PETER MABULA:NAMSHUKURU MUNGU SANA KWA HILI.


BWANA YESU atukuzwe.
Namshukuru MUNGU kwa blog yangu ya www.maishaushindi.blogspot.com maana watu wameshai-view mara Milioni moja hadi kufika leo.
Namshukuru MUNGU maana katika blog hii ya MAISHA YA USHINDI kuna masomo zaidi ya 2000 kutoka kwangu na kwa watumishi wengine.
Namshukuru MUNGU maana shuhuda ndizo zimeongoza kwa kusomwa.
Namshukuru MUNGU maana ameikinga blog yangu dhidi ya  maadui wa mtandao ambao wameiwinda sana, lakini jambo kubwa ni blog kupata kibali mbele za watu wapenda kwenda mbinguni.

Namshukuru MUNGU pia maana sikutangaza biashara ya mtu kwenye blog japokuwa kuna wakati nilishawishika kuitumia kibiashara  ili nipate pesa lakini ROHO wa MUNGU akanikataza maana ningezuia watu kujifunza neno la kukalia kuangalia matangazo tu ya biashara ambazo zingine ni machukizo kwa MUNGU.
Na tena matangazo mengine huwa juu hata ya maandisho ya neno uliyoweka.


Huwa ni ngumu sana kwa blog au website za neno la MUNGU kusomwa kiasi hiki maana watu wengi hupenda udaku na uongo na mambo machafu kuangalia hivyo blog za injili kutokusomwa sana hata hivyo ashukuriwe MUNGU juu mbinguni na amani kwa watu aliowaridhia.
BWANA YESU agizo lake ni kwamba tuihubiri injili kwa kila kiumbe hivyo hata kupitia mtandao maelfu ya watu wanaokolewa na BWANA YESU.
BWANA YESU agizo lake ni hili;
 '' Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.-Marko  16:15-16''
Namshukuru MUNGU maana Nimewahi kuwaongoza sala ya toba watu wengi sana hata hesabu siikumbuki ambao tu waliiona namba yangu kwenye masomo yangu mtandaoni.
Nimewahi kwaombea watu wengi hata nikachoka na kuwa nawashauri tu kiroho ili wasaidiwe huko huko waliko kwenye makanisa ya jirani na makazi yao.
Namshukuru MUNGU maana japokua sikuwahi kupata hata Shilingi 1 kutokana na blog lakini BWANA YESU hakunipungukia na agizo lake liko pale pale  akisema ''  ''Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.Yohana 10:16''
Namshukuru MUNGU kwa familia yangu kunivumilia wakati nikiwa katika majukumu ya kuandaa Neno la MUNGU.
Namshukuru MUNGU maana nimeweza kupigiwa simu na watu wakiwemo watumishi ambao hata sijawahi kuwaza wala kuota kama wanaweza kunipigia simu.
Nimewahi kupigiwa simu na watu kutoka mataifa mengi sana ambao wanakijua kiswahili, Isipokuwa Amerika ya kusini tu ila mabara mengine yote nimewahi kupokea simu kutoka huko.
Namshukuru MUNGU maana watumishi wengine kutoka blog zaidi ya 10 wamewahi kuyatumia masomo yangu binafsi kwenye blog zao.



Namshukuru MUNGU maana wachungaji, Maaskofu, Mitume , Manabii na walimu wa Neno wamewahi kunipigia simu na kunipongeza kwa kazi njema.
Kuna watu wengi sana wamewahi kuniambia kila siku ni lazima wasome Blog ya maisha ya ushindi.
Binafsi namshukuru tu MUNGU wa mbinguni na utukufu wote ni kwake.
Namshukuru MUNGU maana hata wanasiasa baadhi wamewahi kunipigia simu na kunipongeza na kunisihi niendelee hivyo hivyo ili kuisaidia hata serikali katika kuwa na taifa lenye kumhofu MUNGU maana kama kuna majambazi wanaokoka basi hakika kuna watu wanapona kutokana na wizi wa hao waliompokea YESU.
Kama kuna wachawi wanaacha uchawi kwa sababu wamekutana na injili basi hakika  kuna watu wanaopona kutokana na madhara ya uchawi.
Namshukuru sana BABA wa mbinguni kwa ROHO wake kuniongoza na kunisaidia ili nitende mema.
MUNGU awabariki sana na kama wewe unayesoma ujumbe huu ni mmoja wa wasomaji wa blog ya Maisha ya ushindi basi kwa niaba ya wengine wengi nakushukuru na nakubariki kwa jina la YESU KRISTO aliye hai milele.
Nina malengo mengi sana kama BWANA atanijalia kupata Pesa na wataalamu waaminifu maana nakusudia kuifanya Blog yangu kuwa Website inayojitegemea na pia nakusudia kuwa na blog Application  ambayo watu watakuwa na uwezo wa kui-Download na kuwa wanapata kila kinachowekwa kwenye blog.
Najua kwa baadae pia nina maono ya kuajiri watu hata 5 ili baadhi ya matukio ya kiinjili yawe yanawekwa wakati wote na kila jumapili kuwe na matukio yote ya kwenye ibada katika kanisa lolote ambao tutapanga kuwepo siku hiyo yaani iwe mzunguko kwa makanisa yote huku tukiweka pia audio na video ya mahubiri ya mchungaji siku hiyo ili injili ile a ibada kupitia maisha ya ushindi Website.
MUNGU awabariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter Mabula.
Maisha ya ushindi blog.
+255714252292.
mabula1986@gmail.com.

Comments

Unknown said…
Amina na ubarikiwe mtumishi! Mungu akujalie haja ya mao wako. hakika tutashinda na zaidi ya kushinda