SWALI HILI, NAWAULIZA WAKRISTO WOTE DUNIANI!.

Na Mwl Nickson Mabena

"Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakajibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia". MATENDO 19:1-2
Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu, kuna swali natamani niwaulize WAKRISTO Wote Duniani,
Swali hili, Paulo aliwauliza WAKRISTO wa Efeso, baada kuzunguka huku na huko kwenye Huduma, akafika Efeso, akakutana na Wanafunzi kadha wa kadha, akawauliza,
"Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini",
Wakamjibu "La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia".
Nimekisoma kitabu cha Matendo ya Mitume, kuanzia sura ya kwanza hadi ya mwisho, kitu nilichojifunza zaidi, ni jinsi Kanisa la Kwanza lilivyokua linampa Nafasi kubwa Roho Mtakatifu, tofauti na Sasa,
Ilikua watu wakimwamini Yesu, kinachofuata, ni kujazwa Roho Mtakatifu,
Roho Mtakatifu akajidhihirisha kiutendaji, Na Kanisa lilikua limejaa Nguvu za Mungu kubwa sana!.

Wanafunzi hao wa Efeso, walikua hawajawahi kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu, walichokua wanakijua wao kuna Yesu tu, pengine walikua wanaimba kila siku,
Bahati nzuri Paulo, alipofika na Kuwauliza, walikua wawazi na wakamwambia iliyo kweli, kwamba Hatujawahi kuzisikia hizo habari.
Nahisi, angewauliza watu wa Sasa, wangeanza kumpinga kwanza,
Naona ubishani wa Kidhehebu ungezaliwa bila muafaka wowote....
YESU ALIONA ULAZIMA WA KANISA KUWA NA ROHO MTAKATIFU, NDIO MAANA ALIWAAMBIA WANAFUNZI MANENO HAYA;
"Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje, ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache." MDO 1:4-5
Maneno hayo, yalimfanya Paulo awaulize lile swali, maana alijua, lazima watu waliomwamini Yesu, wawe na Roho Mtakatifu!.
Makanisa Mengi sana, HAWAJAWAHI KUSIKIA KWAMBA KUNA ROHO MTAKATIFU!!.
Wanaenenda kwa taratibu za kawaida zilizozoeleka, Wakati huohuo hawana NGUVU ZA MUNGU!.
Paulo alifanya hivi,
"Na Paulo alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri." MDO 19:6

Wakakubali, wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakanena kwa Lugha, wakatabiri!.
NILIPOYASOMA HAYO, NIKATAMANI KUWAULIZA WAKRISTO WOTE, KAMA PAULO ALIVYOWAULIZA WATU WA EFESO,
JE! ULIMPOKEA ROHO MTAKATIFU ULIPOAMINI!??.
NAJUA, JIBU UNALO, SIJUI KAMA LINAFANANA NA LA WATU WA EFESO, AU LIPO TOFAUTI.......
.....Amen, amen...
Bwana Akubariki sana!!.
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments