SIMAMA KATIKA ZAMU YAKO ULIYOPEWA NA MUNGU.

 
Na mtumishi Peter Mabula.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Nakukaribisha tujifunze Neno la MUNGU.
Kila mkristo mcha MUNGU amepewa jukumu la kufanya katika kuusimamisha kusudi la MUNGU.
Warumi 12:4-9 ''Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika KRISTO, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha. Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.'' 
-Kwa kupitia maandiko haya tu machache tunaona kazi 7 ambazo zote zinamhitaji Mteule wa MUNGU kuzisimamia katika kulitimiza kusudi la MUNGU la kuitwa kwake mteule huyo.
-Kuna ambao wamepewa kazi ya unabii.
-Kuna wengine wamepewa huduma mbalimblia.
Kuwa walipewa kufundisha.
-Kuna walioitwa ili kuonya.
-Kuna walioitwa ili kukirimu  watu wengine.
-Kuna walioitwa kusimamiana wengine wameitwa katika kurehemu.
 
Kuna walioitwa wawe manabii kwa mataifa, mfano 
Yeremia 1:5 '' Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.''

Kuna walioitwa ili kuharibu kazi zote za shetani na makundi yote ya mashetani.
Yeremia 51:20 ''Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;'' 

Kuna walioitwa katika kazi ya utume, wengine wameitwa katika kazi ya unabii, wengine wameitwa katika kazi ya uinjilisti, wengine wameitwa katika kazi ya uchungaji na wengine wameitwa katika kazi ya ualimu wa neno la MUNGU.
Waefeso  4:11-12 ''Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa KRISTO ujengwe;''

Kila mteule ameitwa katika kazi fulani ambayo anatakiwa aifanye.
Kila Mteule ameitwa katika kazi ambayo anatakiwa aitende katika zamu yake ya kuishi katika maisha ya wokovu na maisha yote kwa ujumla.
Inawezekana kabisa kuna watu wamepewa kazi moja lakini je kila mmoja anasimama katika zamu yake?
Mathayo 25:15-18,28-29 '' Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. '' 

Talanta ni pesa ambayo unapewa ili uizalishe na kupata faida kubwa.
Inawezekana kabisa kuna waliopewa talanta moja lakini wengine wamepewa talanta 2 na wengine 3 na wengine hata zaidi ya talanta 5 wamepewa. lakini jambo kubwa ni kwamba je kila mmoja anasimama katika zamu yake kama kusudi la MUNGU linavyotaka?

Kila mteule amepewa talanta yake ambayo kupitia hiyo talanta anatakiwa alete faida.
Mfano aliyepewa talanta ya kuhubiri inatakiwa kupitia kuhubiri kwake basi watu waokoke, huko ndio kuizalisha talanta.
Kama umeitwa katika uimbaji basi inatakiwa watu waokoke kupita nyimbo zako, huko ndiko kuizalisha talanta uliyopewa.
Talanta ni karama na ni huduma.
Kuna walioitwa katika talanta ya uimbaji.
Zaburi 33:3-4 '' Mwimbieni wimbo mpya, Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe. Kwa kuwa neno la BWANA lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.''

Ndugu, je wewe umeitwa katika kazi gani?
Je unasimama katika zamu yako kama MUNGU anavyotaka?

Habakuki 2:1  " Mimi Nitasimama Katika Zamu Yangu, Nitajiweka Juu Ya Mnara, Nitaangalia Ili Nione Atakaloniambia, Na Jinsi Atakavyojibu Kwa Habari Za Kulalamika Kwangu". 

 Kumbe Kila Mtu anatakiwa asimame Katika Zamu Yake. 
Kusudi la MUNGU kukuokoa ni ili usimame katika zamu yako aliyokupa wewe.
Ni Zamu Nyingi Zinazungumzwa. 
 Kuna baraka inayotokana na kazi yako njema uliyoitenda katika zamu yako.
Ruthu 2:12 ''BWANA akujazi kwa kazi yako, nawe upewe thawabu kamili na BWANA, MUNGU wa Israeli, ambaye umekuja kukimbilia chini ya mabawa yake.''
-Kuna Watu Wanasimama Sasa Kwenye Zamu Zao Za Maombi. 
-Kuna Watu Wanasimama Sasa Kwenye Zamu Zao Za Kuonya Na Kukemea Dhambi Kama Agizo La MUNGU Lilivyo. 
Kuna wanaotakiwa kusimama katika zamu zao za kuwasaidia watumishi wengine.
Kuna ambao wanatakiwa kusimama katika zamu zao za kusaidia kuipeleka injili.
Kuna ambao wanatakiwa wasimama katika zamu zao ili kuwanunulia wachungaji wao chakula.
Kuna ambao wameitwa katika kutoa sehemu ya pesa zao ili kufikisha injili kule inakotakiwa kufika.
Kila mtu ameitwa katika kazi fulani.
Mithali 14:23 ''Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.''
Je ndugu yangu, wewe umesimama katika zamu yako na unatimiza majukumu yako?

Kila Mtu Anatakiwa Kusimama Katika Majukumu Ambayo BWANA Amempa. 
Jambo mojawapo Biblia inasema siku hizi watenda kazi ni wachache.
Mathayo 9:37 ''Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.''
 
Unadhani kwanini watenda kazi ni wachache?
Ni kwa sababu watu wanashindwa kujua kazi zao na kuna wengine wengi sana wanajua kazi zao lakini hawajui kusimama katika zamu zao.

Ndugu Yangu Jukumu Lako Ni Lipi?
 Je Umesimama Kwenye Zamu Yako?
Ukisikia Neno Zamu Maana yake Ni Jambo La Muda Tu Sio La Kudumu. 
Ndugu, Zamu Yako Isiishe Ukiwa Hujafanya Chochote. 
Itumie Zamu Yako Uliyopewa Na BWANA YESU Maana Kila Mtu Atatoa Hesabu Yake Kwa MUNGU Kwa Yale Aliyoyafanya. 
Wengi Huamka Kipindi Zamu Zao Zimebakiza Muda Mfupi Sana Kuisha. 
Simama Kwenye Zamu Yako Ndugu.
 Zamu Yako Kama Huijui Naomba Ukamuulize Mchungaji Wako Atakusaidia. 
Wote Tumeitwa Kutumika Hata Kama Hatufanyi Jukumu Moja Wote. 
Kuna Wahubiri, Waimbaji, Waombaji, Waalimu N.k
Lakini pia BWANA YESU anasema 
'' Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.-Ufunuo 22:12  ''

 Kila Mkristo amewekwa na MUNGU ili kuujenga mwili wa KRISTO.
Ajabu ni kwamba sio Wakristo wote wanaujua Mwili wa KRISTO kwamba ni kanisa.
Na sio kila mkristo analijua jukumu lake hii la kuujenga mwili wa KRISTO.
Hii ni tafakari kwako mpendwa wangu katika KRISTO YESU.
BWANA yuaja na atamlipa kila mtu sawasawa na kazi na matendo yake.



Kuna ndugu mmoja aliniambia "Wewe Peter utachoka lini kupost Neno"
Nikamwambia wala sitachoka kuhubiri injili maana Injili ni uweza Wa MUNGU uletao Wokovu kwa kila anayemwamini YESU.
Huwa ninafuraha sana pale ninapomhubiri KRISTO maana kuna taji tutapewa watakatifu.

Ushindi kwetu ni lazima.
-Tunafatiliwa sana lakini bado tunashinda.
-Tunazongwa sana lakini BWANA YESU ametushindia.
-Tunasemwa vibaya lakini bado ndio kwanza tunashinda kwa kishindo maana tunaye BWANA YESU.
-Hatuogopi maana tunaye Mfalme wa wafalme YESU KRISTO mwenye uwezo.
-Ninaye YESU tena nimehakikisha maana ni kamanda wangu ndio maana ninashinda vita.

Utukuzwe milele BWANA YESU uliyenipenda hata mimi na kunichagua kuwa wateule wako.

 Ili ukue kiimani, ni lazima sana ujifunze Neno la MUNGU na kulifanyia kazi.
Mojawapo ya kulifanyia kazi neno la MUNGU ni kumtumikia MUNGU katika kazi yako na eneo ambalo amekupa.
Simama katika zamu yako siku zote.
3 Yohana 1:8 '' Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.''

Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke.
Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo yangu mtandaoni.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

0714252292.
mabula1986@gmail.com

Comments