UTAFICHWA NA MAPIGO YOTE YA ULIMI.

Na Mtumishi Peter Mabula.
MAOMBI MAKALI YA LEO.


Ayubu 5:21 ''Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.''

BABA katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ninatubu dhambi zangu zote na uovu wote ambao nimekosea mbele zako.
Naomba neema na Rehema zako ninapoenda kuomba maombi haya ya vita.
Neno lako linasema ''Nitafichwa na mapigo ya ulimi  wala nisiogope maangamizo yatakapokuja maana hayataniweza kwa jina la YESU KRISTO.''
Ninafuta kila pigo la ulimi lililotamkwa na maadui zangu, ninafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Ninafuta kila pigo la ulimi lililotamkwa juu ya uchumba/ndoa yangu, ninafuta kwa jina la YESU KRISTO.
Ninafuta kila pigo la ulimi lililotamkwa na maadui zangu, ninafuta kwa jina la YESU KRISTO.
Ninafuta mapigo ya ulimi juu ya kazi yangu na juu ya nyumba yangu.
Ninafuta kila pigo la ulimi juu ya afya yangu, ninafuta kwa jina la YESU KRISTO.
Anayenitamkia mabaya, hayo ni mapigo ya ulimi na ninayafuta yote kwa jina la YESU KRISTO.
Anayenitamkia kuachika, hayo ni mapigo ya ulimi na ninayafuta yote kwa jina la YESU KRISTO.
Imeandikwa ''Nitafichwa na mapigo yote ya ulimi''
Kila ulimi uliotamka mabaya kwangu, hayo ni mapigo ya ulimi na ninayafuta kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyenitamkia kutokufunga ndoa, ninafuta mapigo yake yote ya ulimi kwa jina la YESU KRISTO.
Kila pigo la ulimi lililotamkwa na wachawi juu yangu ninafuta kwa  damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila pigo la ulimi lililotamkwa na waganga wa kienyeji juu yangu ninafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
BWANA sasa anaenda kunificha na kila pigo la ulimi kutoka kwa wanadamu na kutoka kwa majini.
Kila pigo la ulimi juu yangu ninalifuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyetamka kwamba sitapata kazi, ninafuta mapigo yake yote ya ulimi juu yangu, ninafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila pigo la ulimi kwa ajili ya ukoo wangu, ninafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila pigo la ulimi juu ya familia yangu na watoto wangu, ninafuta mapigo hayo ya ulimi kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila pigo la ulimi juu yangu halitafanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Kama kuna mapigo ya ulimi ambayo bado yananikamata, kuanzia leo natangaza kuwa huru kwa jina la YESU KRISTO, Ninafuta mapigo yote ya ulimi yaliyotamkwa tangu utotoni mwangu, ninafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Natangaza ushindi kuanzia leo na natangaza kushinda mapigo yote ya ulimi.
Kila ulimi uliotamka laana kwangu nafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila ulimi uliotamka laana juu ya kazi na maisha yangu, ninafuta kwa damu ya YESU na kwa jina la YESU KRISTO.
Imeandikwa katika Ayubu 5 Msitari wa 21 kwamba ''Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.''
Kuanzia leo mimi nafichwa na kila pigo la ulimi maana yake hakuna neno baya litakalotamkwa ili linipate, maana kuanzia leo niko huru mbali na mapigo yote ya ulimi kwa jina la YESU KRISTIO.
Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuniweka mbali na mapigo ya ulimi.
Ninakushukuru MUNGU BABA kwa kunipa ushindi mkuu kuanzia leo.
Ni katika jina la YESU KRISTO Ninaomba na kupokea.
Amen Amen.

MUNGU akubariki kwa kuomba maombi hayo ya imani.
Nakutakia ushindi mkuu na nakuomba ili kutunza ushindi wako hakikisha unajiunga na kanisa la kiroho na ishi maisha matakatifu kuanzia leo ndipo utashangalia maana kila atakayekulaani atakuwa anajisumbua bure maana wewe utakuwa kulaaniki.
Ubarikiwe sana.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
mabula1986@gmail.com.
0714252292

Comments