wa 11,
Tunaona watu wawili, Anania na Safira (Mume na Mke) walifanya UJASILIADHAMBI,
Hao nao waliadhibiwa naMungu,
Kuna mtu pia alikuwa mfalme, jana lake ni sauli, naye kwa nafasi aliyopewa na Mungu akageuka na kufanya UJASILIADHAMBI,
Mungu akamwadhibu pia
1SAM 15:1-35, 31:1-6.
Ipo mifano mingine mingi sana san ya WAJASILIADHAMBI, ila kwa leo tuishie hapo.
Nimeyasema hayo ili ijulikane kuwa Mungu anauchukia UJASILIADHMBI,
Na kila mmoja atambue kuwa Kama watenda hayo WAJASILIADHAMBI wa nyakati zile, anaweza kutenda pia kwa WAJSILIADHAMBI wa sasa.
Hivyo tuwe makini, tutende sawasawa na Mapenzi ya Mungu kwa wakati huu ambao Mungu ametupatia fursa ya kuwepo chini ya jua.
Inashangaza na kusikitisha kuona watu wanaendea kutumia vibaya fursa zao walizopewa na Mungu.
Kuna watu wamepata fura ya:
Kuwa marais,
Kuwa mawaziri,
Kuwa wabunge,
Kuwa makatibu wakuu,
Kuwa wakuu wa mikoa,
Kuwa wakuu wa wilaya,
Kuwa maaskari,
Kuwa maaskofu,
Kuwa wachungaji,
Kuwa manabii,
Kuwa mitume,
Kuwa wainjilisti,
Kuwa waimbaji,
Kuwa waombaji,
Kuwa wakulima,
Kuwa wafugaji,
Kuwa wafanyabiashara,
Kuwa na umbo na sura nzuri,
Kuwa wasomi (wanafuzi wa shule za msingi, sekondari, chuo kikuu, waalimu, madaktari, manesi, maafisa kilimo, Maprofesa, N.K)
Wanatumia nafasi zao vibaya kwa kufanya UJASILIADHAMBI.
Mungu amenituma kwa watu hao ili niseme OLE WAO,
Kwa maana kikombe cha ghadhabu ya Mungu kimefurika,
Mungu anakusudia kuleta hukumu juu yao,
Na ijulikane kuwa imeandikwa HUKUMU YA MUNGU HAINA HURUMA,
Kile alichokipanda mtu ndicho atakachokivuna siku ile,
Lakini heri yake Yule atubuye kabla haijaja siku ile,
Kwa maana atakayefika siku ile pasipo kutubu, kwake itakuwa kilio na kusaga meno,
Na ndiyo maana Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,
EWE MJASILIADHAMBI, TUBU LEO UMWAMINI YESU AKUSAMEHE DHAMBI NA KUKUFANYA KUWA MTOTO HALALI WA MUNGU.
Ni mimi ndugu yenu Katika Kristo
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu)
WhatsApp 0757649495.

Comments